Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Waziri Dk.Nchimbi azindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi

$
0
0

IMG_2363

 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova alipowasili kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam.

IMG_2364

  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema.Kulia ni  Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova. Kushoto ni Wanamawasiliano kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu na Sangita Khadka.

IMG_2370

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema akimtambulisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kwa baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kuwasilia eneo la tukio.

IMG_2374

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akibadilishana mawazo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema (kushoto) na Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova wakati wakielekea jukwaa kuu.

IMG_2377

 Balozi wa Ireland nchini Fionnuala Gilsenan (katikati) akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (kushoto) Kulia ni Mkuu wa Mabalozi wa EU nchini Filiberto Sebregondi.

IMG_2381

 Pichani juu na chini Maandamano yakiwasili kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.

IMG_2384

IMG_2385

 Taasisi mbambali zikiwa zimebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kutokomeza ukatili wa Kijinsia.

IMG_2388

IMG_2394

 Meza Kuu ikipokea maandamano.

IMG_2398

 Burudani kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.

IMG_2459

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake kwa Askari na Maofisa wa Jeshi la Polisi, Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali pamoja na wakazi wa Temeke kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini. 

IMG_2438

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou 

IMG_2409

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema akizungumza kwenye uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.

IMG_2419

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi akizungumza kwenye hafla hiyo.

IMG_2431

  Balozi wa Ireland nchini Fionnuala Gilsenan akizungumza kwa niaba ya nchi yake ambapo amesema Ireland itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa ukaribu zaidi.

IMG_2460

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizindua kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi katika uzinduzi uliofanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, wa pili kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou, wapili kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi na Kushoto ni Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini

IMG_2465

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikionyesha kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi katika uzinduzi uliofanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam.

IMG_2469

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akimshukuru Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou mara baada ya kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi ulio chini ya Umoja wa Mataifa.

IMG_2471

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuzindua ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto katika Mkoa wa Kipolisi Temeke. Kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi.Waziri Nchimbi katika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini. 

IMG_2473

Sasa imezinduliwa rasmi.

IMG_2481

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali baada ya waziri huyo kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema.

IMG_2486

 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou akiteta jambo na mmoja wa maafisa wa Jeshi la Polisi mara baada ya uzinduzi huo.

IMG_2497

 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou akifanya mahojiano na mwandishi wa habari wa redio wa BBC. Katikati ni Afisa Habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Usia Nkhoma Ledama.

 

IMG_2499

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini, Dr. Alberic Kacou mara ya uzinduzi.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles