Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Sikika yakanusha taarifa ya upotoshaji wa mswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015

$
0
0

Sikika

Naomba nifafanue kuhusu propaganda inayoenezwa na maafisa wa TCRA kupitia CloundsFM kuhusu Sikika na Mswada wa ‪#‎CyberCrimeBill.

Sikika haikuhudhuria mkutano wa wadau unaodaiwa kufanyika Dodoma kama ilivyodaiwa na  Mh Peter Serukamba na leo maafisa wa TCRA.

Sikika haikutoa maoni kuhusu Mswada wa miamala ya kielektoniki kama ilivyodaiwa na Mh Peter Serukamba na pia leo maafisa wa TCRA.

1.Mkurugenzi wa Sikika, Irenei Kiria (kulia) picha ya Maktaba ya mtandao.

Sikika ilituma maoni ya pamoja ya wadau kwa niaba ya wadau kuhusu #CyberCrimeBill kwa njia ya email kwa Mkiti Kamati Mh Peter Serukamba.

Maoni hayo hayakutumika kuboresha #CyberCrimeBill bali kuongeza tu orodha ya wadau wanaoda iwa “kushiriki” kwa lengo la kuonesha kuridhia.

Kwa kuwa maoni ya wadau hayakuzingatiwa na kwamba ‪#‎CiberCrimeBill iliyopitishwa ina mapungufu mengi, Sikika na wadau bado wanaipinga.

Mwisho tunaomba jina la Sikika lisiendelee kutumika kuhalalisha upitishwaji wa sheria hii.

Irenei Kiria

Mkurugenzi wa Sikika


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles