Documentary hii inayoonyesha mafanikio ya zoezi la Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii au Social Monitoring and accountability (SAM) katika wilaya ya Iramba lililoratibiwa na Shirika la Sikika. Dhana hii ya SAM inalenga kuwapatia uwezo wananchi na wawakilishi wao katika ngazi ya jamii kufuatilia utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya afya na UKIMWI na kudai uwajibikaji kwa viongozi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
↧