Mwandishi Mkuu wa Mbeya Yetu, blogger Joseph Mwaisango akiwa yupo kitandani Hospitali ya Rufaa Mbeya ambaapo amelazwa tokea jana akisumbuliwa na tatizo la tumbo.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Mtandao wa Modewji blog unamtakia uzima na unafuu Mwandishi Mkuu wa Mbeya Yetu Blog, Joseph Mwaisango ambaye jana Aprili 4, alilazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, kutokana na maradhi ya tumbo yanayomsumbua.
Modewji blog na wadau wetu wengine munaendelea kuperuzi nasi kila siku, tuna kila sababu ya kumuombea mwenzetu Mungu amsaidie ili arejee katika majukumu yake ya kila siku katika kutuhabarisha habari kupitia blog.
Aidha, siku ya leo Aprili 5, Joseph Mwaisango akiwsa kitandani Hospitali ya rufaa ya Mbeya anapoendelea na matibabu, alitumia wasaha wa kuwatakia siku kuu njema watu wote wakiwemo wasomaji wa http://mbeyayetu.blogspot.com/ na ndugu jamaa na marafiki.
“Nawatakia Pasaka njema bado naendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa Mbeya” alieleza Joseph Mwaisango kupitia ukurasa wake wa kijamii wa facebook, mapema leo.
Mwaisango akijuliwa haali na familia yake pamoja na baadhi ya wandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya,