Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

“Wajengeeni watoto utamaduni wa kusoma vitabu” – Mama Salma Kikwete

$
0
0

DSC_0002

MKE wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akizindua rasmi Tamasha la kwanza la vitabu vya watoto sambamba na kampeni ya usomaji yenye kauli mbiu ‘Mpe Kila Mtoto Kitabu’  kwenye uzinduzi uliofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Damas Makangale, MOblog Tanzania

MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete amewataka walezi na wazazi nchini kuwanunulia vitabu watoto wao ili kuwajengea utamaduni wa kupenda kujisomea vitabu vya ziada na kiada ili kukuza uelewa wao.

Akizungumza kwenye Tamasha la kwanza la vitabu vya watoto na uzinduzi wa kampeni ya usomaji yenye kauli mbiu ‘Mpe Kila Mtoto Kitabu’ jijini Dar es Salaam leo, Mama Kikwete amesema kwamba wazazi na walezi wana jukumu kubwa la kuwafunda watoto wao kupenda kujisomea vitabu kwa maslahi yao.

“ni muhimu kwa jamii kutambua kwamba msingi wa elimu kwa binadamu yeyote ni kupenda kusoma hasa kusoma vitabu ili kuongeza uelewa na maarifa katika kukabiliana na maisha ya kila siku,” amesema Mama Kikwete

Aliongeza kwamba hapa nchini Tanzania wadau katika tasnia ya vitabu wamekuja na tamasha nzuri lenye jukumu la kuhamasisha watoto umuhimu wa kusoma vitabu na kupanua wigo wa upatikanaji wa vitabu vya watoto nchini.

Mama Kikwete alifafanua zaidi kwamba katika kuandaa vitabu vya watoto ni lazima wadau katika tasnia vitabu kufanya kila jitihada kushirikisha kikamilifu watoto wakati wa uandaaji wa vitabu hapa nchini.

DSC_0336

Mama Salma Kikwete akiwanyanyua wanafunzi kujibu maswali baada ya kuwasomea kitabu cha Hadithi cha “TABU WA TAIRE” katika sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu kwa wanafunzi wa Shule za Msingi katika Mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makubusho ya Taifa.

Amesema wazazi na walezi wana jukumu kubwa la kuwahimiza watoto kusoma vitabu na kuwasomea vitabu vya hadithi ili kuwajengea hamu ya kujua kusoma na kupenda vitabu.

“vitabu ni njia muhimu ya kupata maarifa na kujiendeleza, kutokana na vitabu tunajifunza mbinu na utaalamu mpya wa kufanya kazi zetu za maendeleo. Uzoefu na ugunduzi wote uliowahi kufanywa na mwanadamu unaweza kupatikana kwa kujisomea,” amesema Salma Kikwete

Aliongeza kuwa ni muhimu kwa serikali, taasisi za umma na wadau mbalimbali kuanzisha maktaba za shule na za jamii pale ambapo hazipo na kuziendeleza zilizopo.

Kwa upannde wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Taasisi ya E&D ya Usomaji na Maendeleo, Mama Demere Kitunga amesema kwamba madhumuni ya tamasha ni kutoa fursa kwa umma wa watanzania kujadiliana kuhusu vitabu vya watoto.

“vitabu vya watoto kwa maana ya mawanda, upatikanaji na mvuto; pamoja na kuimarisha majukwaa na mitandao ya kuwezesha upatikanaji wa vitabu vya kujisomea na kuhimiza usomaji kwa watoto,” amesema Mama Kitunga

Amesema kwamba tamasha hilo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yenye dhamira ya kimataifa ‘Haki ya Ushiriki: wapeni Watoto Fursa ya Kuonekana na Kusikika,’

DSC_0350

Wanafunzi na wageni waalikwa kwenye sherehe za uzinduzi huo.

Mama Kitunga amesema kwamba tamasha hili ni la kwanza la aina yake kufanyika hapa nchini, licha ya kwamba juhudi nyingi zimefanywa na wadau wa tasnia kuongeza upatikanaji wa vitabu vya watoto.

Amesema kwamba katika siku za karibuni, mitaala rasmi ya shule imekuwa ikihimiza usomaji wa vitabu vya ziada kuliko ilivyokuwa huko nyuma, hata hivyo mahusiano ya ngano na simulizi zao nyingi zimeingia kwenye hadithi.

Mama Kitunga alifafanua zaidi kwamba tamasha hilo linajipanga kuwashirikisha watoto katika uandishi wa hadithi za kubuni ili kukuza vipaji vya watoto wangali wadogo kuweza kuwajengea uwezo wa kusoma na kuandika siku za usoni.

Aliongeza kwamba lengo linguine ni kupanua wigo wa upatikanaji wa vitabu vyenye viwango vya juu vya ubora na vinavyovutia watoto ili kuhamasisha wazazi, waelimishaji na watendaji katika tasnia ya vitabu kuona fursa ya kuzalisha vitabu bora kwa watoto.

DSC_0229

Baadhi ya wanafunzi wakisimulia hadithi za vitabu kwa njia ya maigizo kwenye uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto uliofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar leo.

DSC_0252

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax Mabula, Mgeni rasmi Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete ,Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Soma, Demere Kitunga na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi (aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa) wakifurahia moja ya hadithi za vitabu zilizokuwa zikisimuliwa kwa njia ya maigizo na baadhi ya wanafunzi mbalimbali shule za msingi kwenye Tamasha la kwanza la vitabu vya watoto na uzinduzi wa kampeni ya usomaji yenye kauli mbiu ‘Mpe Kila Mtoto Kitabu’ jijini Dar es Salaam leo.

DSC_0309

Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha hilo.

DSC_0320

DSC_0346

DSC_0480

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi mtoto Edda Kasika kutoka Shule ya Msingi Maktaba tuzo kwa kushika nafasi ya pili katika uandishi wa insha katika Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa tamasha la vitabu kwa watoto.

DSC_0502

Mmoja wa watunzi wa vitabu vya hadithi vya watoto akipokea tuzo kutoka kwa Mgeni rasmi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

DSC_0523

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi washindi wa insha na mchapishaji wa vitabu bora vya watoto na wageni waalikwa mara baada ya kuzindua rasmi tamasha la vitabu vya watoto wa shule litakaloambatana na warsha ya siku mbili  kwa wanafunzi mbalimbali kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

DSC_0530

Mgeni rasmi Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha wageni kuashiria uzinduzi wa kijiwe cha usomaji utakaombatana na warsha ya siku mbili ikiwemo mafunzo mbalimbali ya uchoraji, uuzwaji wa vitabu mbalimbali, kambi ya kujisomea  kuhamasisha kampeni ya “Mpe Kila Mtoto Kitabu”.

DSC_0540

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia vitabu mbalimbali vyenye hadhi za watoto mara baada ya kuzindua rasmi Tamasha la Vitabu vya watoto lililoandaliwa na Taasisi ya E&D ya usomaji na Maendeleo-Soma kwa ushirikiano na Afrikultur ya Sweeden na kufadhiliwa na Swedish Institute (SI).

DSC_0579

Mama Salma Kikwete akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi wakati akiondoka  mara baada ya uzinduzi huo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles