Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Dkt. Shein mgeni rasmi uzinduzi wa mbio za Mwengi wa Uhuru mkoani Ruvuma

$
0
0

 

3
Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akishaurina na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushotoi)  na Waziri wa Uwezeshaji , Ustawi wa Jamii , Vijana ,wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Zainabu Omary Mohamed(kulia) leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015, utakaozinduliwa tarehe 29.4.2015 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
4
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa Mkuu wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga(kulia) leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015 ,utakaozinduliwa tarehe 29.4.2015 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
6a
Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (katikati)akiongea na waandishi wa habari leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015 utakaozinduliwa tarehe 29.4.2015 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
8
Kikundi cha sanaa cha Mlale JKT mkoani Ruvuna kikitumbuiza leo mjini Songea wakati wa mazoezi ya mwisho ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2015 ,utakaozinduliwa tarehe 29.4.2015 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.(Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO-Songea).
Na Frank Shija, WHVUM
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2015 ambazo Kitaifa zinafanyika Mkoani Ruvuma.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waizri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara wakati wa mazoezi ya ya mwisho yaliyofanyika katika Uwanja wa mpira wa Majimaji mjini Songea.
Waziri Fenella amesema kuwa maandalizi yameenda vizuri na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika sherehe hizo za uzinduzi wa mbuio za Mwenge na kutoa hamasa zaidi kwa Vijana wotye nchini kushuhudia uzinduzi huo ata kwa vile utaonyeshwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya Taifa (TBC).
“Nisema tu kuwa maandalizi yamekwenda vizuri sana mmejionea vijana wa Halaiki walivyo onyesha umahiri wao, niwatate tu wakazi wa mjini wa Songea mjitokeze kwa wingi kuja kushuhudia sherehe hizi za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru lakini pia VIjana nchini kote shuhudieni tukio hili muhumu kwa kuwa litaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa TBC” Alisema Dkt.Fenella
Aidha Waziri Fenella alitoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika zoezi a kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura na baadaye watumie demokrasia kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2015 zinazindulia rasmi tarehe 29 Aprili 2015 mkoani Ruvuma na kilele chake kitakuwa tarehe 14 Oktoba mkoani Dodoma ambapo mbo hizo kwa mwaka huu zimebeba kauli mbiu ya “Tumia Haki yako ya Kidemokrasia” Jiandikishe na kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Mwenge huo wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa katika halmashauri 168 za mikoa 30 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles