Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Asya Idarous, Gusagusa Min Band ndani ya Uingereza kufanya maonyesho Mei 2 na 3

$
0
0

11169017_958488377518759_1048095244_n

Bana ya shoo hiyo ya Gusagusa Min band na Asia Idarous Khamsin itakayofanyika nchini Uingereza.

London, Uingereza

Mbunifu wa mavazi nchini ‘Mama wa Mitindo’, Asia Idarous Khamsin yupo nchini Uingereza akiwa ameambatana na magwiji wa muziki wa taarab kutoka Tanzania, Gusagusa Min Band ambao watafanya maonyesho makubwa ndani ya miji ya nchi hiyo ikiwemo London na Northampton.

Kwa mujibu wa wandaaji wa shoo hiyo nchini humo, Kampuni ya Didas Entertainment ya Uingereza walieleza kuwa, shoo ya kwanza itakuwa Mei 2, katika viunga vya mji wa London na shoo  nyingine ni Mei 3 katika mji wa Northampton ambapo kutakuwa na fashion shoo ‘Divas Catwalk’  itakayopambwa na Mama wa Mitindo, Asia Idarous.

“Gusagusa Min Band na Mama wa Mitindo, Asia Idarous, Tayari wapo ndani ya viunga vya Uingereza na wapo kamili kwa shoo kabambe Mei 2 ndani ya Empire Suite, London na  shoo ya Mei 3, ndani ya Academy, mji wa  Northampton.  Gusagusa ipo full band nzima ikijumuisha wapiga vyombo wao” ilieleza taarifa hiyo kutoka Didas Entertainment.

Aidha, katika safari hiyo, Asia Idarous ameongozana na wadau wengine wakiwemo Mkurugenzi wa Gusagusa Mind Band,  Hasan Farouk,  gwiji wa taarab, Bi Afua Suleiman (muimbaji), Bi Mwanahawa Ally (muimbaji), Jaffer bhai (muimbaji), Khamis Chizi (master keyboard ) na Abdulla Ngonda (mpiga base) na wengineo wengi.

11178372_957991814235082_5347065811729573025_n

 Mama wa Mitindo, Asya Idarous Khamsin (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Gusagusa Min Ban, Achun Baa  na Hamis chizi ‘Master keyboard’  ndani ya viunga vya Milton Keynes UK (Uingereza).

Didas Entertainment imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za burudani ikiwemo kupeleka wasanii kutoka Tanzania na kupiga shoo nchini Uingereza pamoja na shughuli zingine za Sanaa ikiwemo filamu, wasanii wa filamu na uandaaji wa filamu, ambapo hadi mwaka huu imeweza kutimiza miaka 10, tokea kuanzishwa kwake.

11009174_10152877662767684_2829549992663885067_n

Asia Idarous na waimbaji gwiji.

11188171_957971547570442_5616187021648209676_n

Asya Idarous ndani ya pozi kweney viunga vya Milton Keynes United kingdom

11178232_10152886994017684_7247829965855112253_n

Kwa kuweka oda ya kupata tiketi ndani ya UK, whatsapp +447556171941 kwa ku reserve tables

With Didas fashions and Mwanahawa ally

Asya Idarous na  Didas fashions pamoja na Mwanahawa Ally

1375172_10152872390352684_5056457734253432038_n

Achuu Baa meneja wa Gusagusa akiwa ndani ya ndege wakati wa kuwasili kwake ndani ya UK tayari kwa shoo hiyo Mei 2 na Mei 3.

11149355_842666905806201_697106551785747428_n

Gusagusa Mind Band ndani ya UK wakiwa kamili na wenyeji wao.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles