Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all 5755 articles
Browse latest View live

SIMU TV: Uchambuzi wa magazeti ya leo July 26

$
0
0

Untitled

Simu tv: Mbowe hashikiki, avuna kura za “Ndiyo” 269 sawa na asilimia 98. Pata habari kamili katika dondoo za magazeti hapa Simu.Tv; https://youtu.be/pTiAWaYdabo

Simu tv: Urais UKAWA wafunikwa na wingu jeusi. Pitia uchambuzi wa habari zilizopewa vipaumbele katika magazeti ya leo July 26,2015; https://youtu.be/hB2GaEQxuVI 

Simu tv: Yanga yasema hatuzuiliki, yahaidi kipigo kwa Khartum ya Sudan Kusini. Pata habari za michezo kama zilivyoandikwa katika magazeti ya leo;https://youtu.be/ronOqozU5h0  

Simu tv: Mbunge wa CCM mkoani Iringa amwaga chozi baada ya kung’olewa  viti maalum licha ya kukalia kiti hicho zaidi ya miaka 10;https://youtu.be/sRZ5xl0NcoE


Madaktari wa Marekani wawafunda wanachuo wa Chuo Afya Zanzibar

$
0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar Ndg. Adila Hilal Vuai, akiutambulisha Ujumbe wa Madaktari Diaspora kutoka Washington walioletwa na Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Washington  wakali walipofika katika Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar walipofika hapo kutowa Elimu ya Afya ya Saratani ya Matiti na Mano, wakiwa Zanzibar kwa uwenyeji wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washinton Ndg. Iddi Sandaly akiutambulisha Ujumbe wa Madaktari 17 Diaspora, waliofika Zanzibar kutoa Tiba ya Maradhi ya Saratani ya Matiti, Kisukari na Meno akitowa maelezo wakati walipofika katik Chuo cha Elimu ya Afya Mombasa Zanzibar, na kutowa Elimu ya kutambua Saratani ya Matiti kwa Kinamama. na kutowa huduma ya uchunguzi wa Meno.

Rais wa Jumuiya ya Wanawake Afrika Washington (Africa Women’s Cancer Awareness Association ) Dr Ify Anne Nwabukwu, akiutambulisha ujumbe wa Madaktari wa maradhi mbalimbali waliowasili Zanzibar kwa ajili ya kutowa huduma kwa wananchi wa Zanzibar ikiwa ni kusaidia Wafrika wenzao walioko Afrika.

Rais wa Jumuiya ya Wanawake Afrika Washington (Africa Womens Cancer Awereness Association ) Dr Ify Anne Nwabukwu, akiutambulisha ujumbe wa Madaktari wa maradhi mbalimbali waliowasili Zanzibar kwa ajili ya kutowa huduma kwa wananchi wa Zanzibar ikiwa ni kusaidia Wafrika wenzao walioko Afrika.

Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakimsikiliza Dr. Ify akitoa maelezo na kuwatambulisha Madaktari Diaspora aliofuatana nao.

Dr Ify Anne Nwabukwu akitowa Elimu ya tambua viashiria vya Saratani ya Matiti kwa wanafunzi hao wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.

Dr Ify akitowa mada kuhusiana na Saratani ya Matiti kwa Wanafunzi wa Chuo hicho hutoa Elimu ya Udaktari wa aima mbalimbali chuoni hapo.

Dr Ify akionesha Mashine ya kupimia Saratani ya Matiti ya Kisasa inayoitwa Mama Gram hutumika kucunguza viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Wanachuo hao wakati akitowa Elimu ya Saratani ya Matiti jinsi ya kumgundua Mwanamke mwenye matatizo hayo.

             Wanafunzi wa Chuo hicho wamepata fursa ya kuuliza mswali wakati wa Mafunzo hayo.

Mmoja wa Madaktari hayo akitoa mfano hai kutokana na matatizo ya Saratani ya Matiti, kwa Wanachuo hao.

Daktari wa Meno Bi Queenate Ibeto akitoa elimu ya kutunza meno na kinga ya mane kwa Wanafunzi hao jinsi ya kuyatunza meno. wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho.

Daktari wa Meno Venessal Quitero akionesha moja ya tiba ya kunusuru meno kwa wanafunzi hao wakati wakitowa Elimu ya Utunzaji wa Meno na tiba yake.

Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar akionesha mafunzo ya utunzaji wa Meno kwa vitendo jinsi ya kupiga msuwaki inavyotakiwa kuweza kuimarisha meno kuwa imara.

Dr Queenate Ibeto akionesha mfano ya vitendo kwa mmoja wa mnafunzi wa Chuo hichi jinsi ya utumiaji wa msuaki katika kupiga kwa Wanafunzi hao, wakati walipofika kutoa Elimu ya Afya kwa Wanafunzi wa Chuo hicho Mombasa Zanzibar.

Profesa Hailu na Dr Quintero wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwakilishwa kuhusiana na Saratani ya Matiti na Tiba ya Meno, kwa Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar Mombasa wakati walipofika katika Chuo hicho wakiwa Zanzibar kwa ajili ya kutoa Tiba ya Saratani ya Matiti Ugonjwa wa Kisukari na Meno.

Dr Quintero ni mtaalamu ya Magonjwa ya Meno akifafanua moja ya swali lililoulizwa na Wanafunzi wa Chuo hicho.

Mwanafunzi wa chuo hicho akiuliza swali kuhusiana na baadhi ya Wananchi meno yao huwa na ukungu mweusi kwa wataalam hao.

Madaktari wa Diaspora wakigawa misuwaki na dawa za meno kwa wanafunzi hao baada ya kutowa Elimu chuoni hapo.

Dr Silvia Dasi akitowa maelezo kwa wanafunzi hau jinsi ya kumgundua mwanamke mwenye Matiti ya Saratani ya Matiti wakati wakifanya mafunzo hayo kwa wanafunzi hao wanaochukua Elimu ya Afya ya binadamu.

Dr Silvia Dasi akitowa maelezo kwa wanafunzi hau jinsi ya kumgundua mwanamke mwenye matiti ya Saratani ya Matiti wakati wakifanya mafunzo hayo kwa wanafunzi hao wanaochukua Elimu ya Afya ya binadamu.

Dr Ify  akitowa Elimu ya Vitendo kugundua viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Mwanamke akitowa mafunzo hayo ya mmoja wa mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.

Dr Ify akitowa Elimu ya Vitendo kugundua viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Mwanamke akitoa mafunzo hayo ya mmoja wa mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar kulia Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar Ndg Adila Hilal Vuai.

Madaktari Diaspora wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar baada ya kutoa Elimu kwao.

Dr. Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho.

Dr. Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho.

DR Queenate Ibote akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakati walipofika Chuoni hapo kutowa Elimu kwa Wanachuo hicho.

Madaktari wa Diaspora wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar wakiwa nje ya jengo la Chuo hicho katika Skuli ya Sekondari ya SHAA Mombasa Zanzibar.(Picha na OthmanMapara.Blog  Zanzinews.Com).

Okoa hela ya matangazo ya karatasi, pata tovuti ya .tz na tzNIC!

$
0
0

Maranyingi wafanya biashara hufikiria kutangaza biashara zao magazetini, kwenye mabango, vipeperushi na kadhalika. Wafanyabiashra huamini kwamba njia hizi hufikia watu wengi. Je ni kweli kwamba matangazo ya karatasi hufikia walengwa wengi? Kama mfanyabiashara na mtangazaji, unajuaje kuwa tangazo lako limefikia walengwa wangapi na kwa wakati gani?

matangazo

Kwa kutumia tovuti, unaweza kujua ni watu wangapi wanao tembelea tovuti yako, na wanatembelea kwa muda gani. Kwa kujua ni watu wangapi wanaotembelea tovuti yako, utaweza kujua pia ni watu wangapi nje ya mkoa na nchi wanaopata ujumbe wa biashara yako. Kwa kujua kwa muda gani walitembelea tovuti yako, utaweza kujua kwamba ni watu wangapi waliovutiwa na biashara yako.

Hasara ya kutumia matangazo ya karatasi ni kwamba ukomo wa maisha yake ni mfupi. Siku ikiisha tu, gazeti hilo na matangazo yaliyopo ndani yanakua hayana umuhimu. Matangazo ya bandiko pia hua na maisha mafupi. Mvua ikinyesha, karatasi yako inaloana. Mtu anaweza pia akaibandua, au hata kuweka bandiko ya biashara yake juu ya lakwako.

TzNIC ni kampuni ya kiTanzania ambayo imerahisisha usajili wa tovuti za kibiashara na za kibinafsi. Kusajili tovuti yako kwa bei rahisi, sajili jina la kampuni au biashara yako au hata kama ni mtu binafsi kabla mpinzani wako kibiashara hajasajili! Kwa maelezo Zaidi tembelea kurasa za TzNic hapa chini

Website; http://www.tznic.or.tz/

Facebook; https://www.facebook.com/tznic

Twitter; https://twitter.com/tznic

Fastjet kuanza ‘route ya 5’ leo ni ya Dar- Lilongwe (Malawi)

$
0
0

DSC_0480.jpghhhMeneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati akifafanua jambo kwa waandishi (hawapo pichani) wakati wa mkutano maalum na wanahabari akielezea namna fastjet inavyotanua safari zake katika nchi za Afrika, mkutano uliofanyika hivi karibuni Unguja-Zanzibar wakati wa tamasha la 18, la filamu za nchi za majahazi maarufu ZIFF, ambapo fastjet pia ni wadhamini kwa miaka miwili mfululizo (Picha na Andrew Chale wa modewjiblog).

Na Andrew Chale, modewjiblog

(Dar Es Salaam) Shirika la ndege la Fastjet  limeendelea kupanua wigo wake kwa kuanzisha safari zaidi ikiwa ni kuunganisha Afrika kuwa moja kupitia safari za anga kwa gharama nafuu kabisa ambapo asubuhi ya leo  wanatarajia kuizindua rasmi ‘route’ hiyo ambayo inakuwa ni ya tano ya kutoka Dar es Salaam-Tanznaia kwenda Lilongwe-Malawi.

Awali akielezea kwa wandishi wa habari, Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati alipokutana Zanzibar wakati wa tamasha la 18, la filamu za nchi za Majahazi maarufu ZIFF ambapo pia Fastjet ni wa zamani kwa mwaka wa pili mfululizo, alibainisha kuwa maar azote shirika hilo linakuja na huduma bora na kwa gharama nafuu kumsaidia mteja kufanikisha mambo yake mbalimbali kupitia usafiri wa anga.

Anasema kuanzishwa kwa ‘route’ hiyo ya Lilongwe (Malawi), fastjet ipo  pia mbioni kufikia nchi zingine ndani ya Afrika na kwa sasa ipo katika mchakato huo na baadae wataweza kutangaza rasmi huku akiwataka wateja kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono katika juhudi hizo za usafirishaji wa anga.

“Tunajisikia furaha kuweza kusogeza huduma zaidi wateja waliokuwa wakitumia muda mrefu kusafiri kutumia usafiri mwingine kuelekea Malawi, sasa wamepata mkombozi Fastjet ambayo itakuwa ikiruka mara mbili kwa wiki Jumatatu na Ijumaa!… kwa gharama nafuu kabisa” alieleza Kibati.

Kwa upande wake, Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro  anasema tayari watu mbalimbali wameweza kuchangamkia ‘route’ hiyo ya kuelekea Malawi kwani itaendelea kuunganisha watu wote karibu huku ikitoa fursa kwa wafanyabiashara, wanafunzi, shughuli za kiserikali, michezo pamoja na zingine nyingi ikiwemo za kifamilia.

Awali Fastjet ilianzia na safari za ndani za kusafirisha abiria ‘route’ za Mwanza – Dar, Kilimanjaro – Dar na Mbeya – Dar na baadae kuweza kuvuka mipaka zaidi kwa nchi za Afrika kwa ‘rout’ kati ya Dar – Johannesburg (Afrika Kusini), Dar – Lusaka (Zambia), Dar – Harare (Zimbabwe), Dar – Entebbe (Uganda) na kwa sasa hii inayozinduliwa leo Julai 27, ya Dar-Lilongwe (Malawi).

Afisa huyo, anaeleza kuwa, Fastjet itaendelea kutoa huduma bora kupitia usafiri wa anga huku akisisitiza kuwa ‘route’ mbalimbali zikiwa mbioni kufikiwa na shirika hilo.

Want to take your business to Malawi’s thriving capital city?ggNow you can. Our new international route connects Lilongwe with Dar es Salaam every Monday and Friday with fares available from just Tsh 237,600/$99 (Tsh 120,000/$50 fare, plus Tsh 117,600 tax/$49 gov.taxes).

Tickets are on sale now with flights departing from 27th July, so save yourself the hassle of a long drive and fly further for less with fastjet.com

bMeneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati katika mahojiano na wanahabari..

kibatiMeneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo..

fastjetMuonekano wa moja ya  ndege za fastjet kwa ndani…

Unesco kuendelea kusaidiana na Tanzania kuinua elimu

$
0
0

IMG_8896

Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma.

IMG_8887

Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia  elimu.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco  nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.

Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT  wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.

Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama  na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.

Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu ambavyo vitaingizwa.

IMG_8817

Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.

Yusuph aliwataka wadau wanaoshiriki katika kongamano  ambalo lilitarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki kutekeleza wajibu wao kwa makini kwa kuwa Watanzania wanasubiri maelekezo yao kufanikisha utoaji wa elimu ya Tehama yenye kuleta mwelekeo mpya wa matumizi kwa kulenga  kuvumbua na kutumia elimu kwa manufaa ya taifa.

Alisema UNESCO ipo tayari kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha wanafunzi ambao watakuwa na uwezo mkubwa katika Tehama ambao utaibua maendeleo endelevu.

 “Si kutoa walimu wazuri tu bali kuwezesha jamii , wanafunzi na waliopitia mafunzo hayo kuwa na namna mpya ya kufikiri na kuvumbua vitu vipya vya kujiendelea na kuendeleza taifa” alisema Yusuph.

Alisema kimsingi elimu inatoa asilimia 5 lakini maisha yanatoa asilimia zilizobaki kama mtu atatumia vyema msingi wa maarifa aliyopewa.

IMG_8793

 Jaco Du Toit, kutoka ofisi za Unesco kanda ya Nairobi akiendesha majadiliano ya maboresho ya vipengele mbalimbali vya waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu”UNESCO ICT Competency Framework for Teachers in Tanzania” wakati wa kongamano hilo lililomalizika mwishoni mwa juma mjini Bagamoyo.

Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.

Naye Mratibu wa kitaifa wa Mradi Wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo alisema kongamano hilo ni sehemu ya maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara katika vyuo vya Monduli na Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha mafunzo na ufundishaji.

“Leo tuko hapa Bagamoyo kwa ajili ya wadau kudiscuss ICT draft document (kujadili hati hii yenye draft ya mafunzo) ambayo ilipitiwa na watu  watano kabla ya kuikabidhi kwa Wizara ya Elimu “ alisema Faith.

IMG_8775

Alifafanua kwamba Mradi huo ambao awali ulifadhiliwa na  Benki ya Dunia na kukamilika mwaka 2011, haukuridhiwa kutumika hadi mwaka jana ulipokuja mradi wa CFIT ambao uliingizia upitiaji upya wa mradi huo na kuwezesha kuridhiwa kwa matumizi.

Naye  kiongozi wa timu iliyopitia awali katika mradi huo wa CFIT, Profesa  Ralph Masenge amesema wataalamu waliohusika na upitiaji huo kabla ya kongamano walitoka Chuo cha Ualimu Tabora na kile cha Monduli,Chuo kikuu huria Tanzania  na Chuo kikuu cha Dar es salaam.

Alisema awali walipitia kuona mahitaji maalumu ya walimu kisha wakaja na mapendekezo ambayo sasa yanafanyiwa kazi .

Alisema matatizo mengi ya elimu Tanzania yanatokana na uhaba wa vifaa vya elimu  na ubora wa walimu.

Alisema mradi huo utasaidia kutoa elimu bora kwa kuwa na walimu bora na vifaa bora kupitia Tehama.

Alisema mradi huo utasaidia  kuwezesha Tehama kutumiwa kama chombo cha kutumia wanafunzi hasa pale panapokosekana.

Profesa Masenge alisema hatua waliyofikia ni hatua ya matayarisho na kwamba ni matarajio yao kwamba wakishafikisha  hati hiyo kwa wizara masuala ya matumizi ya maabara yatakuwa yamekamilika.

IMG_8849

Pichani juu na chini ni washiriki wakiwasilisha mawazo yao wakati kongamano likiendelea kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha waraka huo.

IMG_8798

IMG_8821

IMG_8787

Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa.

IMG_8842

IKULU yakanusha taarifa ya gazeti la Mwananchi inayodai “Rais Kikwete analipwa Dola za Marekani 192,000 kwa mwaka”

$
0
0

Untitled

Gazeti la Mwananchi la leo, Jumatatu, Julai 27, 2015, kwenye ukurasa wake wa 26 limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Marais watano wanaotajwa kuongoza kwa mishahara minono barani Afrika ni hawa hapa”.

Katika habari hiyo ambayo gazeti hilo linadai chanzo chake ni “uchambuzi wa mtandao wa African Review” inadaiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, anashilikia nafasi ya tano miongoni mwa viongozi 38 wa nchi za Afrika wanaolipwa mshahara mnono zaidi.

Gazeti hilo linadai kuwa Rais Kikwete analipwa Dola za Marekani 192,000 kwa mwaka, ikiwa ni malipo ya Dola za Marekani 16,000 kwa mwezi.

Habari hizi siyo za kweli. Ni uongo na uzandiki. Ni uzushi mtupu na ni uzushi wa hatari.

Mshahara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwezi ama kwa mwaka haufikii na hata wala kukaribia kabisa kiwango kinachotajwa na Gazeti la Mwananchi.

Tangu Uhuru, mwaka 1961, Rais wa Tanganyika na baadaye tangu mwaka 1964 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa miongoni mwa viongozi wanaolipwa mishahara ya chini kabisa duniani.

Mshahara wa Rais wa Tanzania kwa mwezi ni wa chini kiasi cha kwamba mshahara wake unazidiwa, tena kwa mbali, na mishahara wanayolipwa baadhi ya watendaji wakuu wa baadhi ya taasisi za umma nchini.

Aidha, ni jambo la kushangaza kwamba Gazeti la Mwananchi, linalochapishwa hapa nchini, linaweza kupata kiasi cha uongo anacholipwa Rais wa Tanzania katika mitandao ya nje badala ya kuuliza rasmi na kupewa majibu sahihi.

Kwa kujiingiza katika uzushi wa kupindua kiasi hiki, Gazeti la Mwananchi haliwezi kuwa na nia nyingine yoyote isipokuwa nia ya kuwachochea wananchi na kuwajengea chuki dhidi ya Serikali yao na Kiongozi wao Mkuu.

Ni matarajio yetu, kuwa Gazeti la Mwananchi litafanya jitihada za makusudi, kama taaluma ya uandishi wa habari inavyoelekeza, kutafuta usahihi wa jambo hili na kuwaambia Watanzania ukweli.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.

27 Julai, 2015

Vyama vya Siasa 21 vimesaini Maadili ya uchaguzi mkuu Tanzania

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva, akizungumza na wahariri vyombo vya habari Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Julius Mallaba. Picha na Joseph Zablon

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva, Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Julius Mallaba. (Picha na Maktaba).

Vyama vya Siasa 21 vinavyotarajiwa kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani baadaye mwaka huu vimesaini Maadili ya uchaguzi yatakayotumika wakati wa kampeni, kupiga kura na wakati wa kutangaza matokeo.

Maadili hayo yanayohusisha Serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Vyama vya Siasa yalisainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dr. Florence Turuka, Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva na Wawakilishi wa vyama vya Siasa 21 nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume hiyo amesema Chama cha Wananchi (CUF) hakikusaini Maadili hayo kutokana na kuwa na kazi nyingine lakini akasisitiza kuwa Chama hicho kitasaini Maadili hayo wakati wowote.

Akifafanua kuhusu Maadili hayo, Jaji Lubuva alisema Maadili yanapaswa kuanza kutumika rasmi Agosti 22 mwaka huu wakati kampeni za uchaguzi zitakapoanza, katika kipindi cha kupiga kura na wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo.

Alisema Maadili hayo pia yatahusu wajibu wa vyama vya siasa na wagombea na mambo yasiyotakiwa kufanywa na vyama vya siasa na wagombea. Maadili pia yatahusu masuala yanayotakiwa kufanywa na yasiyotakiwa kufanywa wakati wa kupiga kura.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa maadili yaliyosainiwa pia yatahusu maadili kwa Tume ya Uchaguzi yaani mambo yanayotakiwa na yasiyotakiwa kufanywa na Tume hiyo.

Aidha, maadili hayo yatahusu mambo yanayotakiwa na yasiyotakiwa kufanywa na watendaji wa serikali katika kipindi chote cha uchaguzi.

Ndio! Fuso ni Faida imerudi tena!

$
0
0

image 1

Wafanyakazi wa Diamond Motors Limited wakiwapa maelezo mbalimbali watu waliojitokeza katika maonyesho ya Kampeni ya Ndio! Fuso ni Faida iliyoanza 24 julai 2015 jijini Dar es Salaam.

image 2

image 3

image 4

Kampeni ya Ndio! Fuso ni Faida Ilianza kwa kishindo jijini Dar es Salaam na baadae kuelekea mikoa mingine kama vile Tanga, Moshi – Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Kahama-Shinyanga, Dodoma, Iringa, Mbeya, Songea- Ruvuma na mwishowe kuishia Dar es Salaam.    

image 6

image 7

Diamond Motors Limited ni wasambazaji wa magari pekee wanaoongoza nchini Tanzania kwa usambazaji wa Malori aina ya Fuso (MFTBC). Kwa mara nyingine watafanya kampeni ya maonyesho ya Magari yao ijulikanayo kama, Ndio! Fuso ni Faida ambapo kwa Zaidi ya siku  26 mikoa kumi na moja(11)  ilifikiwa na maonyesho haya ambapo waliwaonyesha gari aina ya Fuso FJ na kuitambulisha Fuso FZ;  magari yenye uwezo wa kati na ya uwezo wa juu zaidi ambayo yanafaa zaidi katika shughuli za migodini, kilimo, ujenzi, usafirishaji wa vifaa na mizigo.

Wakati wa maonyesho hayo yaliyoanza mnamo tarehe 24, Julai 2015 jijini Dar es Salaam, malori haya yalikuwepo kwaajili ya majaribio ya kuendesha wakati wa maonyesho.

Timu ya wafanyakazi wa kitengo cha mauzo pamoja na ufundi walisindikiza magari haya wakati wa maonyesho ya siku 26 ndani ya mikoa 11 na maonyesho haya yaliapita katika miji mikuu na wilaya. Malengo na madhumuni ya maonyesho ilikuwa ni kuleta karibu wateja wake katika mikoa husika na kuwaonyesha ufanisi na uwezo wa magari haya uliowaletea manufaa katika uzalishaji wa kibiashara. Kampeni ya Ndio! Fuso ni Faida Ilianza kwa kishindo jijini Dar es Salaam na baadae kuelekea mikoa mingine kama vile Tanga, Moshi – Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Kahama-Shinyanga, Dodoma, Iringa, Mbeya, Songea- Ruvuma na mwishowe kuishia Dar es Salaam.    

Kwa siku 26, za Kampeni ya Ndio! Fuso Ni Faida,  ilionyesha jinsi magari haya yalivyo na uwezo wa kupita katika barabara mbovu na kuonyesha uwezo wake na uimara wa kuhimili barabara hizi.

Wakati wa utambulisho wa gari jipya, Fuso inatarajia kukuza kiwango chake kwa mara nyingine. Magari yote haya yena uwezo wa kati na ya uwezo wa juu yaliyo na kitako kilicho na msingi wa teknolojia ya malori ya Daimler pamoja na Mercedes-Benzi pamoja na kibini iliyohusishwa na teknolojia mpya ya 6S20 injini ya diseli na uwezo wa 6,373cc, uzalishaji wa nguzu ya 170kW(810Nm)/205kW pamoja na mwendo wa  6 mpaka 9 wa mwongozo maambukizi. Kitako cha malori haya yametengenezwa kwaajili ya mizigo mizito, ili kuwapa wateja faida zaidi.

Kila lori la Fuso limekaguliwa na kujaribiwa vizuri na kwa ujumla magari ya Fuso yametembea takribani umbali wa kilometa milioni tisa (9). Malori haya yametengenezwa kwa kutumia teknolojia ya juu duniani na vifaa na uhandisi wa kisasa kabisa wa Kijapani na Kijerumani pamoja na teknolojia ya juu ya injini za diseli.

Magari ya Fuso yametengenezwa ili kumpa mtumiaji faida ya juu kabisa kwa kuwa na gharama rahisi kabisa za uendeshaji ambayo inatoa chaguo sahihi kwa biashara  sahihi. Usalama ni kigezo kingine muhimu kwa magari ya Fuso, Fuso imeendelea kuendeleza vipengere vya usalama kuwalinda madereva, wasafiri na watumiaji wengine wa bara bara. FJ iliyo na muundo wa Aerodynamic, inaruhusu uboreshaji siyo tu wa umbali wa kutembea lakini pia kupunguza kelele ndani ya kibini pamoja na uchovu kwa madereva. Pia ina kifaa maalumu kwaajili ya kuzuia mafuta kwenye miteremko na hivyo kuongeza umbali wa kutembea kwa mafuta kidogo.  Mwendo ambukizi wa tisa (9) kwa gari za mwendo mdogo, inatoa nafasi ya mabadiliko ya gia kuendana na hali ya barabara hasa zilizo mbaya. Vifaa vya mwendo ambukizi kwa nguvu ya kuondokea na  kusambaza  nguvu katika vifaa vingine ni vya viwango vinavyowezesha lori la Fuso FJ kuwa na ubora wa kufanya kazi katika sekta za ujenzi na uchimbaji madini.  

Utoaji mdogo wa hewa chafu kwa mazingira ni ushahidi kuwa Fuso wamejizatiti na uvumbuzi wa teknolojia zinazo tunza mazingira. Lori la Fuso ni uhakika wa uwekezaji wa muda mrefu kwa matengenezo yanayofuata kwa kulinganisha na magari ya washindani, uimara wa vipuri na mahitaji madogo ya matengenezo.

Diamond Motors Limited, (Hansa Group), ni wasambazaji pekee wa magari ya Mitsubish Fuso (MFTBC) nchini Tanzania, mahusiano haya yanayoendelea kukua kati ya kampuni hizi yamewezesha mshikamano kwaajili ya kuendelea kujizolea sifa na kudumisha kiwango cha juu kabisa cha bidhaa na utoaji wa huduma nzuri.  Ikimilikiwa kwa ushirikiano wa Daimler na Mitsubish, malori ya uwezo wa kati pamoja na ya uwezo mkubwa yanatengenezwa katika viwango vya hali ya juu kabisa.

Kwa kushirikiana na kampuni za kimataifa yanayotengeneza bidhaa za magari ambapo wamejenga ushirikiano wa nguvu na kampuni zinazoongoza kidunia kama vile mabasi aina ya Mitsubishi kutoka Japan, matairi ya Yokohama kutoka Japani na MTU kutoka Ujerumani imewezesha Diamond Motors Limited kuwa na uwanja mpana wa wateja kutoka sehemu mbali mbali duniani ambayo imewezesha kukuza secta ya magari nchini Tanzania kufikia kiwango cha juu.

Nia na madhumuni ya kampeni kupitia barabara ya  Ndiyo! Fuso ni Faida ni kudumisha mahusiano imara yaliyopo kati ya kampuni  na wateja na pia kujenga mahusiano mapya na wateja, hii itatoa fursa kwa wateja kuonana moja kwa moja na maafisa mauzo wetu pamoja na timu ya ufundi ambapo watabadilishana taarifa na kuwapa muongozo juu ya bidhaa zetu,  ambapo itawapa wateja nafasi ya kuelewa vema faida za kumiliki gari aina ya Fuso.

Diamond Motors Limited, msambazaji pekee wa magari aina ya Fuso inatambulika katika sekta hii ya magari kwa kutoa huduma bora wakati wa manunuzi na hata baada ya manunuzi kufanyika. Kwa kuzingatia ubora wa karakana za kampuni ya Fuso, wamiliki wa magari wanahakikishiwa muendelezo wa thamani ya magari yao  kwa miaka inayofuata. Maonyesho haya ya barabarani yatatoa fursa kwa wateja kupata nafasi ya kuona, kukagua na kugusa magari haya.


Advanced technology increasingly shaping Africa’s financial sector

$
0
0

sumesh_rahavendra

Sumesh Rahavendra, Vice President of Sales for DHL Express Sub Saharan Africa.

dhl_logo2

The African financial services industry is rapidly evolving as a result of advancing technology which is fueling innovation and growth in the sector. While the sector is mature in most developed countries, it is less saturated in Africa, therefore offering many opportunities for new market entrants to challenge the status quo of how business has traditionally been conducted.

This is according to Sumesh Rahavendra, Vice President of Sales for DHL Express Sub Saharan Africa (http://www.dpdhl.com) who adds, “The burgeoning middle class and abundance of SMEs in Africa present great opportunities for financial services companies to provide retail banking services to individuals, as well as trade finance to SMEs. We see SMEs as the engine for growth in Africa and the lack of access to finance can often hinder their development. With one of the fastest growing middle classes in the world, there is a wave of consumerism for all types of goods and services such as FMCG, electronics and pharmaceuticals.”

The future shape of financial services in Africa 2015(1) report by PwC describes the sector as a marketplace without boundaries. It explains that compared to global markets – where the outlook for financial services is more solid – the risk of disruption in traditional African financial services market has triggered the need for entities to reassess their strategies.

“While most international banks are moving towards e-commerce, in Africa, a number of local banks still share information and conduct business with hard copy documentation,” adds Rahavendra.

An Accenture report titled African financial services come of age(2), suggests a promising future for the region’s banking sector. It reveals that the development of consumer payment networks took years to become fully functional in mature economies, while many countries in Africa are now beginning to expand their traditional payments infrastructure to adapt to new international standards.

“The local retail banking sector is increasingly making use of new technology such as ‘Mobile Money’ platforms. Consumers have started to move away from physical cards, instead relying on their mobile phones to conduct day-to-day banking transactions.”

“In addition to mobile money solutions, most African countries have made a concerted effort to improve their transactional security by moving from the traditional ‘swipe card’ form of retail banking to chip and pin.”

“From a logistics point of view, while banking sector documents continue to present significant shipment volumes intra-Africa, with the new technologies available, there is an increased need for equipment such as servers, ATMs and supplies to be moved into and around the continent, as banks expand into new countries and rural areas. As technology and requirements change, so do our supply chains, and we work very closely with our customers to ensure that we offer them the best possible solutions.”

“The financial sector fueled DHL’s expansion into Africa in 1978 when global banks needed to get documentation to Africa, and it continues to help shape our service offerings on the continent as the sector matures. As the only logistics company to be present in every country and territory in Africa, we not only have front row seats to witness the impressive growth of the sector, but are fortunate enough to work with some of the largest and emerging financial institutions on the continent and play our part in their growth story,” concludes Rahavendra.

GEN, Entrepreneurs’ Organization, Elumelu Foundation Join Forces to Spark Global Entrepreneurship

$
0
0

spark_obama

President Barack Obama with co-founders of the Global SPARK coalition, Jonathan Ortmans, CEO of the Global Entrepreneurship Network; Tony O. Elumelu, CON, Founder of the Tony Elumelu Foundation; and Sriram Bharatam, Chairman, Africa Growth Initiative, (EO); during the Global Entrepreneurship Summit in Nairobi, Kenya, over the weekend.

An impressive collection of organizations have come together to answer President Barack Obama’s call at the Global Entrepreneurship Summit yesterday in Nairobi, Kenya, to advance entrepreneurship and economic growth around the world.

Representatives of the Global Entrepreneurship Network (GEN), Entrepreneurs’ Organization (EO) and Tony Elumelu Foundation (TEF) participated in a formal signing ceremony at the Summit, committing to lead the Spark Global Entrepreneurship initiative. Spark is a coalition that is seeking to mobilize like-minded organizations, companies and investors that collectively generate more than $1 billion dollars in private investment for emerging entrepreneurs by the end of 2017.

“The world is full of nascent entrepreneurs with brilliant ideas—but they need stronger ecosystems to help them unleash those ideas and grow them into game-changing startups,” said Jonathan Ortmans, president of Global Entrepreneurship Network and one of three Spark coalition co-chairs. “Spark increases coordination and collaboration among startup support programs and amplifies their efforts.”

The first wave of companies that have stepped forward include Citi, EY, GE, Google and IBM. Two African companies, Rendeavour, the continent’s largest urban land developer, and SkyPower, the largest provider of utility-scale solar power projects in the world, have joined as well.

“African entrepreneurship has been the missing link in Africa’s development. The actions of just one entrepreneur sends ripples across a community and entrepreneurship lifts people permanently out of poverty and creates social wealth,” said Tony Elumelu, founder of the Tony Elumelu Foundation. “We all know entrepreneurship, anywhere in the world, is not easy nor is success guaranteed. All stakeholders – the private sector, governments, NGOs and donors – must make a commitment to use their respective powers to address the hurdles facing African entrepreneurs. That is what Spark is all about.”

Spark taps into the growing involvement of government programs in helping entrepreneurs start and scale new firms.

U.S. Vice President Joseph Biden announced the Spark initiative at the 2014 Global Entrepreneurship Summit in Morocco and outlined the commitments of some of the most active and effective U.S. government programs such as the Presidential Ambassadors for Global Entrepreneurship, Young African Leaders Initiative, African Women’s Entrepreneurship Program and more.

Spark is asking for commitments from organizations and individuals willing to “start the spark” by collaborating and contributing resources, networks, data and ideas to multiply efforts and help founders start and scale new firms.

“We are excited to leverage our in-market presence in nearly 50 countries to support Spark, inspire today’s entrepreneurs and foster the next generation globally,” said Vijay K. Tirathrai, CEO of Entrepreneurs’ Organization. “Our organization provides numerous platforms to bring entrepreneurs together for enhanced learning and leadership growth. Spark is a natural extension of our commitment and we call on others to join us and affect positive change through entrepreneurial support.”

To join Spark, visit www.startthespark.org.

Kampuni ya Tigo yazindua minara Mkoani Geita

$
0
0

utepe (2)

Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa(aliyevaa suti)akikata utepe kuzindua mnara mpya wa mtandao wa Tigo katika Kijiji cha Ilolangulu Wilayani Mbogwe Mkoani Geita.

maelezo ya Mashauri (1)

Meneja Masoko wa Tigo kanda ya Ziwa Ali Mashauri (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa,alipofika kuzindua mnara mpya katika Kijiji cha Ilolangulu Wilayani Mbogwe.

RC na wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa,akiongozana na wananchi kuondoka baada ya kuzindua mnara wa Tigo katika Kijiji cha Ilolangulu Wilayani Mbogwe.

wakazi wa ilolangulu (2)

Wakazi wa Kijiji cha Ilolangulu Wilayani Mbogwe Mkoani Geita,wakimsikilza Mkuu wa Mkoa huo Fatma Mwassa,wakati wa uzinduzi wa mnara mpya wa mtandao wa Tigo.

Magazeti, majarida na vitabu vyote kwenye simu yako ya mkononi

$
0
0

Je umekwishawahi kukwama kwenye foleni ukajutia kutobeba gazeti walau likusaidie kusogeza muda mbele? Je umekwisha wahi kutafuta chanzo cha habari za uhakika kwenye simu yako ukakikosa?

Je umekwishawahi kuambiwa kuna tangazo la kazi au tenda ila ukashindwa kuliona kwa vile lipo kwenye gazeti la siku za nyuma?

Je umeshawahi kulazimika kuchoma au kutupa magazeti ya siku za nyuma kwa sababu yamejaa sana nyumbani kwako? Au je umeshawahi kuhisi kuna umuhimu wa kuona watoto wako wanachojifunza shuleni?

Je umekwishaona maktaba inayokupa magazeti, majarida au vitabu vyote toka tulipopata uhuru, mahali popote wakati wowote ulipo?

Kama jibu la swali lolote kati ya hayo ni ndio, basi M-Paper inaweza kukupa hayo yote.

Kabla hatujaendelea, tazam video hii ya sekunde thelathini tu hapa chini.

M-Paper ni programu ya simu za mkononi, inayokuletea magazeti, majarida na vitabu vyote kwenye simu yako ya mkononi.  Programu hii ya kipekee itakufanya usome gazeti, jarida au kitabu chote kama kilivyo kwenye makaratasi na si vichwa vya habari pekee.

Kama hiyo haitoshi, watengenezeji wa programu hii watakupa shilingi 10,000 pale utakapodownload app hii ambayo utaitumia kununua magazeti, vitabu na majarida kabla hujaanza kutumia pesa zako.

Oh, jambo jingine la kipekee kuhusu program hii ni kuwa, magazeti, majarida na vitabu vyote vinauzwa kwa nusu bei. Faida mara mbili.

Unaweza kudownload app hii hapa http://www.mpaper.co.tz kisha ukaniandikia maoni yako hapa chini, umeionaje? Kumbuka unadownload BURE, unawekewa 10,000 kwenye akaunti yako hivyo huna cha kupoteza.

mPaper 1 (1)

mPaper 2

mPaper 3

Kampeni za Udiwani ndani ya CCM Kata ya Magomeni zaanza kwa kishindo

$
0
0

ANDKatibuu Mwenezi wa CCM Kata ya Msasani, Bw. Andrew Mangole (kulia) akiwaomba wana CCM kuachana na makundi na  baadala yake wakijenge chama katika misingi imara na kuibuka na ushindi hapo baadae katika uchaguzi Mkuu. (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog).

Na Andrew Chale, modewjiblog

(Magomeni-Kinondoni) Kampeni za kura za maoni kwa wagombea Udiwani ndani ya Cha Cha Mapinduzi (CCM) zimepamba moto ambapo kila mgombea amejitokeza na kujinadi mbele ya wanachama ili achaguliwe kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu hiyo Oktoba mwaka huu.

Kata ya Magomeni kwa nafasi ya Udiwani ndani ya CCM inawaniwa na Makada wane akiwemo aliyekuwa Diwani wa Kata ya Magomeni ambaye anatetea kiti chake,  Dk. Julian Bujugo. Wengine wanaowania katika uchaguzi huo ni pamoja na Nurdin Butembo, Gardiner Dibibi na Sadique Bwanga.

Awali wagombea hao walianza upande wa Magomeni Makuti ndani ya Kata hiyo ya Magomeni  kwa kujinadi kwa Wanachama wa CCM na kisha kuhamia upande wa Magomeni Mapipa ndani ya Ofisi za CCM Kata.

Kwa upande wake mgeni mwalikwa ambaye ni Katibuu Mwenezi wa CCM Kata ya Msasani, Bw. Andrew Mangole aliwaomba wagombea wote wanne kuzingatia maadili ya chama na wagombea kujinadi bila kukashifiana ilikukijenga chama

“Tufanye kampeni kistaarabu. Wagombea wote wazuri na munasifa ndani ya chama ila hapo Agosti Mosi kura zitakazopigwa anatakiwa mmoja tu ashinde na wengine mutakuwa bora zaidi ila kura hazitowatosha ila kwa watakao kuwa kura hazijatosha muendelee kuungana na chama kuleta ushindi wa kishindo” alieleza Katibu Mwenezi huyo Mangole.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Kata Magomeni,  Shaweji aliimiza umoja na ushirikiano kwa wana CCM wote kuakikisha wanaleta ushindi ndani ya chama na nje ya Chama kwa Kata hiyo kuwa chini ya CCM kuendeleza maendeleo ya Kata hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Magomeni CCM, Sadique Kudulo alieleza kuwa CCM ni chama tawala hivyo kitaendelea kuongoza dola kwa  misingi thabiti huku akiwataka wana CCM kutofanya makosa kwa kuchagua mgombea atakaye kiuza chama na kisha kuibuka kidedea katika uchagui hapo baadae.

Aidha, wagombea wote wameweza kujielezea kwa wana CCM kwa kujinadi na kisha kuomba kupigiwa kura hiyo tarehe 1.8.2015. ambapo katika uchaguzi huo wa ndani anatakiwa mgombea mmoja tu apaatikane na kisha jina lake kupelekwa ngazi ya juu ya chama na kisha kurejeshwa baada ya kujadiliwa kwa kina ili kusimamishwa kugombea katika uchaguzi hiyo Oktoba.

SHAWEDMwenyekiti wa CCM Kata ya Magomeni, Shaweji akisisitiza jambo katika mkutano huo wa kampeni  za udiwani ndani  ya  CCM

ANDERKatibuu Mwenezi wa CCM Kata ya Msasani, Bw. Andrew Mangole  akitoa akitoa nasaha zake kwa wana CCM (Hawapo pichani).

bujugo2

bujugoAliyekuwa Diwani wa Kata ya Magomeni ambaye anatetea kiti chake katika Kata hiyo,  Dk. Julian Bujugo akijinadi kwa wana CCM leo Julai 28.2015 Katika ofisi za CCM Kata.

bwangaPICHA ya Juu na chini: Mgombea wa nafasi ya Udiwani kupitia CCM ndani ya Chama hicho, Kijana Sadique Bwanga akiomba kura kwa wana CCM waliojitokeza katika kampeni hizo za ndani zilizofanyika leo Julai 28.2015 katika ofisi za CCM Kata.

bwanga44..Naombeni kura zenu mimi mtoto wenu wazazi wangu!!

gurdinawPICHA ya Juu na chini: Mgombea wa nafasi ya Udiwani kupitia CCM ndani ya Chama hicho, Kijana  Gardner Dibibi akiomba kura kwa wana CCM waliojitokeza katika kampeni hizo za ndani zilizofanyika leo Julai 28.2015 katika ofisi za CCM Kata.

gudina…naomba kura yenu.

mgomba3PICHA ya Juu na chini: Mgombea wa nafasi ya Udiwani kupitia CCM ndani ya Chama hicho, Bw. Nurdin Butembo akiomba kura kwa wana CCM waliojitokeza katika kampeni hizo za ndani zilizofanyika leo Julai 28.2015 katika ofisi za CCM Kata.

mgombea….Napiga magoti  naombeni kura zenu.!

SADIMwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Sadique  akitoa sisitiza wana CCM kuwa kitu kimoja pamojana kuepuka kampeni za matusi ilikukijenga chama .. wakati wa tukio hilo la kampeni za ndani..

wanacgaaSehemu ya wanachama wakiwa ndani ya mkutano huo wa kampeni za ndani.

Bodi ya mikopo ilivyoshiriki maonesho ya vyuo vikuu Jijini Dar Es Salaam

$
0
0

HESLB TCU 1

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipokea maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutoka kwa Ofisa wa HESLB Bi. Veneranda Malima katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (Picha na HESLB).

HESLB TCU 2

Ofisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa ELimu ya Juu (HESLB) Bw. Saleko Mandara (kushoto) akimwelekeza namna ya kujaza fomu ya kurejesha mkopo Bw. Suleiman Zidi Hisabu ambaye ni mwajiriwa wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Zanzibar na mnufaika wa mkopo aliopewa na HESLB. Bw. Hisabu alitembelea banda la HESLB katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (Picha na HESLB).

HESLB TCU 3

Mkurugenzi wa Elimu ya Juu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sylvia Temu akimkabidhi Ofisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Veneranda Malima cheti cha ushiriki katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

HESLB TCU 4

Ofisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Joyce Mgaya (kulia) akijibu maswali ya Bi. Dorah Kusiri, mkazi wa jijini Dar es Salaam kuhusu huduma za HESLB. Bi. Kusiri alitembelea banda la HESLB katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

HESLB TCU 5

Ofisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa ELimu ya Juu (HESLB) Bi. Joyce Mgaya (kulia) akimwelekeza Bw. Sheha Semtawa (aliyekaa) namna ya kujaza fomu ya kuomba mkopo kwa njia ya mtandao. Bw. Semtawa alitembelea banda la alitembelea banda la HESLB katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mwisho wa kuwasilisha maombi ya mkopo ni Julai 31, 2015. (Picha na HESLB).

 

REA kuhusisha sekta binafsi pamoja na benki nchini ili kuongeza kasi ya usambazaji umeme vijijini

$
0
0

PIX 1

Baadhi ya wadau wa Sekta binafsi pamoja na benki zilizopo nchini wakifuatilia ajenda wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) juu ya kuleta maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini.

Na Benedict John-MAELEZO-Dar es salaam

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeadhimia kuhusisha Sekta binafsi pamoja na benki nchini ili kuongeza kasi ya usambazaji umeme Vijijini.

Hatua hiyo itasaidia kuleta maendeleo ya haraka na kufikisha umeme katika maeneo ya vijijini katika maeneo mengi hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava wakati akiongea katika kikao kilichohusisha Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, sekta binafsi pamoja na benki zilizopo nchini.

Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini , kasi ya upelekaji umeme vijijini hapa nchini imeogezeka.

“Baada ya hiki chombo kuingia kazini kasi imeongezeka kwani kwa sasa wananchi waliofungiwa umeme ni zaidi ya asilimia 24 na wakati ule namba ya uwepo wa umeme vijijini ilikuwa asilimia 10 mwaka 2005 ambapo kwa sasa ni karibu asilimia 40 na tunatarajia kuongeza kasi hii kadri tunavyozidi kupata vyanzo vingi vya fedha kwani malengo yetu hapo baadaye ni kuweza kufikia asilimia zaidi ya 70”, alisema Mhandisi Mwihava

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Dkt. Lutengano Mwakahesya ameeleza kuwa kikao hicho kinalenga  kufafanua namna gani sekta binafsi zinavyoweza kupata faida kwa kuingia katika sekta ya nishati pamoja na kushirikia katika kuleta maendeleo ya haraka katika kufikisha umeme kwa asilimia 60 na zaidi.

Amesema kuwa endapo umeme nchini utaenea katika maeneo ya vijijini utaweza kuleta maendeleo makubwa hususani katika kuleta ajira kwa vijana na kuibua miradi mbalimbali kupitia viwanda vidogo vidogo jambo ambalo litapunguza tabia ya baadhi ya watu kukimbilia mijini katika kusaka ajira.

“Maendeleo makubwa yatapatikana iwapo umeme huu utafika vijijini, utasaidia kuleta viwanda vido vidogo kama vile mashine za kukoboa ili ipatikane ajira vijijini na watu waache kuhamia mjini nkutafuta maisha bora kwanbi umeme huu utasaidia wawananchi kuibua miradi mizuri ya maendeleo”. Alisema Mwakahesya.

Ameongeza kuwa, watu wengi hawawezi kulipa shilingi 27,000 hivyo Bodi hiyo inatazamia kuongea na benki za zilizopo nchini pamoja na sekta binafsi ili kuweza kupata njia bora zaidi za kufikisha umeme katika maeneo hayo ya vijijini kwa kuwapa mkopo ambao unaweza kulipwa pole pole kwa kutumia kulipia bili za umeme.

Serikali ilikamilisha mchakato wa uanzishwaji wa Taasisi ya Wakala wa Nishati Vijijini mnamo mwaka 2005 ambapo mwaka 2007 hadi hivi sasa baada ya Wakala kuingia kazini, kasi ya upelekaji ya umeme vijijini imekuwa kubwa.

PIX 2

PIX 3

PIX 4

PIX 5

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wadau wa Sekta binafsi pamoja na benki zilizopo nchini wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) juu ya kuleta maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini .(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).

PIX 6.

PIX 7


CCM kutoa tamko kesho

Mgombea jimbo la Singida magharibi, Wilson Nkhambaku ndani ya CCM aomba kura asema yeye ni jembe

$
0
0

UF3A7791

Mgombea nafasi ubunge kura za maoni jimbo la Singida magharibi, Wilson Elisha Nkhambaku.(Picha na Maktaba).

Na Nathaniel Limu, Puma

MGOMBEA nafasi ubunge kura za maoni jimbo la Singida magharibi, Wilson Elisha Nkhambaku, amesema kuihama CCM mwaka 2010 na kujiunga na upinzani,kitendo hicho kilikuwa ni ajali ya kawaida ya kisiasa.

Amedai kuhama huko na kukaa upinzani kwa muda mfupi,haikuwa tamaa ya kusaka uongozi kama ambavyo baadhi ya watu wanavyofikiria.

Nkhambaku aliyasema hayo wakati alipoulizwa na mwana CCM mkazi wa kijiji cha Puma wilaya ya Ikungi mkoani Singida,kwamba endapo atapewa ridhaa kuwa mbunge wa jimbo la Singida magharibi kwa tiketi ya CCM,hatakihama tena chama kama alivyofanya mwaka 2010.

Akifafanua,alisema zoezi la kura za maoni za CCM 2010 jimbo la Singida magharaibi,wakazi wengi  wa jimboni na wa mkoa wa Singida kwa ujumla,wanafahamu kilichotendeka.

“Mimi kama mtoto wenu….jembe lenu,kibinadamu nilichukizwa sana na kitendo hicho cha kupokwa kura zake.Udhulumaji huo ulichangia nichukue uamuzi wa kuacha njia sahihi”,alifafanua zaidi Nkhambaku.

Kwa ujasiri mkubwa Nkhambaku,alisema baada ya muda mfupi sana,hasira hizo zilitoweka na ndipo alipobaini amekosea njia na mara moja alirejea  njia sahihi nyumbani CCM.

“Trafiki alipopima ajali hiyo ya kisiasa,alitoa majibu kwamba ajali hiyo sikuifanya kwa kusukumwa na tama ya kusaka uongozi kwenye kambi ya upinzani,bali ilisababishwa na watu wengine”,alisema.

Nkhambaku alisema kwa upande wwake rais Kikwete kupitia vyombo vyake,alibaini kwamba ajali hiyo ya kisiasa nilisababishiwa na ndipo alipoamua kumteua kuwa mkuu wa wilaya ya Kishampu mkoani Shinyanga.

“Kwa taarifa yenu sijamwangusha Rais Kikwete, mtoto wenu jembe lenu,pale Kishampu nimetekeleza majukumu yangu kwa ufanisi mkubwa uliopelekea nipewe nishani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Kikwete”,alisema kwa kujiamini.

Nkhambaku ametumia fursa hiyo kuwaomba wana CCM wa jimbo la Singida magharibi wampe kura za kutosha kama njia mojawapo ya kumuunga mkono rais Kikwete kwa kumwamini na kumpa ukuu wa wilaya.

Wagombea wengine walioko kwenye kinyang’anyiro hicho ni Dk.Grace Puja, Samwel Dinawi, Hamisi Lissu Mahanju, Hamisi Ngila, Yona Makala, Dk.Hamisi Mahuna na Elibariki Kingu.

Wagombea hao juzi wamehitimisha zoezi la kampeni kura za maoni na wanatarajiwa kupigiwa kura Agosti mosi mwaka huu.

AUDIO ya mahojiano na Balozi Amina Salum Ali kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU

$
0
0
balozi Amina

Mhe. Balozi Amina Salum Ali akifafanua jambo ndani ya Kilimanjaro Studio.

Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania

Katika kipindi cha wiki hii tumebahatika kuungana na Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali

Karibu

Mmliki wa St. Mathew, St. Mark adaiwa talaka na mgawanyo wa mali

$
0
0

court_gavel

Na Mwandishi Wetu

MDAI katika kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali Magreth Mwangu mkazi wa Mkoani Singida dhidi ya Mkurugenzi wa Shule za sekondari za St.Mathew na St Marks Thadei Mtembei amelalamikia kitendo cha Benki ya CRDB kutoa taarifa zake za benki bila idhini yake wala ya mahakama.

Pia ameilalamikia mahakama ya Mwanzo Kizuiani inayosikiliza kesi hiyo kwa kutumia Wakili wa kujitegemea licha ya kuwa mawakili hawaruhusiwi katika mahakama ya Mwanzo.

Kesi hiyo inasikilizwa na hakimu Rajab Tamaambele.

Wakili huyo amekuwa akimwakilisha mdaiwa ambaye amekuwa hafiki mahakamani tangu kesi hiyo ifunguliwe kwa kile kilichoelezwa wamepata kibali kutoka kwa mwanasheria mkuu wa serikali kinachoruhusu kesi hiyo kusikilizwa na wakili bila mdaiwa kuwepo.

Kwa mujibu wa Mwangu tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani hapo mdaiwa amekuwa hafiki mahakamani na badala yake amekuwa akiwakilishwa na mtoto wake,Peter Mtembei ambaye ni Wakili hali iliyofanya kesi hiyo mpaka inaisha na kufungwa ushahidi mdaiwa akiwa hajasikiliza shahidi hata mmoja.

Hata hivyo Mmiliki huyo wa St, Mathew juzi alifika mahakamani kufuatia amri ya mahakama kufuatia malalamiko ya mdai aliyokuwa akitoa mahakamani kutokana na Mtembei kushindwa kufika kwenye kesi hiyo tangu ilipofunguliwa na  iliyomtaka afike mwenyewe mahakamani hapo na endapo asingefika mahakama ingehamia nyumbani kwake.

Akitoa ushahidi wake, Mtembei alisema alifahamiana na Mwangu wakati akiwa na mfanya usafi katika duka lake la dawa.

Alisema hakuwahi kumuoa mama huyo wala kuishi naye licha ya kuzaa naye watoto watatu.

Alisema mama huyo hana hadhi ya kuwa mke wake kwani ameishia darasa la saba elimu ambayo ni ya chini sana.

“Huyu alikuwa ni mfanya usafi tu ni nesi msaidizi kazi yake ilikuwa ni kufanya usafi na hata kufunga vidonda tu” alisema.

Alisema duka hilo la dawa lilifungwa baada ya kuonekana aliyekuwa analihudumia hana elimu.

Mtembei alisema mdai hana uhusiano na mali alizonazo kwani yeye ana mke wake wa ndoa na huyo alikuwa ni mwanamke tu aliyezaa naye.

“Huyu ni mwanamke tu niliyezaa naye hana haki kwenye mali zangu” alisema

Alipohojiwa na mahakama kama alifunga ndoa na mdai alisema kuwa hajawahi kufunga naye ndoa licha ya kutoa mahari ya Ng’ombe watano. “Nilimpelekea baba yake vindama vitano tu kama zawadi” alisema

Alisema hajawahi kufunga ndoa ya kimila na mdai kama inavyodaiwa na mdai hana haki yoyote katika mali zake.

Kwa upande mwingine mdai alihoji sababu za mdaiwa kwenda Benki ya CRDB na kutoa taarifa za fedha za akaunti yake bila kuwa na amri iliyotolewa na mahakama.

“Mdai kwa kutumia nafasi nzuri ya kifedha aliyokuwa nayo ameweza kwenda benki ya CRDB na kupewa taarifa za fedha kwenye akaunti yangu bila ruhusa yangu au ruhusa ya mahakama jambo ambalo limeniathiri kisaikolojia’ alisema

Hata hivyo hakimuTamaambele alisema hafahamu ni wapi mdaiwa alitoa taarifa hiyo lakini mahakama inaipokea kuwa sehemu ya ushahidi.

Kesi hiyo imepangwa kutolewa hukumu Agosti 25, mwaka huu.

Katika kesi hiyo mdai anaiomba mahakama imuamuru mdaiwa kupa takala,kutoa Sh. Milioni 800 na makazi ya kukaa mdai na watoto wake.

Tigo yazindua Duka Jipya Ifakara

$
0
0

ifakara picha no 1

Katibu Tawala wilaya ya Kilombero ndugu Yahya Naniya akikata utepe ikiwa ni ishara rasmi ya  uzinduzi wa duka la Tigo lililopo Ifakara mjini, kutoka kushoto ni Meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya Pwani, Isack Shoo, Inspekta Dotto Ngimbwa kutoka ofisi ya OCD Kilombero na mwisho kulia  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya mashariki Goodluck Charles.

ifakara picha no 7

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya mashariki, Goodluck Charles akizungumza machache kwenye hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.

ifakara picha no 8

Katibu Tawala wilaya ya Kilombero ndugu Yahya Naniya, akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa duka la Tigo lililopo Ifakara mjini.

ifakara picha no 2

Wafanyakazi wa duka la Tigo lililopo Ifakara mjini wakipozi kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi aliyevaa tai nyekundu ndugu Yahya Naniya ambae ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kilombero, muda mfupi baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa duka hilo.

ifakara picha no 4

Meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya Pwani, Isack Shoo akitoa maelekezo jinsi watakavyo hudumia wateja kwa mgeni rasmi Katibu tawala wa wilaya ya Kilombero ndugu Yahya  Naniya baada ya uzinduzi wa duka hilo lililopo Ifakara mjini.

ifakara picha no 5

Muonekano wa duka jipya kwa wateja wa Tigo lililopo Ifakara mjini.

ifakara picha no 6

Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa duka la Tigo Ifakara mjini ndugu Yahya  Naniya ambae ni Katibu tawala wa wilaya ya Kilombero (wapili kutoka kulia) akiwa katika meza kuu na  Goodluck Charles Mkurugenzi wa Tigo kanda ya mashariki(wa pili kushoto)  Inspekta Dotto Ngimbwa kutoka ofisi ya OCD Kilombero(kushoto) na Meneja wa operesheni kwa wateja Tigo kanda ya Pwani, Isack Shoo (kulia).

Viewing all 5755 articles
Browse latest View live