Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Waziri wa Habari Dkt. Fenella Mukangara azindua Baraza Jipya la Kiswahili

$
0
0

IMG_0875

Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara akitoa hotuba kwa wajumbe wa Baraza jipya la Kiswahili na kulitaka Baraza hilo kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika kutoa elimu ya matumizi fasaha ya Kiswahili sanifu ili kupunguza upotoshwaji wa matumizi ya lugha ya Kiswahili.Kulia ni Mwenyekiti Mpya wa Baraza la kiswahili Bi.Martha Qorro.

IMG_0849

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa kulitumikia Baraza la Kiswahili Bw.Suleiman Hegga akitoa hotuba na kuwataka wajumbe wa Baraza la Kiswahili kushikamana na kuendeleza yale waliyoanza ili kukiletea kiswahili maendeleo Afrika na duniani kwa ujumla.katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko na Kulia ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara.

IMG_0797

Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara akimpa zawadi mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa kutumikia Baraza la Kiswahili Bw.Suleiman Hegga wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la Kiswahili Jijini Dar es Salaam.

IMG_0750

Wanakikundi cha fataki wakitoa Igizo kwa Njia ya ushairi lililosisitiza matumizi bora ya lugha ya Kiswahili kwa maendeleo ya lugha hiyo afrika na duniani kwa ujumla,wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la Kiswahili iliyofanyika katika ukumbi wa uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam.

IMG_0765

Wanakikundi cha fataki wakimsalimia Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara(aliyesuka) wakati wa hafla ya uzinduzi Baraza jipya la Kiswahili Jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Profesa Hermas Mwansoko,Kushoto kwake ni Mwenyekiti Mpya wa Baraza hilo Bi.Martha Qorro na wa Mwisho ni Makamu Mwenyeki Bw. Omar Kiputiputi.

IMG_0789

Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara(kulia)akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Profesa Hermas Mwansoko,wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza Jipya la Kiswahili Jijini Dar es Salaam.

IMG_0871

Wajumbe wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) wakimsikiliza Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la Kiswahili iliyofanyika katika ukumbi wa uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam.

IMG_0892

Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza Jipya la Kiswahili.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles