Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all 5755 articles
Browse latest View live

BBC Swahili presents: The new-look Dira ya Dunia

$
0
0

bbc swahili

Kipindi cha Kiswahili cha BBC Televisheni Dira ya Dunia sasa kinakujia na muonekano mpya unaovutia.

Kipindi hicho kinachopeperusha Taarifa ya habari kwa zaidi ya wasikilizaji milioni 6.9 itakuwa na sura mpya inayojumuisha maandishi mapya yaliyotiwa nakshi,vipindi vipya na ripoti za kina zinazojumuisha habari, michezo na burudani.

 Tangu ilipozinduliwa mwaka wa 2012 Dira ya Dunia TV, inatazamwa kila siku na mashabiki nchini Tanzania, Kenya, Burundi na katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Aidha ina mashabiki si haba katika mitandao ya kijamii.

Mtangazaji nyota wa idhaa hii ya Kiswahili, Salim Kikeke, alitunukiwa mataji ya Tuzo Za Watu  na Mtangazaji bora wa Runinga wa mwaka, kwa mwaka wa pili mtawalio.

Mshindi wa tuzo hizo anachaguliwa na umma.

Kikeke anasaidiana na watangazaji wenza, Kassim Kayira, Zuhura Yunus na Peter Musembi.

Dira Ya Dunia yenye sura mpya itaendelea kuwaletea wageni wenye uzoefu wa maswala tofauti.

Wageni waliohojiwa tayari katika Dira ya dunia ni pamoja na  rais  Jakaya Kikwete wa Tanzania, rais Pierre  Nkurunziza wa Burundi  na rais Yoweri Museveni wa Uganda mbali na wasanii waliobobea kama vile  Diamond Platnumz kutoka  Tanzania, Eddy Kenzo kutoka Uganda na Juliani wa Kenya.

 “Siamimi kwa hakika kuwa imekuwa takriban miaka mitatu tayari .

Imekuwa safari ya kuvutia sana.

Mapokezi yetu katika kanda zima ya Afrika Mashariki na kati ni ya kufana na kuridhisha.

Tunapania kuendelea kuwapasha habari wasikilizaji wetu kuwa elimisha na pia kuwa burudisha kwa miaka mingi.

Hii sura tunayoizindua ni thibitisho tosha kuwa ari yetu ni hiyo.”, anasema  mtangazaji nyota Salim Kikeke.

Kwa upande wake Mhariri na Mtayarishi mkuu  wa Dira ya Dunia bi Mariam Omar anasema kuwa ”inafurahisha mno kwa mtazamaji kuwa tunaimarisha kipindi chetu maarufu ”Dira ya Dunia.”

  Tutaendelea kuwapa watazamaji wetu habari za utendeti zaidi na kwa njia za kuvutia watazamaji wetu ambao bila shaka watakuwa na uwezo zaidi wa kuwasiliana nasi na kuchangia habari tutakazo peperusha.”

Details of BBC Swahili on social media –

Over 896,000 fans on Facebook (as of June 2015) and monthly interactions (i.e. likes, comments, shares) on the page was at 1.4m in April 2015. On Twitter, @bbcswahili has 49,800 followers (as of June 2015).


JUST IN: Saed Kubenea achukua fomu ya kuwania ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Ubungo

$
0
0

kubenea-mpoki

Mwanahabari mkongwe Saed Kubenea (pichani) achukua fomu kuomba ridhaa ya kuwania ubunge kupitia Chadema jimbo la Ubungo.

Saed Kubenea ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd., inayochapisha magazeti ya MwanaHALISI; MSETO; MwanaHALISI Online na MwanaHALISI Forum na ndiye mmiliki wa kampuni hiyo.

NHC yatoa msaada wa mashine za matofali, Sh. 500,000 kwa vijana walioacha kutumia dawa za kulevya Kigogo, Dar

$
0
0

 Vijana waliopata ushauri nasaha wa kuacha kutumia dawa za kulevya, wakishangilia baada ya Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguye (aliyevaa koti) kuwakabidhi msaada wa mashine tatu za kufyatulia matofali pamoja na mtaji wa sh. 500,000 katika hafla iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kigogo, Dar es Salaam jana.  Katikati mstari wa mbele ni Mchungaji wa kanisa hilo, Jackson Haranja ambaye pia ni mlezi wa vijana hao wapatao 40. Kulia mstari wa mbele ni Yahya Charahani ambaye ni Ofisa Mawasiliano wa NHC. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Saguye akimkabidhi mashine hizo Mlezi wa vijana hao, Mchungaji Haranja.

 Mchungaji Haranja akitoa shukurani kwa shirika hilo baada ya kupokea msaada huo ambapo aliseama utasaidia sana kuinua hali ya maisha ya vijana hao waliokuwa wameathirika na dawa za kulevya.

Saguye akizungumza na vijana hao kuhusu lengo la kuwapatia msaada wa mashine hizo.

Asilimia 70 ya wagonjwa wa saratani hupoteza maisha katika nchi zinazoendelea – Mhe. Uhuru Kenyatta

$
0
0

12_7

Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta akitambulishwa wake wa marais kutoka nchi mbalimbali za Afrika na Mkewe mama Margaret Kenyatta  kabla ya kufungua mkutano wa tisa wa Jukwaa la wake wa marais wa Afrika la kutokomeza magonjwa ya saratani za mfumo wa uzazi ambazo ni mlango wa kizazi, matiti na tezi dume unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta (KICC) uliopo mjini Nairobi. Kushoto ni Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete.

CKV9RFDWoAA1kFz

Na Anna Nkinda – Nairobi, Kenya

Asillimia 70 ya wagonjwa wa saratani hupoteza maisha katika nchi zinazoendelea na katika Bara la Afrika lenye watu zaidi ya milioni 804 asilimia  12.4 wanapata saratani kabla ya kufikia umri wa miaka 75  na asilimia  90 wanapata ugonjwa huo wakiwa na  umri wa chini ya miaka 40.

Hayo yamesemwa na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakati akifungua mkutano wa tisa wa Jukwaa la wake wa marais wa Afrika la kutokomeza magonjwa ya saratani za mfumo wa uzazi ambazo ni mlango wa kizazi, matiti na tezi dume unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta (KICC) uliopo mjini Nairobi.

Rais Kenyatta alisema Ripoti ya saratani iliyotolewa mwaka 2014 na  Shirika la Kimataifa la kutafiti saratani kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ilionyesha takwimu mpya za saratani zinaongezeka  kila mwaka na kwa upande wa Afrika  vifo vingi vinatokana na saratani ya mlango wa kizazi.

“Watu wanapoteza maisha na kuugua saratani kutokana na kutokuwa na uelewa wa ugonjwa huo, kutokuchukua hatua za mapema na watu kutambulika  kuwa na ugonjwa wa saratani wakati umefikia hatua ya mwisho kutokana na hili tutaendelea kuwa na wagonjwa ambao wanapata maumivu, wanashindwa kupata matibabu kwa wakati na  uangalizi wa karibu katika bara letu”.

Ni lazima tuhakikishe jamii inajulishwa kuhusu ugonjwa wa saratani na  kubadilisha aina ya maisha tunayoishi kama watu wataacha kuvuta sigara, watakula vyakula vyenye afya, atapunguza kunywa pombe na kufanya mazoezi mara kwa mara tutakuwa tumezuia asilimia 40 ya saratani”, alisema.

Aidha Mhe. Rais Kenyatta alisema katika bara la Afrika ugonjwa wa saratani siyo moja ya agenda inayopewa kipaumbele katika masuala ya afya ukilinganisha na magonjwa mengine kama ya  kuambukiza  lakini sasa ili kupambana na saratani kunatakiwa kuwa na mikakati kwa nchi chache ambazo zitaweza kukutana na  kufanya utafiti na kutoa matibabu ili kuzuia watu wasife na hivyo kuokoa maisha katika hatua ya mwanzo ya ugonjwa.

Mhe. Rais Kenyatta alimalizia kwa kusisitiza kuwa watu wanahitaji kupata chanjo ya hepatitis ambayo inazuia saratani ya  Ini na  Human Papilloma Virus (HPV) inayozuia saratani ya mlango wa kizazi ambazo zitasaidia kupunguza idadi ya saratani katika bara la Afrika.

Akiwakaribisha wake wa marais na wadau mbalimbali wa afya  waliohudhuria mkutano huo Mke wa Rais wa Kenya Mhe. Mama Margaret Kenyatta alisema ni muhimu wadau hao wakaendelea kushirikiana na kufanya kazi  kwa pamoja ili kukabiliana na magonjwa hayo ya saratani.

Mhe. Mama Kenyata ambaye ni Mwenyekiti mpya wa Jukwaa la wake wa marais wa Afrika la kutokomeza magonjwa ya saratani za mfumo wa uzazi ambazo ni mlango wa kizazi, matiti na tezi dume kwa mwaka 2015 – 16 alisema wamefanikiwa kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu magonjwa ya saratani wanachotakiwa kukifanya hivi sasa ni  kuendelea kuhamasisha jamii ili waweze kujichunguza dalili za awali za saratani na kutibiwa kuzuia kwani saratani nyingi zikigundulika mapema zinatibika.

Alisisitiza, “Tunatakiwa kuwashawishi viongozi, Serikali na sekta binafsi na taasisi zisizo za kiserikali kuchukua hatua za lazima ili kuweza kukabiliana na saratani na hivyo kuokoa maisha ya watu wetu”.

Kuhusu ulaji wa vyakula alihimiza ni muhimu waafrika wakaangalia maisha ya zamani na kurudi nyuma kwa  kuanza kula vyakula vya asili na kuacha  kula vyakula vilivyosindikwa  hasa kwa vijana”

Mkutano huo wa siku tatu wenye kauli mbiu ya wekeza kuokoa maisha: wajibu wa ushirikiano wa sekta binafsi ulihuhuriwa na wake wa Marais kutoka nchi 12 akiwemo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Salma Kikwete.

Profile za watangazaji wa BBC, Dira ya Dunia

UN yakanusha uzushi wa Jamii Forum na Indian Ocean Newsletter

$
0
0

IMG_7871

Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez.

UMOJA wa Mataifa umetaka vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa kuhakikisha  vinatoa taarifa zao kwa usahihi kuhusu maandalizi ya uchaguzi na uchaguzi wenyewe.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa Dar es salaam, kufuatia taarifa iliyochapishwa na jarida moja kwamba UN inataka kujitoa katika kusaidia mandalizi ya uchaguzi nchini Tanzania.

Aidha alisema kwamba si kweli kuwa Umoja wa Mataifa haujaridhishwa na mwenendo wa maandalizi ya uchaguzi nchini Tanzania na kwamba Umoja huo utaendelea kushirikiana na serikali na vyombo vingine vya uchaguzi kuhakikisha uchaguzi unakwenda vyema.

Indian Ocean Newsletter ya Julai 10 mwaka huu ilichapisha habari iliyoandikwa na kichwa cha habari  “State is facing electoral commissions negligence” na kusema kwamba Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez, haridhishwi na mwenendo wa maandalizi ya uchaguzi na uchaguzi wenyewe na kutishia kuondoa msaada wa mamilioni unaoratibiwa na UNDP kutoka kwa wahisani mbalimbali.

Aidha Julai 15, 2015, mtandao wa Jamii Forum ilitafsiri habari hiyo kwa  Kiswahili na kuitawanya kwa wasomaji wake.

Taarifa ambayo sio sahihi iliyochapwa na Jamii forum hii hapa link: http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/885659-un-yaeleza-kutoridhishwa-kwake-na-vurugu-za-uchaguzi-nchini-tanzania.html#post13289399

Ukweli ulivyo

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini hajawahi kukutana  wala kuzungumza na watu wa Indian Ocean Newsletter  .

Aidha taarifa zilizotolewa na kijarida hicho na tafsiri yake iliyowekwa mtandao wa kijamii wa Jamii Forums hazikujengwa katika ukweli.

Pia  Umoja wa Mataifa utaendelea kufanyakazi na mamlaka za Tanzania na wananchi wake na kuwa Uhusiano kati ya Umoja wa Mataifa na mamlaka za uchaguzi nchini Tanzania na Jumuiya ya kimataifa inayofadhili mradi wa DEP unawasilisha mahusiano muhimu miongoni mwa wadau mbalimbali wanaotaka kuwapo na uchaguzi huru na wa amani.

Alisema katika makubaliano kuna kamati ya mradi inayojumuisha wadau wote na ina wajibu kuongoza na kutoa mwongozo wa utekelezaji  mradi huo kimkakati.

Maamuzi ya mradi huo hufanywa na kamati hiyo na kamati ya ufundi ya mradi iliyopo Bara na Zanzibar.

Kutokana na ukweli huo Umoja wa Mataifa unavitaka vyombo vya habari vya kitaifa na Kimataifa kuhakikisha kwamba inatoa taarifa za ukweli na za usahihi kipindi hiki cha maandalizi na uchaguzi wenyewe.

Biometric Voter Registration (BVR)   Machines operator, Kheri Mkali attends Rebeca Kimu at Bunju A in Dar es Salaam yesterday during the trial registration. PHOTO|VENANCE NESTORY

Biometric Voter Registration (BVR) Machines operator, Kheri Mkali attends Rebeca Kimu at Bunju A in Dar es Salaam yesterday during the trial registration. (LIBRARY PHOTO|VENANCE NESTORY).

Background

The Democratic Empowerment Project is a three year project launched on the 12th of March 2013 and is directly executed by UNDP with UN Women and UNESCO through a donor basket fund. It follows two previous electoral support projects in Tanzania: the Electoral Assistance Project of 2005 and the Election Support Project of 2010. The USD 25m project has four main components, namely, a) supporting legal and institutional reforms; b) support improvement of Electoral Management body’s capacities(NEC and ZEC); c) promote inclusive participation in political and electoral processes, and d) support national peace infrastructures.  More specifically, the project has been supporting both NEC and ZEC to improve their institutional capacity both in the context of the conduct of the voter registration process (but not the provision of the BVR kits which is the government’s responsibility) and the preparations for the 2015 general elections. DEP’s support has included technical and advisory services, staff training, voter education and stakeholder engagement. Such stakeholders include the Office of the Registrar of Political Parties, political parties, media, civil society and groups representing women, youth and people with disabilities.  So far DEP has supported and implemented most of these activities either directly or via cooperation agreements with the electoral management bodies who execute specific activities directly in line with their mandate.

Issued by: The Office of the UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative – Mr. Alvaro Rodriguez

For more information, please contactHoyce Temu-UN Communications Specialist at hoyce.temu@one.un.org  or Aine Mushi, UN Coordination Specialist at aine.mushi@one.un.org

Advisory – Indian Ocean Newsletter 20July15.docx

Below is the Indian Newsletter article in French

Raia 32 kati ya 37 wa Afrika Kusini wafika kilele cha Uhuru kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto yatima washuka salama

$
0
0
Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Erastus Rufunguro akimpokea muigizaji maarufu wa filamu wa nchini Afrka Kusini, Jacky Devnarain maarufu kama Rajesh Kumar, jina alilotumia katika tamthiliya ya Isidingo the Need aliposhuka yeye na wenzie 37 waliopanda mlima huo kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wasichana wanaotoka katika familia maskini.
Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Eva Mallya akimpatia kinywaji, Muigizaji Jacky mara baada ya kufika katika lango la Marangu, akishuka kutoka Mlima Kilimanjaro.
Muigizaji Jacky akisalimiana na Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Tanzania (TANAPA), Ibrahim Musa baada ya kushuka kutoka Kilele cha Uhuru ambako kati ya watu 37 waliopanda mlima huo ,32 ndio waliofanikiwa kufika kileleni.
E86A6648 (1280x853)Mkuu wa wilaya ya Siha, Dkt. Charles Mlingwa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla fupi ya mapokezi ya ugeni huo ulioanda mlima Kilimanjaro akimkaribisha keki Muigizaji Jacky mara baada ya kuteremka kutoka Mlima Kilimanjaro.
Washiriki wa timu hiyo iliyopanda mlima Kilimanjaro kwa uratibu wa Mfuko wa Mandela wakifika katika lango la Marangu mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro.
Miongoni mwa wapandaji hao alikuwemo Ofisa Uhusiano wa nje wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom, Maya Makanjee.
Makanjee akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wenzake wa zoezi hilo mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro.
Washiriki wa zoezi hilo wakifurahia Keki iliyopambwa kwa rangi za Bendera ya taifa la Afrika Kusini,na Baba wa taifa hilo,Mzee Nelson Mandela akisalimia.
Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Erastus Runguro akizungumza jambo na muigizaji ,Jacky Devnarain (Rajesh Kumar).
Muigizaji Jacky akisindikizwa na Mhifadhi ,Charles Ngendo kupata sehemu ya kupumzika kwa muda.
Muigizaji Jacky(Rajesh Kumar ) akiwa amepumzika katika eneo maalumu la wageni.
Muigizaji Jacky (Rajesh Kumar ) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Hifadhi za Taifa,Tanzania, Ibrahim Musa.
Keki maalumu iliyotengenezwa na kupambwa kwa rangi za Bendera ya Taifa la Afrika Kusini iliyokabidhiwa kwa washiriki wa zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya familia maskini.(Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini).

DHL and SOS Children’s Villages benefit over 3,500 youths from half a decade of partnership in Africa

$
0
0

dhl_logo2

*Youths from 11 countries reached out to through sponsorship and employee engagement activities

*To date, over 2,000 employees have volunteered in various activities to participate in the partnership

*Inaugural regional conference organized to discuss challenges and future plans

Deutsche Post DHL Group (DPDHL Group) (http://www.dpdhl.com), the world’s leading logistics company, together with non-governmental organization SOS Children’s Villages, have celebrated half a decade of a successful partnership that has helped to improve the employment prospects of disadvantaged young people from SOS Children’s villages across 11 countries in Africa. The partnership between DPDHL Group and SOS Children’s Villages began in 2010 in South Africa and Madagascar and has since expanded to nine other African countries – Ethiopia, Ghana, Kenya, Morocco, Mauritius, Nigeria, Swaziland, Tanzania and Uganda

“Education and employability are highly important topics for Deutsche Post DHL Group and, through our GoTeach program, play a central role in our Corporate Responsibility strategy,” said Christof Ehrhart, Executive Vice President, Corporate Communications and Responsibility, Deutsche Post DHL Group. “We are keen to support the direct development of future logistics talent, but we also firmly believe that education and employability make an important contribution to stability and prosperity in the world, Through five years of partnership with SOS Children’s Villages, we have already seen first-hand the benefits and positive impact that engagement between business and charities that create opportunities for young people can have.”    

“Empowering youth and improving their employment prospects is the objective of the international partnership between SOS Children’s Villages and Deutsche Post DHL Group. The success of our partnership is rooted in the commitment of our employees who volunteer their time to mentor youths aged 15-25 and to help them get ready for their foray into the job market,” said Christoph Selig, Head of GoTeach Program, Deutsche Post DHL Group.

“Employees mentor youths from both SOS Children’s Villages and SOS Family Strengthening Programs, and organize a variety of tailored career development activities that deliver tangible results for the mentees,” he added. “It really has been a joy to see the partnership and correspondingly, our outreach to young people, grow. To date, our employees have engaged with over 3,500 youths in Africa.”

Over the past five years, DPDHL Group has organized a variety of activities in the 11 countries, including job shadowing exercises, mentorship programs between DHL employees and SOS children, skills transfer, internships, sports activities and environmental initiatives.

To discuss challenges and future plans, an inaugural conference will take place over four days in Kenya, with teams from both organizations coming together to jointly develop new ideas on how to further strengthen the partnership in Africa and the Middle East.

Speaking from the inaugural regional Africa DHL-SOS Children’s Villages GoTeach Conference in Karen, Nairobi, where more than 50 participants from both organizations are meeting from July 14 to 17, Tom Were, National Director, SOS Children’s Villages Kenya, said, “While SOS provides a loving home for the children that we care for, DHL enables their independence through their employee volunteer program. The program empowers our youth through exposure to the working world and educating them on the career options available. As a result, our youth become self-reliant, responsible, and contributing members of society. We are looking forward to deepening this partnership and extending our outreach to more youth in Africa over the next few years.”

As part of the DPDHL Group GoTeach program, the Group works with two global partners, Teach For All and SOS Children’s Villages, to improve educational opportunity and employability for young people.

Through its partnership with SOS Children’s Villages, which was established in 2010, DPDHL Group today works with Villages in 26 countries in Africa, Asia, Latin America and Europe.(1) Along with financial support for educational programs and youth facilities, the activities focus on career guidance, teaching basic professional skills and providing young people with their first exposure to the working environment. DPDHL Group collaborates closely with local SOS Children’s Villages to develop support measures tailored directly to the needs of the community.

In 2014, DPDHL Group volunteers organized more than 160 different activities reaching more than 1,600 young people from socially disadvantaged backgrounds, offering over 100 internships and finally permanently employing 25 young talents.

Corporate Responsibility is an integral part of DPDHL Group’s corporate strategy with “Living Responsibility” as its motto. It focuses on environmental protection (GoGreen), disaster management (GoHelp) and education (GoTeach) and supports employee volunteerism through Global Volunteer Day, and the Living Responsibility Fund.

(1) Brazil, Costa Rica, Colombia, Dominican Republic, El Salvador, Ethiopia, Ghana, Haiti, Indonesia, Jordan, Kenya, Lithuania, Madagascar, Morocco, Mauritius, Mexico, Nigeria, Panama, Paraguay, Peru, South Africa, Swaziland, Tanzania, Thailand, Uganda and Vietnam.


These Powerful Pictures Speaks More Than Anything

E-commerce overtaking offline retail

Magufuli aenedelea kujitambulisha na kuwashukuru wanachi wa Chato mpaka Dodoma kwa kishindo

$
0
0

Baadhi ya Wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga na vitongoji vyake wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsalimia kwa  furaha kubwa Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa kwa wananchi hao akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

  Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi ndani ya mji wa Ushirombo,wilayani Bukombe,mkoa wa Geita mapema leo mchna alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisaini vitabu vya ofisi ya CCM juu ya gari ndani ya mji wa Ushirombo,wilayani Bukombe,mkoa wa Geita alipopita kuwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji Bukombe mchana huu alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji wa Masumbwe wilayani Mbogwe mkoa wa Geita mchana huu alipokuwa akipita njiani kuwashukuru na kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.


Baadhi ya Wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga na vitongoji vyake wakimsikiliza Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli  mara baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi hao alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi  alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji wa Kahama mchana huu alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

Baadhi ya Wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga na vitongoji vyake wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsalimia kwa  furaha kubwa Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa kwa wananchi hao akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi ndani ya mji wa Ushirombo,wilayani Bukombe,mkoa wa Geita mapema leo mchna alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisaini vitabu vya ofisi ya CCM juu ya gari ndani ya mji wa Ushirombo,wilayani Bukombe,mkoa wa Geita alipopita kuwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji Bukombe mchana huu alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji wa Masumbwe wilayani Mbogwe mkoa wa Geita mchana huu alipokuwa akipita njiani kuwashukuru na kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.


Baadhi ya Wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga na vitongoji vyake wakimsikiliza Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli  mara baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi hao alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi  alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji wa Kahama mchana huu alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.(PICHA NA MICHUZI JR-CHATO-DODOMA).

Fastjet waja na ‘rout ya 5’!! kuanza safari ya Malawi, Julai 27 mwaka huu

$
0
0

DSC_0263Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro (kulia) akifafanua jambo kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wandishi wa habari akielezea kampuni hiyo ilivyoweza kusaidia sanaa kwa Tanzania na Afrika. Kushoto kwake ni CEO wa ZIFF, Prof. Martin Mhando. 

Na Andrew Chale, modewjiblog

Shirika la ndege la Fastjet  limeendelea kupanua wigo wake kwa kuanzisha ‘rout’   zaidi za safari zake ikiwa ni kuunganisha Afrika kuwa moja.

Kwa mujibu wa Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro  anasema  kampuni hiyo inatarajia kuizindua rasmi  safari zake kwa kwenda, Malawi.

“Julai 27, Fastjet tutazindua rasmi  safari ya kutoka Dar es Salaam-Lilongwe Malawi. Hii inakuwa ni ‘rout’ yetu ya tano  katika safari zetu za Kimataifa ndani ya Afrika… lengo ni kufikia nchi mbalimbali za Afrika.” Anabainisha Lucy Mbogolo.

Hata hivyo anabainisha kuwa,  wanaendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wateja wao juu ya   huduma ya Fastjet  Ambayo imeendelea kuwa bora zaidi kila kukicha huku akisisitiza kwa wateja kufanya ‘booking’ mapema pamoja na kuzielewa sheria na taratibu za usafirishaji wa anga.

Awali Fastjet ilianzia na safari za ndani za kusafirisha abiria ‘rout’ za Mwanza – Dar, Kilimanjaro – Dar na Mbeya – Dar sasa hivi wamevuka mipaka zaidi kwa nchi za Afrika  zikiwemo, kati ya Dar – Johannesburg, Dar – Lusaka, Dar – Harare,Dar – Entebbe nah ii inayotarajiwa kuzinduliwa wiki ijayo ya Dar-Lilongwe.

Aidha, Lucy Mbogoro alibainisha kuwa Fastjet itaendelea kusaidia kukuza sekta ya sanaa nchini na Bara la Afrika kwa kuwaunganisha wadau wa sekta hiyo ikiwemo wasanii wa filamu, muziki na sanaa kwa ujumla.

Lucy Mbogoro anasema hayo ambaapo kwa mwaka huu ni mwaka wa pili mfululizo wakiendelea kudhamini tamasha la Filamu za nchi za majahazi maalufu kama ZIFF. DSC_0311Mwanamuziki wa Kimataifa, Moussa Diallo kutoka Mali (kushoto), akifafanua jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wandishi wa habari. Kulia kwake ni Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro ambao wamedhamini tamasha hilo kwa mwaka wa pili mfululizo kwa upande wa usafirishaji.. DSC_0328Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro  akizungumza na waandishi wa habarimuda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano huo.. (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog).fastjetmoja ya ndege za Fastjet kama inavyoonekana pichani.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu yaendesha mafunzo ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na Malaria jijini Moshi, Kilimanjaro

$
0
0

UFUNGUZI 1

Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kinga, Dkt. Neema Rusibamayila kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii akiwahutubia washiriki wa mafunzo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

UFUNGUZI 2

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo ya awali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

UFUNGUZI 4

Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kinga, Dkt. Neema Rusibamayila kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii akizindua matokeo muhimu ya Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma ya Afya Nchini wa mwaka 2014/2015 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

UFUNGUZI 5 (2)

Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kinga, Dkt. Neema Rusibamayila kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii akionyesha kijitabu cha matokeo muhimu ya Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma ya Afya Nchini wa mwaka 2014/2015 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

UFUNGUZI 6

Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kinga, Dkt. Neema Rusibamayila kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Andrewleon Quaker kijitabu cha matokeo muhimu ya Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma ya Afya Nchini wa mwaka 2014/2015 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Na Veronica Kazimoto, Moshi

Afya ya Uzazi na Mtoto ni viashiria vizuri vinavyoonyesha maendeleo ya uchumi na kijamii na vinaainishwa na utoaji endelevu wa huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Kinga, Dkt. Neema Rusibamayila kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii wakati akifungua rasmi mafunzo ya Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 yaliyofanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro.

“Kutokana na umuhimu wa viashiria hivyo, Serikali kupitia Mpango wake wa Afya ya Uzazi na Mtoto imefanya juhudi za ziada katika kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na matatizo ya uzazi na vifo vya watoto wachanga nchini”, Amesema Dkt. Rusibamayila.

Dkt. Rusibamayila amesema kuwa vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi vimeendelea kupungua ambapo kwa mwaka 2012 kulikuwa na vifo 432 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa hai ikilinganishwa na vifo 454 kwa kila watoto waliozaliwa hai 100,000 iliyopatikana kwenye Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa mwaka 2010.

Vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka vifo 51 kati ya watoto 1,000 waliozaliwa hai kama ilivyopatikana kutoka kwenye Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa mwaka 2010 na kufikia vifo 45 kati  ya watoto 1,000 waliozaliwa hai kwa mwaka 2012.

Aidha, Dkt. Rusibamayila ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo amewaasa washiriki hao kufanya kazi yao kwa weledi ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata takwimu sahihi za  Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 kwa ajili ya kupanga maendeleo.

Pamoja na ufunguzi wa mafunzo hayo, Mgeni rasmi huyo amezindua matokeo muhimu ya Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma ya Afya Nchini wa mwaka 2014/2015.

Matokeo ya utafiti huo yanaonyesha kuwa, vituo saba (07) kati ya kumi (10) vinatoa huduma zote za msingi za afya yaani tiba kwa watoto, chanjo pamoja na ufuatiliaji wa mwenendo wa ukuaji wa mtoto.

Aidha, huduma za matibabu kwa watoto wagonjwa zinapatikana kwa asilimia 98   katika vituo vyote vinavyotoa huduma za afya Nchini, pia zaidi ya vituo vinane (8) kati ya kumi (10) nchini vinatoa huduma za chanjo kwa watoto.

Kwa huduma za kisasa za uzazi wa mpango zinapatikana kwa asilimia 80 ya vituo vyote vinavyotoa huduma za afya, ikilinganishwa na asilimia 76 kwa utafiti wa namna hii wa mwaka 2006.

Aidha,  kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2014/2015 karibu vituo vyote vya Serikali (sawa na asilimia 97) vinatoa huduma za uzazi wa mpango ikilinganishwa na asilimia 35 ya vituo binafsi vya kibiashara na asilimia 41 ya vituo vinavyomilikiwa na asasi za kidini.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo amesema utafiti huu wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015  unalenga kukusanya taarifa nyingi za sekta ya afya zinazotumika katika kutathmini malengo mbalimbali na pia kusaidia katika kupanga mikakati mipya.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mara nyingine tena inafanya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ambao kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2010. Utafiti huu utaanza rasmi mwishoni mwa mwezi Agosti, 2015 kwa nchi nzima yaani Tanzania Bara na Visiwani.

Prof. John Nkoma awarded at EACO Congress in Kampala

$
0
0

Prof.  John Nkoma Awarded at EACO Congress- Kampala

Hon. Nyombi Thembo, Minister of State for Information and CommunicationsTechnologies  (ICTs) Uganda  gives an award of appreciation to Prof. John S. Nkoma for having served as a Founding Executive Committee Member of the East African Communications Organization (EACO) and “Eleven years of excellent service and development with Tanzania Communications Regulatory Authority!(TCRA)” as Director General, from 2004 to June 2015. The award was presented to Prof. Nkoma during the 21st EACO Congress and Assemblies held in recently Kampala, Uganda. (Photo by a Correspondent)

 

Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF), wakutana na wahariri, Dar

$
0
0

MKURUGENZI Mkuu wa kwanza wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, akiwasilisha mada wakati wa warsha iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa Wahariri kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam, Julai 22, 2015

Na K-VIS MEDIA

MFUKO wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umekutana na Wahariri wa vyombo vya Habari nchini, kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam, Julai 22, 2015, kwa nia ya kujitambulisha na kuelezea mikakati yake ya kiutendaji na majukumu iliyo nayo.

Akiwasilisha mada kwa Wahariri hao, Mkurugenzi Mkuu wa Kwanza wa Mfuko huo, Masha Mshomba, amesema, Mfuko huo umeanzishwa ili kutekeleza sheria ya fidia kwa wafanyakazi (Sheria namba 20, ya mwaka 2008.

“Majukumu ya Mfuko huu ni kuwasaidia wafanyakazi wanaoathirika kuweza kurudi kazini au kushiriki katika shughuli nyingine zitakazowapa kipato.” Alisema Mshomba na kuongeza kuwa majukumu mengine ni pamoja na kutunza kumbukumbu za matukio ya ajali, magonjwa na vifo vinavyotokana na kazi, ikiwa ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu kazi za mfuko na manufaa yake

Alisema, Mfuko huo ni mpya na kwamba unahitaji ushirikiano wa dhati kutoka vyombo vya habari na ndio maana Mfuko umeona umuhimu wa kukutana na Wahariri wa vyombo vya habari kwani wao ndio kiungo kati ya Mfuko na Umma.

Akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Irine Isaka, amesema, Mfuko huo umekuja kurahisisha ushughulikiwaji wa malalamiko ya fidia kwa wafanyakazi moja kwa moja bila ya kuanza kupitia sehemu nyingine.

Alisema, SSRA kama mama wa Mifuko yote, inao wajibu wa kuisaidia WCF katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria na Wahariri wa vyombo vya Habari ni kiungo muhimu katika kuhakikisha umma wa Watanzania unajua shughuli na kazi za Mfuko huo.

Naye kwa upande wake, Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena alishukuru WCF kwa kuwaalika wahariri ili kuwaeleza vema shughuli na majukumu ya Mfuko huo kwani vyombo vya habari ndio wakala wa Umma na taasisi za kutoa huduma kama WCF.

Ninawapongeza WCF kwa kuwa majasiri wa kuwaalika wahariri na kukutana nao na kupokea maswali yao, kwani taasisi nyingine huogopa kufanya hivyo tena katika hatua ya awali kama yenu, alisema Meena.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Irine Isaka, akifungua warsha hiyo.

Mhariri Shemax Ngahamera akizungumza kwenye warsha hiyo.

Mhariri wa vipindi wa ITV/Radio One, Steven Chuwa, (kulia), na Mhariri Mtendaji wa EFM, Scolastica Mazula, wakipitia mada zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.

Mhariri Mshiriki wa gazeti la Nipashe, Ramadhan Mbwaduke, akiuliza swali.

Mhariri gazeti la Serikali, Sunday News, Ichikaeli Maro, akizungumza wakati wa warsha hiyo.

Baadhi ya Wahariri wakinukuu yaliyokuwa yakielezwa kwenye warsha hiyo.

Mhariri Anold Victor, akiuliza swali.

Mhariri mkongwe, Mzee Yasin Sadick, akifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye warsha hiyo.

Baadhi ya Wahariri, wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa juu ya kazi na huduma zitolewazo na WCF.

Mhariri  wa kujitegemea Mzee Wence Mushi akiuliza swali.


Jumuiya ya watanzania wa DMV na washirika wao watoa huduma za kimatibabu na madawa bure katika hospitali ya Mwanayamala jijini Dar‏‎

$
0
0

Mkurugenzi wa Taasisi ya kinamama wa Kiafika inayohusika na ugonjwa wa Saratani ya matiti Bi. Ify Nwabuku(kushoto) akizungumza na wakina mama (hawapo pichani) wakati wa utoaji wa matibabu bure kwa wakina mama katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar. Kushoto ni Bi Asha Nyang’anyi ambaye ni mwanakamati wa ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumiwa jumuiya ya Watanzania DMV.

DSC_0179

Wakina mama wakimsikiliza kwa makini Bi. Ify Nwabuku wakati akitoa maelezo juu ya upimaji wa Saratani kwa wakina mama waliofika kupima afya zao katika hospitali ya Mwananyamala zilizokuwa zikitolewa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao walioamua kutoa huduma za kitabibu na madawa bure.

Dk. George Quintero(kushoto) kutoka Marekani akimtibu meno mtoto Living Andrew aliyeshikwa na mama yake huku akisaidiana na Dk. Emilton Ndashau (kulia) wakatia wa utoaji wa uduma bure iliyodhaminiwa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.

DSC_0189

Dk. Somtochukwa Agunwah (kushoto) kutoka Marekani akimtibu mmoja wa mama aliyekuwa anaumwa jino katika hospitali ya Mwananyamala huku akisaidiwa na Dk. Kilechi Nwankwo(kulia) kutoka Marekani pamoja na Dk. Kisumo Armogaston.

Dk. William Desdery ambaye ni daktari wa macho akimtibu mmoja wa wakina mama waliofika katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar kwa ajili ya matibabu yanayotolewa bure na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao.

Dk. Sharon Sagoo akipima dawa zilizotolewa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao  kwa ajili ya kupewa wagonjwa waliofika kupata matibabu katika hospitali ya Mwananyamala.

 

Dk. Jummy Amuwo akihakiki madawa.

Hizi ni baadhi ya Dawa zilizotolewa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao kwa ajili ya wagonjwa wa Hospitali ya Mwananyamala na pia zinatolewa bure.

Rais wa Jumuiya ya Jumuiya ya Watanzania DMV, Bw. Iddi Sandaly(kustoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi. Adama Gibateh(katikati) pamoja na Kushoto ni Bi Asha Nyang’anyi ambaye ni mwanakamatiwa ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumiwa jumuiya ya Watanzania DMV.

Here comes Women’s empowerment show, successful women in the spotligh

$
0
0

fatema 1

fatema 2

fatema 3

Educate, Empower and Inspire is a women’s empowerment show. The aim of this show is to put successful women in the spotlight and get a glimpse as to how they are making a difference to our society and how they can inspire others to do the same.

My first guest was Dr. Trish Scanlan who runs the paediatric oncology department at Muhimbili hospital. Since her involvement in 2008, along with her dedicated team of Tanzanian doctors and nurses, the short term survival rates of children with cancer rocketed from 12% to 60%.

check out the full interview here below;

The Potentiality of E-Commerce Innovation in Tanzania

$
0
0

jovago 1

The growth of ICT utilization in Tanzania particularly the internet and mobile phones has influenced the rate of online interaction and communication among the vast populace. The growth of internet usage in Africa has led to the revolution of communication, commerce, and development into a globalized world. Due to the potentials of the internet, many individual users and content providers are at the critical stage of creating more connections in the business.

Tanzania, in recent years, has experienced a tremendous digital revolution due to telecommunication developments. Many entrepreneurs from both within and outside the country have greatly exploited the opportunity to invest through e-commerce as the way of generating income and improving service delivery to customers and this leads to growth of the economy.

According to the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) report of 2014, there is approximately an increase of about 9 million internet users in the country. This proves that the communication technological development in the country has accelerated and attracted more users compared to the past years when the internet use was very low.

Moreover, the influx of smart phones and other internet supporting devices like portable computers have facilitated online business due to user-friendly features and low cost of internet use in the country. The wide use of smart phones by the majority in the country has made it easy for the investors to get connected with customers wherever they are, hence overcoming the distance barriers.

Furthermore, the booming of e-commerce opportunities and services in the country has brought about several advantages which can be seen through multiple entrepreneurship tenures that keep the online business growing day to day. Some of the companies that have emerged in the country to utilize business opportunities include Jovago.com and many others in the traveling, insurance and banking sectors just to mention few. Some of the changes which have been created through e-commerce in Tanzania can be inscribed as follows;

Less expense of advertising and marketing: The Tanzania Trade Development Authority argues that, “The essence of e-commerce has helped business enterprises or suppliers with marketing services online by enabling them to place their products and services before their target customers, this potential opportunity helps service providers attract a vast number of consumers by speeding up the flow of information from their end to other heterogeneous consumers”. The break has helped entrepreneurs to overcome and escape from the huge costs that come with traditional media advertising such as televisions, radios and newspapers.

Physical and digital goods: People are able to sell and buy goods or services online. The essence of online services has removed the middlemen, as service providers and consumers are linked via internet hence removing the previous barriers of middlemen. With e-commerce, prices and services can be seen right away and agreement can be made and reached in no time.

Getting reliable services right away: Businessmen and consumers have succeeded to overcome the distance bottleneck in selling and buying goods or services. “It is now easy for an individual to sell and buy a product or service inside and outside Tanzania. One can order a service regardless of location, all that is needed is internet access. For example, Jovago Tanzania offers plenty of opportunity and services for people around the globe to book hotels, and travel services in their prospective targeted destination, thus easing your vocations to the maximum”  Andrea Guzzoni , Country Manager of  Jovago Tanzania argued.

Interconnectedness of consumers and service providers: With e-commerce, the businessmen can easily attend to numerous consumers at the same time and also provide immediate feedback. Also electronic commerce is an easy way of receiving questions about product and services, also improving response to customer queries. It also provides an easy opportunity to work even beyond the normal service working hours.

Hence, e-commerce is accelerating the growth of economies at an individual level, company and state at large through GDP. It has also led to the improvement of service delivery to consumers and easily meeting consumer’s demands and satisfaction    

Testing for Malaria reduces over prescription by over 70%

$
0
0

LSHTM LOGO BLK

act

150722act

Drug shop in Uganda.

*Introducing rapid diagnostic tests in Ugandan drug shops improves treatment of malaria patients

Using malaria rapid diagnostic tests (RDT) in registered drug shops in a highly endemic region in Uganda substantially reduced over diagnosis of malaria, improving the use of valuable malaria drugs, according to a new study published in PLOS ONE.

Most of the 15,000 patients that visited drug shops with a fever chose to buy an RDT when offered one by the trained vendors taking part in the study. Once they performed the test, results showed that less than 60% of the patients had, in fact, malaria. The vendors usually complied with the test results, reducing over prescription of malaria drugs by 73%.

The researchers from the Artemisinin-based Combination Therapy (ACT) Consortium (http://www.actconsortium.org) at the Ministry of Health in Uganda and the London School of Hygiene & Tropical Medicine in the UK carried out the study because up to 80% of malaria cases in Uganda are treated in the private sector.

The private sector is a common source of treatment in many other malaria-endemic areas, especially where there is poor access to public health facilities. Patients buy antimalarial drugs in shops to medicate themselves, although malaria is not always the cause of their fever, and thus inappropriate treatment is very common.

Prof. Anthony Mbonye from the Ugandan Ministry of Health and lead author of the study, said: “Our findings show that it is feasible to collaborate with the private health sector and introduce malaria RDTs in drug shops. The next step is to refine the strategy and understand the cost implications of scaling it up in Uganda. Our long term aim is to provide evidence to help the World Health Organization develop guidance to improve malaria treatment in the private sector.”

Dr Sian Clarke from the London School of Hygiene & Tropical Medicine, also a principal investigator in the research, said: “This study shows that RDTs can improve the use of ACTs – the most effective treatment for malaria – in drug shops, but it’s not without its challenges. These tests alone will not improve the treatment of other diseases. We now need to continue working with the Ministry of Health to investigate how to improve our approach and expand it to other common illnesses.”

At present, drug shop vendors usually treat patients based on their signs and symptoms without testing their blood for the presence of malaria parasites, as recommended by the World Health Organization. This can result in patients with a fever being over diagnosed with malaria and purchasing an ACT which they don’t need.

Microscopy is a method that requires laboratory equipment and qualified staff, while RDTs are alternative, simple tools that require minimal training to diagnose malaria. These rapid tests can help health workers and vendors in remote locations to prescribe the correct treatment for malaria.

An investigation conducted alongside the trial, published in Critical Public Health, found that despite their popularity, malaria tests were not a simple fix in the private sector. Patients welcomed the RDTs as well as government involvement in improving drug shops, and vendors “felt big” and more akin to qualified health workers in the public sector for being allowed to test blood. But researchers warn that this could give a false impression of vendors’ other skills and services, and regulation by authorities is needed.

The team have recently received a new grant to investigate the feasibility of training and equipping registered drug shops to manage three key childhood diseases: malaria, pneumonia and diarrhoea.

The ACT Consortium is funded by a grant from the Bill & Melinda Gates Foundation to London School of Hygiene & Tropical Medicine.

Wakazi wa Dar es salaam kupata matibabu yatakayotolewa na wataalamu kutoka Hospitali za Apollo

$
0
0

apollo-03

apollo-04

Watanzania wanashauriwa kuitumia fursa hii ya kipekee ya ziara ya kitabibu itakayofanywa na madaktari kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad.  Kwa miaka mingi, watanzania wameshindwa kupata matibabu sahihi nchini kitendo ambacho kimewasababishia kusafiri nje ya nchi kupata matibabu sahihi ya mfumo wa fahamu, uti wa mgongo, figo pamoja na magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo.  Nia na madhumuni ya ziara ya madaktari na washauri hawa kutoka Hospitali za Apollo nchini Tanzania ni kuhakikisha kwamba wagonjwa wanapata vipimo sahihi kwa gharama nafuu. Madaktari bingwa watatu wanao ongoza katika Hospitali za Apollo watafanya kazi kwa kushirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Hindu Mandal kutoa huduma za kimataifa kwa watanzania.

Wagonjwa wanaougua magonjwa yanayohusiana na uti wa mgongo, mishipa ya fahamu, figo na magonjwa ya kibofu cha mkojo, wanashauriwa kuhudhuria na kushiriki tukio hili la kipekee. Madaktari watatembelea wagonjwa, kufuatilia historia za wagonjwa na kuwashauri matibabu sahihi kutokana na ripoti za matibabu na vipimo.

Daktari wa kwanza atakayeshiriki katika kutoa ushauri na matibabu ni Dkt. Alok Ranjan ambaye ni mtaalamu katika upasuaji mishipa ya fahamu na uti wa mgongo katika Hospitali za Apollo mjini Hyderabad.  Atapatikana siku ya Jumatatu ya tarehe 27 Julai na tarehe 28 Julai kati ya saa 03 asubuhi  na 11 jioni kwa tarehe hizo mbili katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam.  Dkt. Alon Ranjan ni mtaalamu anayeongoza katika upausaji wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kwa zaidi ya miaka 20 kwa kufanya upasuaji mgumu wa mishipa. Dkt. Alok Ranjan ameongoza timu yake kufanya  pasuaji mbali mbali za mishipa ya fahamu zaidi ya 1,000  kama vile upasuaji mdogo wa mtindio wa ubongo, upasuaji wenye madhara madogo wa uti wa mgongo, upasuaji mgumu wa uti wa mgongo, na upasuaji kwa kutumia kifaa maalumu cha kuangalia uti wa mgongo na ubongo.  

Kliniki ya ushauri na tiba ya pili imepangwa kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 31 Julai na 01 Agosti katika Hospitali ya Hindu Mandal ya Dar es salaam. Wagonjwa watapata fursa ya kupata ushauri na tiba kutoka kwa Dkt. Rajagopal ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa uzazi na Dkt. Sanjay Maitra ambaye ni mtaalamu wa figo kati ya saa 3 asubuhi na saa 11 Jioni kwa siku za Ijumaa na Jumamosi. Huduma hizi za ushauri na tiba, zitatolewa kwa gharama nafuu.

Dkt. Rajagopal  amebobea katika magonjwa ya mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi kwa wanaume. Amekuwa mshauri mwandamizi wa tiba wa magonjwa ya vina vya uzazi katika Hospitali za Apollo mjini Hyderabad tangu mwaka 1994.

Dkt Sanjay Maitra amebobea katika huduma na tiba za magonjwa ya figo na magonjwa yanayo shabihiana na haya.  Kwa kawaida madaktari hawa hutibu magonjwa sugu ya figo, uvimbe katika figo, figo zilizoshindwa kufanya kazi na jiwe figo ikiwa ni pamoja na kuelimisha juu ya masuala mbali mbali ya upandikizaji wa figo na usafishaji.  Dkt. Sanjay Maitra ana uzoefu wa miaka mingi katika tiba ya figo na alimaliza masomo yake ya utaalamu wa magonjwa ya figo kutoka katika chuo cha AIIMS mjini New Delhi. Dkt Sanjay Maitra pia amekuwa akitoa mafunzo ya upandikizaji wa figo kutoka katika miili iliyo kufa na iliyo hai, huduma muhimu za ubadilishaji wa figo, usimamizi wa mda mrefu wa usafishaji wa figo kwa wagonjwa.

Hii siyo mara ya kwanza kwa madaktari hawa kutembelea Dar es salaam.  Ushirikiano huu endelevu na Hospitali ya Hindu Mandal unathibitisha dhamira ya Hospitali za Apollo katika kutoa huduma bora za afya na nia thabiti ya kuendeleza mahusiano na Tanzania ambayo yameazishwa kwa Zaidi ya muongo mmoja.

Katika siku hizi ambazo madaktari hawa watatoa tiba na ushauri,  Dkt. Alok Ranjan, Dkt. Sanjay Maitra na Dkt. Rajagopal watakuwa wanapitia kujua hali za wagonjwa ambao waliwahi kutibiwa mjini Hyderabad au ambao walitibiwa kipindi ambacho madaktari hawa walitembelea Dar es salaam mara ya mwisho.  Katika kipindi hiki, madaktari hawa watafanya mahojiano na wagonjwa kujua historia ya ugonjwa wao, kuwafanyia vipimo, kujadili sababu zinazoweza kuwa vyanzo vya ugonjwa wao, matibabu yanayoweza kutolewa inchini, kuwaandikia wagonjwa dawa na kufanya mipango ya vipimo au kupendekeza matibabu ya ziada.  Kwa baadhi ya wagonjwa, kutegemeana na ukubwa wa tatizo la mgonjwa na hali yake, wagonjwa wanaweza kushauriwa kutafuta matibabu zaidi nje ya nchi kwa matibabu ambayo hayawezi kufanyika nchini Tanzania.  Katika kipindi hiki, wagonjwa watajadiliana na madaktari majibu ya vipimo au ripoti za vipimo vilivyofanyika hivi karibuni.  Kliniki hii ni fursa ya kipekee kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa yahusianayo na uti wa mgongo, mishipa ya fahamu, figo na magonjwa ya kibofu cha mkojo na ambao wanahitaji ushauri mbadala au wale ambao hawawezi kumudu gharama za kupata matibabu nje ya nchi.

Ndugu Radhey Mohan, Makamu wa Raisi wa Maendeleo ya Kimataifa Kibiashara anadhamini kliniki hizi kwa kushirikiana na Hospitali ya Hindu Mandal.

Wagonjwa wanahamasishwa kufaidika na kufursa hii na wanashauriwa kujiandikisha kupata ahadi ya  kuwaona madaktari hawa katika Hospitali ya Hindu Mandal kwa kupiga simu nambari +255 22 211 4991-4

Viewing all 5755 articles
Browse latest View live