Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe akiweka shada la maua sehemu ya kumbukumbu ya watu waliokufa kufuatia shambulio la Bomu la Nyuklia katika mji wa Hiroshima mwaka 1945. (Picha na Jiji Press/AFP).
Baadhi ya watoto wakiwa wameshika taa wakati wa kuwaombea watu waliokufa katika mlipuko huo nchini Japan.
Japan imefanya kumbukumbu ya miaka 68 tangu kutokea shambulizi la bomu la Nuklia katika eneo la Hiroshima.
Watu wapatao 50,000 wamehudhuria kumbukumbu hiyo ambapo walikaa kimya kwa dakika moja kutowa heshima kwa maelfu ya watu waliouwawa katika tukio hilo la kihistoria lililoshuhudiwa mwaka 1945.
Mashambulio mengine ya silaha ya bomu la Nuklia yalishuhudiwa siku tatu baadae katika eneo la Nagasaki nchini humo, katika mwaka huo huo ambapo maelfu ya wajapan zaidi waliuawa, hatua iliyoifanya nchi hiyo kusalimu amri katika vita vya pili vya dunia.
Waziri Mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe akiwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria kumbukumbu hiyo amesema nchi yake kama mhanga pekee wa shambulio la bomu la Nuklia ina jukumu la kutafuta njia za kumaliza uwepo wa silaha hizo.