Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

SuperSport yaja na burudani kemkem za ligi mbambali za soka katika msimu mpya unaoanza mwezi huu.

$
0
0

DSC_0895

Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar kuhusiana na msimu mpya  wa  ligi za soka katika SuperSport. Wengine katika picha kutoka kushoto ni  Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Furaha Samalu Meneja Mauzo Salum Salum pamoja na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi.

DSC_0882

Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema DStv imezidi kusogeza huduma kwa wateja wake ambapo hivi karibuni imefungua tawi jipya  Kariakoo barabara ya Msimbazi na kuongeza kuwa kuanzia sasa Channel ya SuperSport itakuwa ikionekana katika eneo lote la kusini mwa jangwa la Sahara.

DSC_0898

Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu  (kushoto) akizungumza na wanahabari ambapo amewataka wananchi kujiunga na huduma za DStv kwani bei zake ni nafuu na picha zake zinaonekana katika kiwango bora.

Kama mtu ni mteja aliyeunganishwa na DStv, sasa atapata msisimko zaidi akisikia kuwa kuanzia mwezi huu wa Agosti SuperSport’s football itawaletea mambo mengi na mazuri zaidi.

Katika msimu mpya, SuperSport itawaletea michapo yote inayohusu soka la Uingereza kwa sasa ambapo kocha mtata Jose Maurinho amerejea katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Kama vile hiyo haitoshi pia Bundesliga itakuwa ikionekana katika SuperSport pekee katika eneo lote la Kusini mwa Jangwa la Sahara itakuwa ni ligi nyingine itakasisimu katika msimu mpya.

Kwa sasa Ligi hiyo ndio inayopewa kiwango cha juu barani Ulaya kufuatia mafanikio ya timu za Bayern Munich na Borussia Dortmund katika msimu uliopita wa michuano ya Ligi ya UEFA na sasa wanatamba kuwa na moja ya meneja mwenye mafanikio katika kipindi cha miaka mitano Pep Guardiola.

SuperSport ni mahali pekee kutazama ligi mbalimbali za soka.

Ligi hizo ni pamoja na English Premier League (EPL), Spanish La Liga, Italian Serie A, German Bundesliga, UEFA Champions League, UEFA Europa League, South African Premier Soccer League (PSL), Kenya Premier League (KPL), Uganda Super League (USL), Nigerian Premier League (NPL), Angolan Girabola, Ghana Premier League, Zambia Premier League na CAF Champions League.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles