Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all 5755 articles
Browse latest View live

Cool Things You Didn’t Know You Could Do With Google

$
0
0

If you go to Google Translate, there’s an option where you can manually draw things like Chinese characters, which will then be translated for you into English.

4. Tackle geography trivia.

Untitled 4

 Using the new Google Maps tool Smarty Pins, you can take on Google in a geography trivia game in which you will be asked questions with location-based answers, and you will answer by placing a pin in the world map. You can try just general knowledge or tackle specific categories like science or sport.

7. Discover how popular different words are.

Untitled 7

Using the Google Ngram viewer, you can search more than 5 million books published between 1800 and 2008 to find out how often different words were used, and then compare them on a graph. TIL: For a brief period in the 1830s, elephants were more popular than cats.

9. Find and download loads of cool fonts for free.

Untitled 9

google.com

If you go to Google Fonts, there’s a huge collection of completely free fonts you can use. You can either download them to your computer or make them the default font in your browser.

11. Plan your wedding.

Untitled

Yep, Google even has a comprehensive wedding planner to make sure everything is in place for your special day. It’ll help you do everything from announcing the news of your engagement to finding a venue, making a budget, creating a schedule and guest list, setting up a shareable photo stream from the day, and even making an entire website to keep everything in one handy place.

AD-Amazing-Facts-About-Google-17-1

This hugely interactive site was set up by Google to celebrate The Hobbit films and lets you play your way through five famous battles, follow the stories of your favourite characters (including clips from the films themselves), or simply explore the map itself.

18. Play with Legos.

AD-Amazing-Facts-About-Google-18

Feel like a kid again by going to buildwithchrome.com. You can put up constructions all over the real world using its map function, check out cool stuff other people have already built, or learn to become a master bricklayer with Build Academy.


Ya Moto band, Orijino Komedi wafanya kweli tamasha la ZIFF 2015

$
0
0

DSC_0225Wanamuziki wa bendi ya Ya Moto wakishambulia jukwaa usiku huo…

Na Andrew Chale, modewjiblog

(ZANZIBAR) Kundi la muziki wa kizazi kipya nchini, YAMOTO BAND lenye maskani yake Temeke Jijini Dar es Salaam na kundi la vichekesho la Orijino Komedi ‘OK’   usiku wa Julai 21 wameweza kukonga nyoyo za wadau wa burudani waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la 18, la kimataifa la filamu za nchi za Majahazi (Zanzibar International Films Festival-ZIFF) linaloendelea visiwani hapa.

Katika shoo hiyo iliyojaa kila aina ya burudani, makundi hayo yaliweza kuteka vilivyo kwa kuonyesha kile walichokitaka wadau wa burudani waliojitokeza kwa wingi.

Kundi la OK, lililokuwa na Masanja Mkandamizi, Joti, Mpoki, Wakuvwanga na Mc Legan walishambulia jukwaa kwa kuingiia mmoja mmoja na baadae  kundi hilo la Ya Moto  nao walihitimisha burudani kwa kupiga nyimbo zao mbalinbali mpya na za zamani.

Mbali na makundi hayo pia, usiku huo kulikuwa na burudani kutoka kwa wanamuziki Baraka Da Prince, Chemical,  Kidumbaki  na wengine wengi.

Tamasha hilo lililoanza  Julai 18, linatarajia kufikia tamati Julai 26 mwaka huu huku filamu mbalimbali zikiendelea kuonyeshwa pamoja na burudani ya muziki kila siku katika viunga vya Unguja na Pemba.

DSC_0092Joti na Mc Legan wakishambulia jukwaa..DSC_0114

DSC_0095

DSC_0101

DSC_0104Masanja Mkandamizaji.. DSC_0097Joti..

DSC_0244Dogo Aslay…

DSC_0299

DSC_0234Ya Moto band…

DSC_0183Msanii Baraka Da Princce…. akiimba jukwaani ZIFF 2015

DSC_0131Msanii wa kufokafoka Mwanadada Chemical akishambulia jukwaa la ZIFF 2015

Joshua Nassari achaguliwa kupeperusha bendera ya Chadema Jimbo la Arumeru Mashariki

$
0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Joshua Nassari akizungumza namna alivyotekeleza ahadi zake katika kipindi kilichopita wakati wa mkutano Mkuu wa Jimbo uliofanyika kwenye Mji mdogo wa Usa River ambao  alichaguliwa bila kupingwa ili kupeperusha bendera ya Chadema katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Wanachama wa Chadema wakipiga kura za maoni kwaajili ya kumchagua mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki katika Mji Mdogo wa Usa River, Joshua Nassari alipata kura 387  na kura 2 za hapana.
Wanachama wa Chadema wakifurahia jambo katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini ambaye alikuwaa Mbunge wa Chadema jimbo la Karatu mkoa wa Arusha, Israel Natse (kulia)na Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Kalist Lazaro wakimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (kati) baada ya kutangazwa mshindi.
WanaChadema wakifatilia kwa makini mkutano mkuu wa jimbo ambao pia ulifanya uchaguzi wa wabunge wa viti Maalumu, Rebeca Mngodo aliibuka mshindi wa kwanza kwa kupata kura 62 kati ya wagombea watano.
Wanachama wa Chadema wakifurahia jambo katika mkutano huo Mkuu wa jimbo uliofanyika katika Mji Mdogo wa Usa River.
Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Joshua Nassari (kulia) akizungumza jambo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk. Elly Macha.

 

Pinda akutana na wananchi wa Mlele

$
0
0

IMGL6981 2

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akifafanua jambo kwa kutumia  kompyuta ndogo (Ipad) wakati alipozungumza  na wanafamilia wa Mzee Katinda wa kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele akiwa katika mapumziko mafupi nyumbani kwake  Kibaoni, Katavi julai 22, 2015. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).

IMGL6966

Mke wa Waziri Mama Tunu Pinda  akiwaonyesha picha mbalimbali alizopiga vijana wa kabila la Kisukuma aliokutana nao nyumbani kwa Mzee  Katinda katika kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele  ambako yeye na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wako katika mapumziko mafupi  kijijini Kibaoni.

IMGL6997

Watoto  wa familia ya  mzee Katinda wa  Kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele  wakicheza ngoma ya Kisukuma mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Mheshimiwa Pinda yuko katika mapumziko mafupi kijijini kwake Kibaoni, Katavi.

IMGL6992

IMGL7027

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana  na  wasichana wa Kisukuma  nyumbani kwa Mzee Katinda kwenye kitongoji cha Tupindo wilayani  Mlele  akiwa  katika mapumziko mafupi  nyumbani kwake Kibaoni, Katavi   Juai 22, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Takukuru yamkingia kifua Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma

$
0
0

Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Sipora Liana.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Sipora Liana, akijieleza mbele ya Baraza la  Maadili kwa Viongozi wa Umma Dar es Salaam leo, alipofikishwa kwa tuhuma za kukiuka maadili ya viongozi wa umma alipokuwa Halmshauri ya Manispaa ya Mkuranga mkoani Pwani kabla ya kuhamishiwa Tabora.

 Jaji Msumi (katikati), akiwa na wenzake akisikiliza shauri hilo.

Na Dotto Mwaibale

KAMANDA wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Wilaya ya Mkuranga, Damas Pasalau, amemkingia kifua aliyekuwa Mkurugenzi wa Halamashauri ya Manispaa ya Mkuranga Sipora Liana kwa tuhuma zinazomkabili katika Baraza la Maadili ya Utumishi wa Umma.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa katika vikao vya baraza a maadili vilivyoanza jana jijini Dar es Salaam, Sipora ambaye kwa sasa Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha  anakabiliwa na tuhuma za kukiuka maadili.

Inadaiwa kuwa mnamo mwaka 2009/2010 Sipora alimchukulia hatua za kinidhamu bila sababu za msingi kwa kumsimamisha kazi aliyekuwa Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika Wilaya ya Mkuranga Dk. Fransis Mallya kinyume na sheria ya maadili ya utumishi wa umma.

Pasalaus alitoa utetezi kwa muda wa dakika 30 ambapo kati ya hizo 10 alizitumia kutoa utetezi wakati akiulizwa maswali na Mwanasheria wa Serikali Getrude Cyriacus.

Pasalau ambaye mara kwa mara alibanwa na mwanasheria huyo kwaajiri ya kutoa ushahidi sahihi aliendelea kumtetea huku akitoa mifano mbalimbali na utendaji kazi wake uliofanyika katika Wilaya aliyotoka Sipora huku akidai kuwa ni kitendo hichop ni chuki binafsi hivyo zisiruhusiwe kushika nafasi kwenye mali za umma.

Wakati akitoa ushahidi huo alimtaka Jaji Hamis Msumi kutenda haki na kudai kuwa Mkurugenzi huyo hana kosa bali ni hujuma za baadhi ya watu ambao walikuwa kwa maslahi yao binafsi katika ofisi za Manispaa hiyo.

Alisema awali katika Manispaa hiyo kulikuwa na msuguano kati ya Madiwani, watumishi wa umma na wakurugenzi jambo ambalo baada ya kufanyika kwa uchunguzi na taasisi hiyo ilibainika uwepo wa ubadhilifu wa mali za umma.

“Baada ya Sipora kuwasili katika halmashauri hiyo ambapo katika utendaji kazi wake mzuri watu wengi hawakumpenda kwani wengi wao walikuwa wakifanya shughuli zao kwa maslahi binafsi,” alisema.

Alidai baada ya Mkurugenzi huyo kufika na kuonekana utendaji wake unawabana baadhi ya watu akiwemo Mallya na wenzie waliunda kundi ambalo lilikuwa ni kwaajili ya kupambana nae.

“Watu hawa walitumia vyombo vya udhibiti wa maadili kutunga hoja za uwongo ili kuweza kufanikisha malengo yao.

” Ila kiukweli mwenyekiti huyu mama amethubutu na ameweza kulingana na hali ya mazingira yaliyoko katika halmashauri ile kwatu watendaji wengi hawakupenda watu wa aina hii,” alisema.

Akifafanua zaidi kuhusu tatizo lililotokea hadi hatua za kusimamishwa kazi zilipotokea alidai kuwa baada ya Mkurugenzi huyo kuwasili katika halmashauri hiyo alianza kufuatilia idara ya Mallya katika kukamilisha miradi ya Mabwawa ya Mkwalia pamoja na ununuzi wa vitotozi visivyofanyakazi na kuweka mashamba hewa ambapo hakuwa amefanya kazi yeyote.

Hata hivyo shauri hilo liliahirishwa kutokana na anaedaiwa kuwa ni mlalamikiwa Sipora, kutofika na mashahidi wake kama alivyowasilisha idadi yao katika baraza la hilo.

Akihairisha kikao cha baraza hilo, Jaji Msumi alisema shauri hilo litasikilizwa hadi pale itakapotolewa hati maalum ya wito kwa mashahidi wa Mkurugenzi huyo.

 

 

.

Makamu wa Rais Dkt. Bilal afungua maonesho ya 10 ya sayansi na teknolojia ya vyuo vya elimu ya juu nchini

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua  rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.  Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mvumbuzi wa mashine ya kuchujia maji safi, Dkt. Askwar Hilonga, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, Atilio Raphael (kushoto kwake) na William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani waliyoibuni maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani iliyobuniwa maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati  Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akioneshwa Plastiki zilizotengenezwa  kwa kutumia Mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo cha The United African University Of Tanzania (UAUT) Chang Kilee, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo hicho katika Maonesho ya 10 ya  Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya Mashine ya 3D Printer iliyobuniwa nchini Korea na inayotumika kufundishia wanafunzi wa IT wa Chuo cha ‘The United African University Of Tanzania’ (UAUT), wakati alipotembelea banda la maonesho la Chuo hicho katika Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Chuo hicho, Chang Kilee, akimpa maelezo kuhusu Mashine hiyo. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja kati ya mashine za kufanya miamala za Max Malipo, huku akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Machungu Msama,  wakati alipotembelea banda lao la maonesho katika Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tunguu Zanzibar, Hadi Mohamed  (kushoto) na baadhi ya wanafunzi wake, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo hicho kwenye Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya walimu, viongozi na wanafunzi wa Vyuo Vikuu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya walimu, Kung Fu na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udom.

Dkt. Bilal, akisalimiana na mmoja wa Walimu wa Chuo cha Liaoning Shi hua, Liju Shi, wakati alipotembelea katika Banda lao.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.

Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.

Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.

Baadhi ya Wahadhiri na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM, wakitoa burudani ya mchezo wa Kung Fu, wakati wa ufunguzi huo.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM, wakitoa burudani ya mchezo wa Kung Fu, wakati wa ufunguzi huo.

Bhalalusesa asisitiza umuhimu wa umahiri katika Tehama

$
0
0

IMG_8834

Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (hayupo pichani) kufungua kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo.

IMG_8915

Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalusesa wakati akifungua rasmi kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu linalofanyika mjini Bagamoyo. Kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.

Na Mwandishi wetu, Bagamoyo

KAMISHINA wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa, amesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba viwango vya umahiri vya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini vinakua vya juu kukidhi haja ya matumizi ya kufundishia na kujifunza nchini.

Alitoa kauli hiyo mjini hapa wakati akifungua  kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin  Kulwa alisema kwamba changamoto ya Tehama inaonekana wazi katika matumizi yake na hivyo wakufunzi lazima wawe mahiri.

“Duniani kote, sekta ya uchumi, fani mbalimbali, taasisi na hata mifumo ya maisha yanategemea sana matumizi ya Tehama kwa sasa. Kadhalika, maendeleo makubwa katika Tehama yamebadili namna mambo yanavyofanyika,” alisema.

Alisema kwa kuhakikisha kwamba kuna maendeleo  ya kutosha ni vyema walimu kuwa na umahiri unaotakiwa kwani Tehama inachangamoto nyingi zinazotakiwa kuangaliwa ili kuweza kuitumia ipasavyo kuleta mabadiliko katika jamiii.

Aliwataka washiriki kuhakikisha kwamba wanapitia  muswada huo kwa makini na kujazia maeneo yote ambayo wataalamu wameshindwa kumaliza na kusaidia kuweka mtaala huo vyema kwa mafunzo.

Kongamano hilo ambalo ni sehemu ya mradi wa kuimarisha uelewa kwa wanafunzi na wakufunzi vyuo vya walimu ili kuboresha matumizi ya Tehama katika mafunzo hasa masomo ya sayansi limeshirikisha wataalamu mbalimbali na kuendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na watu wa China.

Alisema kwamba serikali inatambua kuwa Tehama inaweza kutumika vyema katika kubadili na kuboresha mfumo wa elimu Tanzania.

Aidha alisema Sera mpya ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 inatambua umuhimu wa Tehama katika kuboresha viwango vya elimu nchini Tanzania.

Alisema moja ya malengo ya sera ni kuonesha mahitaji halisi ya Tehama nchini katika upande wa wataalamu na vifaa ili kufanikisha utoaji wa elimu hata ya masafa katika ngazi zote.

Kongamano hilo ni moja ya mradi wa China Funds in Trust Project (CFIT) wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua tehama na kuitumia.

Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama  na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.

Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu vitaingizwa.

IMG_8909

IMG_8842

Pichani juu na chini ni washiriki wa kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu wakati kongamano hilo likiendelea mjini Bagamoyo.

IMG_8843

IMG_8831

Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge (kushoto) akijadili jambo na mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (katikati). Kulia ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.

IMG_8826

Kiongozi wa kitaifa wa mradi wa CFIT, Prof. Ralph Masenge (kulia),  akifurahi jambo na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (katikati) pamoja na Mratibu wa kitaifa wa mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (kushoto) mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa kongamano linalohusu upitiaji wa waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.

IMG_8928

Mgeni rasmi Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa (walioketi wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo inayomalizika leo mjini Bagamoyo.

TPA yatoa shilingi milioni mbili kusaidia wanahabari wanaopambana na ujangili nchini

$
0
0

2

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Awadh Massawe akizungumza na wanahabari wakati akikabidhi hundi ya sh.milioni mbili kwa Taasisi ya Habari Development Association Dar es Salaam jana asubuhi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Awadh Massawe (kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni mbili kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Habari Development Association (HDA), Kunze Mswanyama (kulia), Dar es Salaam jana asubuhi kwa ajili ya kuandaa mafunzo ya kuwawezesha waandishi wa habari kujenga weledi wa kufanya tafiti na kuandika habari za kupambana na ujangili. Wa pili kushoto ni Ofisa Mwandamizi wa Mawasiliano wa TPA, Focus Mauki na Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Benard James.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Habari Development Association (HDA), Kunze Mswanyama (kulia), akizungumzia kuhusu mafunzo na umuhimu wa wanahabari katika kupambana na ujangili wa rasilimali za taifa kabla ya kukabidhiwa msaada wa sh.milioni 2 kutoka TPA. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TPA, Awadh Massawe.

Kaimu Mkurugenzi wa TPA, Awadhi Massawe (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Mwandamizi wa Mawasiliano wa TPA, Focus Mauki na Mkurugenzi wa Taasisi ya Habari Development Association (HDA), Kunze Mswanyama.

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imetoa sh. milioni 2 kwa Taasisi ya Habari Development Association kwa ajili kuandaa mafunzo ya kuwawezesha waandishi wa habari kujenga weledi wa kufanya tafiti na kuandika habari za kupambana na ujangili.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadh Massawe alikabidhi hundi ya thamani ya fedha hizo kwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Kunze Mswanyama jijini Dar es Salaam jana.“Tunaunga mkono juhudi hizi za kupambana na ujangili,” alisema Massawe.

Alisema TPA imefanya hivyo kwa kuwa nchi ina tatizo la uwindaji haramu hasa wa ndovu na usafirishaji wa pembe za ndovu na kulisababishia hasara taifa kupitia mipaka yake.

Alifafanua kuwa bandari ya Dar es Salaam ni sehemu ya mpaka wa taifa, hivyo lazima TPA iunge mkono juhudi za kuelimisha jamii na kuzuia uhalifu huo.

Massawe alisema kwa sasa wanatarajia kufunga kamera 400 za CCTV ili kuimarisha ulinzi na kuwa skana tatu zimeletwa bandarini kwa ajili yakuziongezea nguvu skana mbili zilizopo.

Pia, alisema wanatarajia kupata msaada wa mbwa maalumu wa ulinzi watakaotolewa na Serikali ya Marekani. Alisema TPA inaendelea kuwajengea uwezo wafanyakazi kimaadili ili kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uaminifu kwa faida ya taifa.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Mswanyama alisema fedha walizopewa watazitumia kwa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari 54  kwa masuala ya ujangili kupata weledi na kutafiti na kufichua ujangili. “Tunahitaji kujenga uwezo wa kupambana na ujangili  ili taifa liweze kunufaika nazo,” alisema.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)


Kampeni ya ‘Wazazi Nipendeni’ kuzinduliwa rasmi leo viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar

$
0
0

Mshauri wa masuala ya Malaria kutoka Taasisi ya Jhpiego, Jasmin Chadewa (kushoto), akitoa huduma ya kumpa dawa ya vitamini A, mtoto Rahim Simai,  viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi ikiwa ni utoaji huduma wa elimu ya afya kwa wajawazito na matumizi ya dawa aina ya SP, upimaji wa malaria pamoja na matumizi ya vyandarua kama muendelezo wa huduma za afya ya mama mjamzito na mtoto kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili wa Kampeni ya Wazazi Nipendeni utakaofanyika kesho katika viwanja hivyo.

Wakina mama wakisubiri kupata huduma katika moja ya banda yaliyopo viwanja vya Mwembe Yanga.

Maofisa Taasisi ya Center for Comminication Programs Johns Hopkins University wakifunga kitanda cha kujifungulia wajawazito wakati wakitoa huduma mbalimbali viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi tayari kwa uzinduzi wa Kampeni ya Wazazi Nipendeni utakaofanyika katika viwanja hivyo kesho.

Mtaalamu wa Maabara Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Mbwana Mohamed (katikati), akimtoa damu, Juma Bakari mkazi wa Yombo Kilakala ikiwa ni utoaji huduma kuelekea uzinduzi wa Kampeni ya Wazazi Nipendeni utakaofanyika kesho. Katikati ni Maida Millanzi wa Hospitali hiyo.

Maofisa Taasisi ya Center for Comminication Programs Johns Hopkins University wakifunga chandarua katika utoaji wa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi.

Msimamizi wa masuala ya Malaria  Kata ya Kurasini Hondo Mwindeni (wa pili kulia), akiwaelekeza wananchi waliotembelea moja ya banda jinsi ya kujikinga na vidudu vya malaria.

Mtaalamu wa Maabara Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Mbwana Mohamed akimtoa damu mpiga picha wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Abdallah Kaniki kwa ajili ya kumpima malaria.

Burudani mbalimbali zikiendelea. Lakini leo katika viwanja hivyo itakuwa ni zaidi ya burudani.

Dotto Mwaibale

BENDI ya muziki wa dansi nchini, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ wanatarajia kutoa burudani  ya nguvu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Wazazi Nipendeni’, itakayofanyika leo kwenye viwanja vya Mwembe Yanga wilayani Temeke jijini , Dar es Salaam.

Mbali na bendi hiyo kutumbuiza leo, pia kutakuwa na uhondo mwingine utakaotolewa na wasanii wa kizazi kipya nchini Chegge Chegunda, Mh Temba na Juma Nature.

Akizungumza Dar es Salaam jana kiongozi wa FM Academia, Nyoshi el Sadaat alisema watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi, ili kujua jinsi ya kujikinga na maambukizi pamoja na kumlinda mama na mtoto huku  wakipata burudani kali toka kwetu bure.

Alisema kuwa nyimbo zote zitakazoimbwa katika viwanja hivyo, zitakuwa na ujumbe utakaogusa watu wa rika zote.

Kiongozi huyo alisema licha ya kupiga nyimbo hizo zitakazokuwa na ujumbe utakaowagusa wa watu rika zote kutokana na maambukizi, pia watapiga nyimbo zao zilizowahi kutamba na zinazotamba sasa.

“Tutaporomosha nyimbo zetu zote kali zikiwemo Heshima kwa wanawake, Anna, Sumbungengi, Prison, Kazi ni kazi na nyingine nyingi ambazo tunaamini zitakuwa burudani tosha kwa mashabiki wa dansi watakaofika viwanja vya Mwembe Yanga,” alisema Nyoshi

Nyoshi alisema hii itakuwa ni mara ya pili kushiriki kampeni yenye maudhui kama hayo, hivyo hatowaangusha katika upande wa burudani.”Kundi letu limejipanga vizuri na tutahakikisha ujumbe tutakaoutoa siku hiyo utabadilisha mwenendo wa jamii ya Tanzania na kujua thamani zaidi ya kumlinda mama na mtoto,” alisema Nyoshi.

Kwa upande wake Meneja wa Mradi huo wa Wazazi Nipendeni, Waziri Nyoni  alisema kila kitu kimekamilika kuhusiana na tamasha hilo na pia utoaji wa elimu kuhusu Afya ya mama na Mtoto inaendelea kwa siku zote mbili jana na leo.

“Elimu ya afya ya mama na mtoto ni muhimu hivyo tunawakaribisha watanzania wote mje kupata burudani na elimu ya afya ya mama na mtoto.

Alisema kufayika kwa Kampeni ya Wazazi Nipendeni ni ya awamu ya pili kwa udhamini wa  shirika la Maendeleo ya Kimataifa la watu wa Marekani (USAID),  ikiwa kwa lengo la kumwezesha mjamzito na mwenza wake kuchukua hatua muhimu kuwa na maendeleo mazuri ya ujauzito, kujifungua salama na kuwa na mtoto mwenye afya njema, hadi anapofika mwaka mmoja,” alisema.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

Phidesia Mwakilima aibuka kidedea uchaguzi wa Ubunge wa viti maalum kupitia tiketi ya Jumuiya ya Wazazi CCM

$
0
0
http://2.bp.blogspot.com/-RCy23A0BZXU/VXGrU4TGNzI/AAAAAAAAPCU/JU7jwGuH2Mw/s1600/11390351_860026487378599_5734199586013076232_n.jpg

Mwanadada  Phidesia Mwakilima.

Na Woinde Shizza, wa libeneke la kaskazini blog

Mkurugenzi wa kampuni ya Phide Entertainment  ambaye pia ni Meneja masoko wa  kituo cha redio Triple A ya Arusha, Phidesia Mwakilima, ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa mbunge viti maalum kupitia Jumuiya ya wazazi (UWT) Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha.

Phidesia Mwakilima, amepata kura 18 na kuwashinda, Aimbora Nnko, aliyepata kura 6, Angela Mwanri kura 4 na Anna John kura 2 ,uchaguzi huo umefanyika ukumbi wa CCM, mkoa.

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo Katibu wa Jumuiya ya wazazi mkoa, wa Arusha, Mayasa Kimbau, amewataka wale ambao kura zao hazikutosha kutokukata tamaa bali wajipange kwa chaguzi zingine ndani ya chama.

Akawataka wanawake wasiwe wanyonge kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi bali wawe mstari wa mbele kujitokeza kila uchaguzi utakapotokea.

TTCL yaunganisha Ofisi na Kanda za MSD kwenye Mkongo

$
0
0
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akionesha orodha ya wateja wanaopata huduma ya mkongo toka kampuni hiyo kwenye tableti yake, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL kwenye hafla ya kukabidhi mradi wa huduma ya mkongo kwa Bohari ya Dawa nchini (MSD) leo jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akionesha orodha ya wateja wanaopata huduma ya mkongo toka kampuni hiyo kwenye tableti yake, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL kwenye hafla ya kukabidhi mradi wa huduma ya mkongo kwa Bohari ya Dawa nchini (MSD) leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania inayotolewa na kampuni ya TTCL. Ofisi za Kanda za MSD zimeunganishwa na Makao Makuu na huduma za mkongo wa mawasiliano ili kufanya kazi zake kwa haraka na ufanisi zaidi.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania inayotolewa na kampuni ya TTCL. Ofisi za Kanda za MSD zimeunganishwa na Makao Makuu na huduma za mkongo wa mawasiliano ili kufanya kazi zake kwa haraka na ufanisi zaidi.

Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Bohari ya Dawa Nchini (MSD) pamoja na wageni waalikwa wakiwemo wanahabari wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) unaotolewa na kampuni ya TTCL.

Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Bohari ya Dawa Nchini (MSD) pamoja na wageni waalikwa wakiwemo wanahabari wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) unaotolewa na kampuni ya TTCL.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akishuhudia kabla ya kukabidhiwa.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akishuhudia kabla ya kukabidhiwa.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam, kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akishuhudia.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam, kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akishuhudia.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (wa tatu kushoto waliokaa) na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (wa pili kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania na Bohari ya Dawa Nchini katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania na kampuni ya TTCL.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (wa tatu kushoto waliokaa) na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (wa pili kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania na Bohari ya Dawa Nchini katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania na kampuni ya TTCL.

KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imekabidhi mradi mkubwa wa Mkongo wa Mawasiliano ambao umeyaunganisha matawi yote ya Bohari ya Dawa Nchini (MSD) na Makao Makuu ili kufanya kazi zake kwa haraka na kwa ufanisi. Hafla ya kukabidhi mradi huo imefanyika leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi mradi huo, kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania, Peter Ngota alisema kampuni hiyo inajisikia fahari kufanikiwa kuunganisha ofisi zote za kanda za MSD na Makao makuu kupitia mkongo wa mawasiliano ambao ni salama na wauhakika katika utendaji wa kazi.

Alisema MSD ni moja ya wateja wake wakubwa ambao wameunganishwa kihuduma kupitia mkongo wa mawasiliano ambao ufanisi wake ni mkubwa na salama kwa wateja tofauti na teknolojia nyingine za mawasiliano. Alisema huduma za mkongo wa mawasiliano zinazotolewa na TTCL kwa wateja wake ni salama na zenye ubora katika ufanisi jambo ambalo limevuta idadi kubwa ya wateja kuongezeka kila uchao.

Alisema kwa sasa TTCL inatoa huduma hizo kwa makampuni ya simu, taasisi mbalimbali za umma na binafsi, mabenki, hospitali kadhaa, vyombo vya habari, wateja binafsi pamoja na mataifa kama Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Zambia na nchi ya Malawi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani alisema MSD ilianza kufungiwa mawasiliano ya mkongo Mwezi Mei, 2011 kwa kuunganisha ofisi za makao makuu na baadaye ofisi mpya za mauzo zilizopo Muleba zilizounganishwa mwaka 2013.

Alisema MSD ilifanya uamuzi wa kuhamia kwenye teknolojia ya Mkongo baada ya kuona uwepo wa matatizo makubwa yaliyokuwepo katika teknolojia ya awali ambayo ni waya wa jadi yaani shaba ambayo pia ilitolewa na kampuni ya TTCL.

“…Bohari ya Dawa iliamua kuhamia katika teknolojia hii baada ya kufanya utafiti wa kina na kuona faida ambazo zinaweza kupatikana kwa kutumia teknolojia hii (mkongo) na hivyo kuachana na matatizo yanayosababishwa na teknolojia ya shaba. Hii ina maana mkongo unaweza kubeba habari zaidi na kwa ubora mkubwa kuliko waya wa shaba,” alisema Mwaifwani.

Alisema kwa sasa MSD imeanza kupata mafanikio makubwa baada ya kuanza kutumia huduma za mkongo na tayari TTCL imeyaunganisha Ofisi 10 za MSD ambazo ni Kanda nane (8) pamoja na vituo viwili vya mauzo; alizitaja Kanda zilizounganishwa ni pamoja na Dar es Salaam, Moshi, Iringa, Mbeya, Mwanza, Tabora, Dodoma, Mtwara, Muleba, Tanga, Makao Makuu ya Muda Jamana na Ofisi za Keko Mwanga.

“…Tunasema kwamba Bohari ya Dawa imedhamiria kuokoa maisha ya Watanzania kwa kutumia teknolojia ya Mkongo yenye kasi zaidi, usalama, na gharama nafuu zaidi katika kuhakikisha dawa zenye ubora zinamfikia kila Mtanzania kwa wakati na kupunguza kero ya kusubiri huduma zetu kwa muda mrefu kwani sasa huduma zinapatikana kwa wakati kwa kuwa teknolojia inayotumika ni ya kisasa na yenye ubora wenye kukidhi viwango vinavyohitajika na bohari ya dawa,” alisema Mkurugenzi Mkuu, Mwaifwani.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

Rais Kikwete aifariji familia ya marehemu John Edward Mchechu

$
0
0

1

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bw. Nehemia Mchechu. Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa Mkurugenzi huyo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam julai 23, 2015 kumpa pole kufuatia kifo cha Baba yake aliyekuwa anaugua ugonjwa wa kiharusi.

Marehemu atasafirishwa kuelekea Muheza, Tanga kwa ajili ya Mazishi. Mazishi yatafanyika Kijiji cha Enzi, Muheza – Tanga siku ya Jumamosi tarehe 25/07/2015.(PICHA ZOTE NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM).

2

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Marehemu John Edward Mchechu ambaye ni baba wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bw. Nehemia Mchechu. Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa Mkurugenzi huyo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam julai 23, 2015 kumpa pole kufuatia kifo cha Baba yake aliyekuwa anaugua ugonjwa wa kiharusi.

3

Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiifariji familia ya marehemu John Edward Mchechu Mbezi beach jijini Dar es Salaam julai 23, 2015. (wapili kushoto) mtoto wa Marehemu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu.

4

Familia ya marehemu John Edward Mchechu.

5 6

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka mara baada ya kuifariji familia ya marehemu John Edward Mchechu (katika) mtoto wa Marehemu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu.

7

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana viongozi mara baada ya kuifariji familia ya marehemu John Edward Mchechu (katika) mtoto wa Marehemu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu.

8

Waombolezaji.

9

????????????????????????????????????

Kadama Malunde achaguliwa Mwenyekiti mpya wa wanahabari Shinyanga

$
0
0
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo.

Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao wakijiuzuru nyadhifa zao kabla ya uchaguzi mkuu kupata viongozi wapya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC).

Msimamizi wa uchaguzi mkuu wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga David Nkulila akizungumza jambo wakati wa uchaguzi mjini Shinyanga.

Mwenyekiti mpya wa SPC Kadama Malunde, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Malunde1 blog akipongezana na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shija Felician (kulia).


Viongozi wapya wa SPC wakiwa meza kuu.

 

Katibu mkuu mpya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ndugu Stephen Wang’anyi akizungumza baada ya uchaguzi, kushoto ni mweka hazina aliyetetea kiti chake bi Stella Ibengwe.


Baadhi ya viongozi wa SPC wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga

CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club-SPC)  Julai 23, 2015 kimefanya Uchaguzi wake Mkuu wa viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo ambapo mwanahabari, Kadama Malunde amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo Mkuu wa SPC uliofanyika mjini Shinyanga, David Nkulila alisema, Malunde ametwaa nafasi hiyo baada ya kuwashinda wagombea wenzake watatu ambao ni Patrick Mabula, Marco Mipawa na Greyson Kakuru.

Kadama Malunde ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Kahama FM na Mkurugenzi wa Malunde1 blog ambayo ni blogu Mwanachama wa Chama cha Blogu Tanzania (Tanzania Bloggers Network, TBN).

Nkulila aliwataja viongozi wengine wapya waliochaguliwa kuwa ni Stephen Wang’anyi akichaguliwa kuwa Katibu Mkuu, Shaaban Alei kuwa Makamu Mwenyekiti, Katibu Msaidizi Ally Lytawi na mweka hazina ni Stella Ibengwe pamoja na kamati tendaji ya wajumbe watano.

Baada ya kutangaza matokeo hayo Nkulila amewataka wanachama wa klabu hiyo, kuachana na tofauti zillizokuwepo wakati wa uchaguzi na badala yake kushirikiana na viongozi waliowachaguliwa ili kuleta maendeleo na mabadiliko katika klabu hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti mpya wa SPC, Kadama aliwashukuru wanachama wote wa chama hicho kwa kumkubali aweze kushirikiana nao kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wanahabari mkoani hapo pamoja na kuleta maendeleo kwa klabu hiyo. Aidha aliahidi kutenda haki kwa kila mmoja na kuzingatia katiba ya chama katika utendaji wa kazi za chama.

Kwa upande wake Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Felician amewataka viongozi wapya wa klabu hiyo kuendeleza misingi ya ushirikiano waliouacha na kuwasisitiza kufanya kazi kwa uwazi na ukweli huku wakizingatia maadili ya wanahabari.

Rais Kikwete atunukiwa Tuzo ya Kudumisha Utawala Bora Barani Afrika

$
0
0

Jakaya-Kikwete1

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Jitihada za muongo mzima wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuimarisha na kudumisha Utawala Bora katika Tanzania zimetambuliwa kimataifa kwa Rais kutunukiwa Tuzo la Utawala Bora Barani Afrika mwaka 2015 (Good Governance in Africa.)

Rais Kikwete ametunukiwa Tuzo hiyo na Taasisi ya African Achievers Awards yenye makao yake makuu katika Afrika Kusini kutokana na kutambua mchango wake mkubwa katika kulea, kuimarisha, kuendeleza na kudumisha Utawala Bora katika Tanzania katika miaka yote 10 ya uongozi.

Rais Kikwete anajiunga na watu wachache ambao wamepata kupokea tuzo hiyo tokea lilipotolewa kwa mara ya kwanza kwa Askofu Mkuu Desmond Tutu wa Afrika Kusini mwaka 2011 kwa kutambua mapambano yake katika kutetea haki za binadamu,usawa, haki na amani.

            Rais Kikwete ameteuliwa kutoka miongoni mwa zaidi ya watu 1,202 ambao majina yao yaliwasilishwa kwenye Jopo la Kimataifa Linalojitegemea na lenye wajumbe kutoka Uingereza na Afrika Kusini kwa ajili ya uteuzi.

Kutokana na tunuku hiyo, Rais Kikwete amealikwa kwenda Afrika Kusini kupokea tuzo hiyo katika sherehe kubwa inayofanyika jioni ya kesho, Jumamosi, Julai 25, 2015 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Sandton (Sandton Convention Centre) mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Kwa sababu ya kukabiliwa na shughuli nyingi hapa nyumbani, Rais Kikwete amemwomba Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Asha Rose Migiro, kumwakilisha katika sherehe ya kupokea tuzo hiyo ambako pia atatoa mada kuhusu “Umoja wa Afrika: Fursa na Changamoto (Africa’s Unity: Prospects and Challenges) kwa niaba ya Rais Kikwete.

Tuzo za African Archievers Awards zinalenga kuwatambua watu binafsi na taasisi ambazo zimejitambulisha  kwa michango yao kwa ustawi na maendeleo ya Bara la Afrika.

Katika barua ya kumjulisha Rais Kikwete kuhusu uteuzi wake, Mtendaji wa African Achievers Awards, Bwana Rex Indaminabo amesema: “Uongozi wa African Achievers Awards unayo furaha kukujulisha juu ya uteuzi wako wa kupokea  Tuzo la 2015 African Achievers Awards katika kundi la Utawala Bora Barani Afrika.”

Ameongeza Mtendaji huyo: “Ni kwa furaha na heshima kubwa kuwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri na Taasisi ya Uongozi na Menejimenti  wanakuandikia kukupongeza kwa kuteuliwa kwenye orodha ya mwisho na hatimaye kuwa mshindi wa Tuzo la African Achievers Awards katika kundi la Utawala Bora katika Afrika.”

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.

24 Julai, 2015

Mchungaji Natse awaaga jimbo la Karatu , Qambala kupeperusha bendara ya Chadema

$
0
0
Mbunge mstaafu wa Jimbo la Karatu mkoa wa Arusha,Mchungaji Israel Natse akizungumza katika mkutano mkuu wa Jimbo hilo ambao ulifanya uchaguzi wa madiwani na Wabunge wa  Viti Maalumu mgombe Ubunge wa Jimbo la Karatu,katikati ni Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha,Kalisti Lazaro na Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Karatu,Thomas Darabe.
Mbunge wa Viti Maalumu wilaya ya Karatu, Cecilia Paresso akizungumza katika mkutano huo ambao alichaguliwa na wajumbe wanawake kuwania nafasi hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya hosteli ya KKKT Karatu na kumpongeza mch.Natse kwa kuamua kuachia nafasi wanachama wengine.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya hosteli ya KKKT Karatu na kumpongeza mch.Natse kwa kuamua kuachia nafasi wanachama wengine.
Mwanamke wa kwanza kuwahi kujitokeza kuomba ridhaa ya wanachama kumchagua kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Karatu,Fransisca Duwe akijinadi kwa wajumbe.
Willy Qamballa mmoja wa wagombea akijinadi kwa wajumbe.
Aliyekua Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Karatu,Lazaro Maasay akiomba kura kwa wajumbe.
Mshindi wa kura za maoni za Ubunge Jimbo la Karatu,Willy Qamballa akiwashukuru wajumbe baada ya kujizolea kura 217 na mpinzani wake wa karibu Lazaro alipata kura 84.
Mshindi wa kura za maoni za Ubunge Jimbo la Karatu,Willy Qamballa akifurahia na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi.

 


Tabora wanufaika na Mafunzo ya ULINGO – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP)

$
0
0

ULINGO WA WANAWAKE WANASIASA – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP) ni shirika lisilo la kiserikali lililoendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watia nia wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu katika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa nchi ikiwa ni kuchangia kutoa elimu inayolenga kuleta usawa kama haki msingi ya Mtanzania. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na UNWomen.

Mafunzo hayo yamewanufaisha walengwa husika kwa kujipatia elimu hiyo huku wawezeshaji wakiwa ni Hilda Stuart Dadu na Emmiliana Msaguka waliohakikisha wanawafikia watiania katika mkoa wa Tabora na kuendesha mafunzo hayo pale Student Center.

t-wcp (2)

Wanufaika na watia nia za kugombea nafasi mbalimbali na wa vyama tofauti tofauti wakifuatila mafunzo hayo yaliyotolewa na Hilda Stuart Dadu kutoma TWCP.

t-wcp (3)

Watia nia wakichukua kumbukumbu za mafunzo hayo.

t-wcp (4)

Miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo akifuatilia jambo kwa umakini.

t-wcp (5)

Wakati mafunzo yakiendelea na maswali yakiulizwa kwa ufafanuzi zaidi kutoka kwa wawezeshaji.

t-wcp (6)

Hilda Stuart Dadu wa ULINGO (aliyesimama) akisisitiza jambo wakati mafunzo yakiendelea.

t-wcp (1)

t-wcp (7)

t-wcp (8)

Hawa, mgombea wa ubunge wa viti maalumu kwa tiketi ya Chadema akiuliza swali kwa muwezeshaji.

unnamed (1)

Muwezeshaji Emmiliana akitoa zoezi kwa wanafunzi wake ili kukazia zaidi kile walichofundishwa na kukifanya kwa vitendo.

t-wcp (13)

Miongoni mwa wanakundi wakijadiliana jambo baada ya kupewa zoezi na muwezeshaji wa mafunzo.

t-wcp (10)

t-wcp (9)

Picha ya pamoja ya wanufaika wa mafunzo ya ULINGO na wawezeshaji wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo watia nia za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Mafunzo hayo yamekuja wakati huu ambao ndiyo haswa muda mwafaka wa uchaguzi mkuu wa ngazi za udiwani, ubunge na Urais.

Dkt Magufuli arejea jijini Dar baada ya kujitambulisha mikoa kadhaa, apokelewa kwa kishindo

$
0
0

7

Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mji wa Chalinze (hawapo pichani) alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodomaakitokea Mkoani  Dodoma. (PICHA NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP).

Wakazi wa Bagamoyo wakimsikiliza Dkt Magufuli wakati alipokuwa akijitambulisha kwao.

Mkazi wa Bagamoyo akifurahia jambo.

 Wananchi wakimshangilia Dkt Magufuli (hayupo pichani) alipokuwa akijitambulisha kwao hapo mjani mjini Bagamoyo

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze, ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akiwasalimia Wananchi wa Chalinze na kumkaribisha Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru Wananchi wa Chalinze (hawapo pichani) pamoja na kujitambulisha kwao alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.

 Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze, ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akiwasalimia Wananchi wa Chalinze na kumkaribisha Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru Wananchi wa Chalinze (hawapo pichani) pamoja na kujitambulisha kwao alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.

Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mji wa Chalinze (hawapo pichani) alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodomaakitokea Mkoani  Dodoma.

 
Wananchi wa Chalinze wakiwa wamelizunguka gari la Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Kiwangwa  alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.

Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimshangilia kwa mayowe Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Kiwangwa alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.

 

Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimsikiliza Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Chalinze alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo na Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli mjini Bagamoyo,aliposimama mjini hapo kujitambulisha na kuwashukuru kwa kujitokeza kwao kwa wingi kumpokea,alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete pamoja na  Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia jambo mjini Bagamoyo,aliposimama mjini hapo kujitambulisha na kuwashukuru kwa kujitokeza kwao kwa wingi kumpokea,alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.

 Wananchi wakifuatilia kwa makini meneno ya Dkt Magufuli.
 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Rajab Luhwavi akizungumza jambo na Mh.Ridhiwani Kikwete.
 Dkt. Magufuli akijitambulisha kwa wakazi wa mji wa Bagamoyo mapema jana.

Worth reading: A Touching True Love Story…!

$
0
0

Chinese Man Married Dead Bride Who Died 8 Days before the wedding.

Chinese_man_Married_Dead_Bride_001

A 26-year-old Chinese man Zhuang Huagui has married his dead girlfriend Hu Zhao, 21, The couple originally planned to get married on February 4, but on January 28, one week before their wedding, the girl was stabbed to death by two break-in thieves. With all the pain, lost and love, the man still decided to marry his dead girlfriend.

Chinese_man_Married_Dead_Bride_002

Chinese_man_Married_Dead_Bride_003

Chinese_man_Married_Dead_Bride_004

Chinese_man_Married_Dead_Bride_005

Their wedding ceremony was held at a funeral parlor in Zhangzhou, Fujian, China, and family from both sides witnessed their wedding. The bride was dressed with beautiful wedding gown and lying in a crystal coffin.

Chinese_man_Married_Dead_Bride_006

Chinese_man_Married_Dead_Bride_007

Zhuang Huagui held his wife’s wedding photo in front of the funeral parlor to welcome the guests for coming to the wedding.

Chinese_man_Married_Dead_Bride_008

The broom gave wedding ring to his dead wife.

Chinese_man_Married_Dead_Bride_009

This is true love, the girl in heaven will be touched…

1267725670_6747cf45_1267725833

Rais Kikwete amuapisha Mkurugenzi mpya wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani Kombey Ikulu jijini Dar

$
0
0

t (1)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ikulu jijini Dar es salaam, Julai 25, 2015.

t (2)

Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey akiweka sahihi kwenye hati baada ya kuapishwa kuwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ikulu jijini Dar es salaam jana jioni, Julai 25, 2015.

Rais-uteuzi-tume ya uchaguzi.doc 

Mama Kikwete apewa tuzo ya kimataifa ya mwaka 2015 ya Kiongozi bora Mwanamke

$
0
0

unnamed-51

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea TUZO maalum ya “ CWL International Women of Excellency Award for Leadership” kutoka kwa Profesa Joseph Adaikalam, Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Chuo Kukuu cha Binary kilichoko nchini Malaysia kwa kutambua na kuthamini mchango wake katika maendeleo ya wanawake nchini Tanzania na Afrika tarehe 24.7.2015. Aliyesimama (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Mlima, akifuatiwa na Profesa Bulochana Nair na Kulia ni Profesa Datin Rohini Devi wa Chuo Kikuu cha Binary.(PICHA NA JOHN LUKUWI).

Na Anna Nkinda – Kuala Lumpur, Malaysia

Mke wa Rais Mhe. Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya kimataifa ya mwaka 2015 ya Kiongozi bora Mwanamke (International Woman of Excellence Award for Leadership) na kituo cha Uongozi cha wanawake cha chuo kikuu cha Binary cha nchini Malaysia kutokana na mchango wake mkubwa katika uhamasishaji wa maendeleo ya wanawake watanzania.

Tuzo hiyo imetolewa na Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa chuo hicho Prof. Joseph Adaikalam katika ukumbi wa mikutano uliopo chuo kikuu cha Binary kilichopo Kuala Lumpur nchini Malaysia.

Akiongea mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Mhe. Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alikishukuru kituo hicho na kusema amefarijika kwa kuona jinsi kinavyothamini maendeleo ya Wanawake wa Afrika na Dunia kwa ujumla. Kwa kupitia tuzo hiyo wameonesha jinsi wanavyotambua na kuthamini juhudi zinazofanywa na wanawake.

Mhe. Mama Kikwete alisema “Tuzo hii siyo yangu pake yangu bali ni ya ushindi wa wanawake wote wa Tanzania, Afrika na maeneo mengine ambao wanafanya jitihada kubwa ya kukabiliana na vikwazo kadhaa vinavyowazuia kupiga hatua kubwa ya maendeleo. Mafanikio yanayoonekana yanapatikana ingawaje safari bado ni ndefu na yenye changamoto nyingi”.

Nilipoanza majukumu yangu kama Mke wa Rais wa nchi yetu, nilitambua umuhimu wa kuwa na chombo kitakachoniwezesha kuhamasisha jamii na rasilimali ili niweze kutoa mchango wangu kwa ajili ya maendeleo ya jamii yetu. Hivyo nilianzisha Taasisi ya WAMA ikiwa na Dira ya kuiona Tanzania ambayo wanawake wanawezeshwa na kuishi maisha bora”.

Aliendelea kufafanua kwamba tangu awali alitambua  ili kumkomboa mwanamke ni muhimu kuzingatia mazingira na mahitaji yake yote kwa pamoja. Alitambua  kwa kumpatia mtoto wa kike elimu, kutamuepusha na ndoa za utotoni, ujauzito katika umri mdogo, kutapunguza matukio ya vifo vinavyotokana na uzazi na vifo vya watoto wachanga.

Mwenyekiti huyo wa WAMA alimalizia kwa kusema kuwa  mwanamke aliyeelimika anatambua na kuweza kutumia fursa za kiuchumi na kujiendeleza yeye mwenyewe na jamii inayomzunguka.

Akisoma wasifu wa Mhe. Mama Kikwete Prof. Sulochana Nair ambaye ni Makamu na Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho  alisema tuzo hiyo ni ya juu na  kwa mara ya kwanza imetolewa kwa mke wa Rais hii ni kutokana na kazi anazozifanya za kuwasaidia wanawake, watoto na watanzania kwa ujumla.

Prof. Sulochana  alisema Mama Kikwete kupitia Taasisi ya Wama ametoa   fursa za elimu ya sekondari kwa watoto wa kike ambao ni yatima na wengine wanaotoka familia masikini hadi sasa zaidi ya watoto 800 wamenufaika, kufanya uraghibishi dhidi ya ndoa za utotoni, mimba katika umri mdogo.

 Kupiga vita maambukizi ya VVU kwa vijana na kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ,kufanya uraghibishi ili kuishirikisha jamii katika kutoa chanjo, upimaji na matibabu ya saratani za shingo ya kizazi na matiti, kutoa mafunzo na uratibu wa kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Tuzo ya kimataifa ya Kiongozi bora Mwanamke (International Woman of Excellence Award for Leadership)inayotolewa na kituo hicho pale wanapoona na kutambua mchango wa mwanamke aliyejitokeza  kwa juhudi zake za kusaidia na kuhamasisha maendeleo ya wasichana na wanawake Duniani.

Viewing all 5755 articles
Browse latest View live