Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Asilimia 45 ya wanaolazwa hospitalini ni kutokana na ulevi wa kupindukia nchini Uingereza

$
0
0

Dejected businessman having drink at bar

.Takwimu zinasema wagonjwa wengi waliolazwa ni madhara ya kunywa pombe kupita kiasi

.Takwimu za huduma za jamii ongezeko la wagonjwa ni mara mbili katika miaka kumi

.Wanawake vijana waongezeka hospitalini kwa magonjwa yanayohusiana na pombe

Na Damas Makangale, MOblog kwa Msaada wa Mtandao

Takwimu zilizotolewa na Serikali ya Uingereza hivi karibuni idara afya na Huduma za Jamii zinasema kwamba wagonjwa nchini Uingereza wanatokana na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Takwimu zinasema kwamba magonjwa yanayotokana na ulevi wa kupindukia yameongezeka maradufu hasa kwa vijana wenye umri wa miaka 45 kwenda chini na takwimu zinasema wagonjwa wameongezeka mara mbili ndani ya miaka kumi.

Ongezeko hilo ni maradufu sana kwa vijana na inaonyesha kwamba ugonjwa wa ini unasababishwa na ulevi wa kupita kiasi na hasa unywaji wa pombe kali na tatizo hilo limejitokeza sana kwa watu wenye umri wa kati hasa vijana.

Takwimu kutoka  idara ya Afya na Huduma za Jamii zinaonyesha kwamba mwaka 2012/13 , jumla ya watu 26,209 na wanawake 12,461 wenye umri wa miaka 45-49 kulazwa hospitalini kutokana na pombe au ulevi wa kupindukia.

Katika kipindi hicho kulikuwa na asilimia 178 katika watu waliolazwa wenye umri wa miaka 65-69 na ongezeko la asilimia 177 katika wanawake waliolazwa wenye umri wa miaka 60 hadi 64.

Wataalam wanasema kuwa hiyo ilikuwa mkusanyiko wa madhara ya maisha ya muda mrefu ya kunywa pombe hasa kwa vijana na wakinamama wajawazito baada ya Serikali kuondoa vikwazo kadhaa vya unywaji wa pombe kati ya 1960 na 1970.

Mkuu wa Idara ya Afya nchini Uingereza, Julia Manning amesema : ‘mara nyingi matatizo ya ini au figo yanasababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi lakini kwa siku za karibuni unywaji wa pombe kwenye jamii umekuwa maradufu.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles