Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni, Paul Makonda akiwa na maafisa wa jeshi la Polisi wakielekea eneo la nyuma jirani na ofisi za madereva.
“Huenda hufahamu…basi tunakufahamisha sasa!!!
Na Andrew Chale,Modewji blog
Matukio kuanzia asubuhi:
Mtandao wako bora ambao ulipiga kambi ndani ya kituo cha mabasi Ubungo na kulala hapa hapa, umeweza kukusanyia wewe msomaji wetu matukio muhimu ambayo yameweza kupatikana kuanzia usiku, asubuhi na hadi mchana ulipomalizika mgomo huo wa madereva leo Mei 5, majira ya saa sita mchana mgomo ambao umedumu zaidi ya masaa 31.
Hali ya usiku ndani ya kituo kulikuwa na baridi kali pia pamoja na mvua mvua iliyokuwa ikinyesha na kuacha. Abiria wengi walilala kwenye magari ambayo walikwisha katia tiketi zao huku wengine wakilala kwenye banda la kusubiria wasafiri wanaowasili na wanaoondoka.
Ndani ya vibanda vya biashara hali ilikuwa shwari kabisa kwani kila mmoja alikuwa akiendelea kupata hiki na kile ikiwemo vinywaji na chakula huduma ambayo ilikuwa ikitolewa muda wote na watu walikuwa ni wengi.
Vijana wa ‘kihuni’ watulizwa
Hali ya usalama ilikuwa imeimarishwa hasa kwa vijana wa kihuni pamoja na watoto wadogo ambao kazi yao kubwa ni kuokotaokota vitu ndani ya kituo hicho cha mabasi ambapo ulinzi shirikishi walikuwa wakipita kila mahala ndani ya stendi hiyo katika kuhakikisha usalama.
Hata hivyo baadhi ya magari yaaliweza kuwasha Tv, kwa kuweka mikanda na abiria kuangalia sinema huku wengine wakiwa wamelala. Baadhi ya mabasi ‘classic’ abiria wao hawakupata sana taabu kama wengine kwani wao ndani ya mabasi yao, waliwasha ‘kipupwe’ na wengine feni huku wakitazama Tv ikiwemo chaneli za kawaida za nje na ndani pia baadhi ya viti vyao vilikuwa rafiki hata kwa matumizi ya kulala.
Usiku huo ulivyokuwa ukionekana ndani ya kituo hicho cha mabasi Ubungo.
Mwanamke kujifungua mtoto
Miongoni mwa matukio katika mgomo huu ni la mwanamke kujifungua mtoto. Mwanamke huyo, ambaye imeelezwa alikuwa anaelekea katika moja ya mikoa ya Kusini, alishikwa na uchungu usiku wa manane wakati amelala ndani ya gari hali iliyopelekea kujifungua huku akisaidiwa na wanawake wengine waliokuwa pamoja ndani ya gari usiku huo.
‘Hope fail’
Majira ya saa 10, kasoro usiku huo, baadhi ya abiria walianza kuamshana juu ya hatima ya safari zao kama zitakuwapo ama la na wao wachukue maamuzi. Hata hivyo tumaini lao hilo, lilipotea kadri muda ulivyozidi kuendelea na kukucha kwani madereva walikuwa wakiwaambia kuwa kwa sasa gari hazitoondoka mpaka hapo watakapohakikishiwa matakwa yao, hali ambayo ilizidi kuwanyong’onyesha na kupoteza tumaini kwa abiria hao ama tunaweza sema ‘hope fail’.
Saa moja kasoro, baadhi ya mabasai ya Shabiby Line Bus, yaliweza kuhamasisha abiria wake waingie kwenye magari kwa ajili ya safari, hata hivyo gari ya kwanza iliyotoka iliweza kusindikizwa kwa ‘eskoti’ huku ikizomewa katika maeneo ya Ubungo ilipokuwa ikitoka, hata hivyo gari hilo, kwa mujibu wa watu waliokuwa maeneo ya Mbezi walieleza kuwa, ilipokelewa mawe, licha ya kuendelea na safari zake ambapo taarifa zaidi pia tutawaletea kadri zitakapopatikana kuwa nasi.
Mbali ya hilo, kuondoka, pia mabasi mengine ya Shabiby, yaliweza kutoka likiwemo lile lililokuwa likielekea Dodoma pamoja na lile la Msimbati Line Bus, ambalo ni ndugu na Shabiby Line lililokuwa likielekea Mtwara. Katika safari hizo za mapema, mabasi hayo ya Shabiby pamoja na yale ya Dar Express kwa pamoja yaliondoka muda huo wa saa tatu kasoro huku yakiwa na msafara wa Polisi.
‘Osama akamatwa na Trafiki Ubungo’
Katika kile ambacho kilionekana kuwa Osama kutaka kufanya yake, Polisi wa Usalama Barabarani ‘trafiki’ aliweza kumvaa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la utani Osama na kumkamata baada ya trafiki huyo kumuamuru aondoke mahala alipokuwa amesimama jirani na basi la Shabiby.
Osama alimtolea lugha ya matusi trafiki huyo hali iliyopelekea maafisa usalama, polisi na mgambo waliokuwa wameweka usalama mahala hapo kuingilia kati na kumtia nguvuni, lakini Osama ‘aliwadindia’ huku vijana mbalimbali wapiga debe na abiria wakipiga kelele za kumzomea askari trafiki kwa kitendo chake cha kutaka kumkamata. Hata hivyo, tukio hilo lilimalizika kimya kimya baada ya Osama kuachiwa na kisha kuondoka zake.
Askari wa Polisi usalama barabarani ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiwa amemkunja ‘Osama’ baada ya wawili hao kutofautiana kiswahili. ‘Waanifahamu’ kizanzibar aaaah.!!
Osama akiwa katika uso wa ‘kummaindi’ trafiki aliyemzingua kituoni hapo.
Abiria wataka kuandamana
Hali ya abiria baada ya kuona kuwa mbaya, majira ya saa tatu asubuhi, waliamua kukusanyana makundi huku wakihamasishana waandamane kushinikiza wasafirishwe. Abiria hao walikuwa na hoja mbalimbali ikiwemo kushinikiza jeshi hilo kuweza kuwasaidia wasafirishwe ama wachukue hatua baada ya kuona baadhi ya makampuni ya Shabiby wakianza safari zao huku baadhi ya magari mengine yakiwa hayajui hatima yake.
Abiria hao wakitoa malalamiko yao kwa mwanahabari juu ya kutaka kufanya maandamano, lakini baadae waliamua kupotezea..
Mwanadada ajitoa ‘muhanga’ kutetea abiria wenzake
Mwanadada Khadija Muhando, ambaye ni mwenye Albinisimu, aliyekuwa akisafiri kuelekea Mkoani Arusha, aliweza kupenya na kuingia katikati ya maofisa wa jeshi la Polisi na kuanza kutoa kilio chake huku akitaka kujua hatima yao ya safari.
Mwanadada huyo, alimvaa Kamanda Mkuu wa Usalama barabarani nchini, Kamanda Mpinga na maofisa wake na kuanza kumlazimisha aamuru madeeva wawasafirishe, Khadija aliwasumbua mara kwa mara viongozi hao huku wakati mwingine wakiamua na kwenda kusimama mahala pengine lakini naye aliapa kuwa atakula sahani moja na hadi apate jibu la pamoja.
Khadija Muhando akionekana kumvaa Kamanda Mpinga ili atoe amri abiria waruhisiwe kuondoka, licha ya Kamanda Mpinga kumwelezea dada huyo kuwa mgomo unashughulikiwa asubiri kidogo..
Hali iliendelea kuwa hivi. Kamanda Mpinga na abiria wakizozana juu ya kumaliza mgomo huo..!!
Abiria Khadija Muhando akiwa anajadiliana na askari kanzu aliyefika eneo hilo, lakini naye hakufua dafu alimwambia akae pembeni kwani sio saizi yake katika kile anachokitaka yeye hapo juu ya kupewa jibu sahihi..!
Muafaka bado..!
Hata walivyokuja viongozi, Khadija alikaa pembeni huku akisubiria kuwabana viongozi hao..!
Muafaka bado..!
Mkuu wa Wilaya Paul Makonda awasili Ubungo
Mkuu wa Wilaya Paul Makonda aliwasili katika kituo hicho majira ya saa nne asubuhi ambapo baada ya muda waliamua kuwafuata baadhi ya viongozi wa madereva na wamiliki waliokuwa wamekaa nyuma kabisa ya kituo hicho cha mabasi jirani kabisa na ofisi ya madereva.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Makonda alipowaili Ubungo..!
Mkuu wa Wilaya Makonda, akiwasikiliza makamanda wa Polisi wakipanga mikakati..!
Mabomu yapigwa, viongozi wapigwa mawe, chupa
Katika kile ambacho kinaelezwa mara kwa mara kuwa fujo zinasababishwa na Polisi dhidi ya raia wema, kimejidhihirisha leo majira ya saa tano asubuhi Mei 5, baada ya Polisi kuamua kwa makusudi kutumia nguvu ambazo hazikuwa za lazima katika kuwanyamazisha madereva na wapiga debe waliokuwa wamejitokeza katika eneo ambalo Maofisa wa Polisi, Mkuu wa Wilaya Makonda, viongozi wa wamiliki wa mabasi,madereva na wandishi wa habari, ambapo askari waliokuwa na mbwa pamoja na mabomu ya machozi waliweza kufyatua hovyo mabomu hayo na kupiga risasi za moto juu ilikutawanya watu hao.
Baada ya mabomu haayo kupigwa, viongozi hao na Makamanda waliamua kulala chini huku wamekumbatiana , yaani ni tukio ambalo limeingia katika karne kwani ‘ukomavu’ au ‘ubwanyenye’ wa viongozi wetu ulionekana katika tukio hili ambalo viongozi hao wote walilala chini sehemu moja wakiwa wameshikana huku juu maabomu yakipigwa na mawe yakirushwa kwa kupigwa wao.
Ni tukio la la dakika 10 hadi 15, watu wanne, walijeruhiwa vibaya kwa kupigwa mawe na chupa zilizokuwa zikirushwa na watu hao.
Miongoni wa watu hao ni madereva ambao mmoja wapo alipasuliwa katika paji la uso na mwingine kichwani pamoja na kijana mmoja mdogo alijeruhiwa baada ya mbwa kumng’ata.. HILIKUWA NI PATASHIKA YA AINA YAKE KWANI BAADA YA HAPO KILA MMOJA ALIOMBA MAJI YA KUNAWA MACHO SI MKUU WA WILAYA AMA KAMANDA WA POLISI WOTE WALIPATWA NA TAFRANI HIYO.
viongozi hao wakielekea eneo ambalo wangezungumzia muafaka wao huo..!
Mkutano ukiendelea…kabla ya mabomu na kutupiwa mawe hayajaanza..!!
….Mabomu na kutupiwa mawe yalipoanza. viongozi hao wakakumbuka ‘depo’ na kulala chini si kamanda wa Polisi Wambura wa Kinondoni wala, Kamanda Mpinga, ama DC Makonda, wote walilala chini kujinusuru na hali ya usalama. Tutakuletea video ya tukio!!
Viongozi wakiomba maji ya kunawa usoni…!! hali ilikuwa tete huu ndio umuhimu wa kupitia depo unapohitajika kwa viongozi wengi..!
Hapa waliamua bora watoke eneo hilo kwani si salama.. tena!!
Mbowe wa Chadema awasili na kushangiliwa na umati mkubwa wa madereva
Umati mkubwa ulikusanyika na kumshangilia Mbunge wa Hai, na Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe aliyetinga katika ofisi hizo za madereva na kuungana na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya Makonda na makamanda wa Polisi wa Kinondoni, usalama barabarani na viongozi wa madereva.
Baada ya muda kadhaa kupita, wakiwa ndani ya ofisi hizo, wote kwa pamoja walifikiana hatua ya kukubaliana na kisha wakatoka nje majira ya saa sita kasoro ambapo walielekea katika eneo maalum na viongozi wa madereva walitoa maneno kadhaa akiwemo Rashid Salehe na baadae BONGE, ambaapo baada ya haapo DC Makonda aliamua kuchukua ‘kesi’ hiyo huku akiwaambia kuwa yeye ni bingwa wa migomo hivyo suala hilo kufika kwake ni sawa na kwenda kwa mwenye nalo hivyo wampe siku 7 tu, watamaliza matatizo yote huku akiwataka waache mgomo huo na waendelee na majukumu yao ambapo endapo pia mambo ya msingi ikiwemo suala la wajumbe wa kamati ya kushughulikia madai yao hakutakuwa na mtu muhimu wa madereva na wanayemuamini wao, basi amewaomba warejee katika mgomo huo tena yaani siku ya Mei 6, saa nne asubuhu.
Mbowe ashangiliwa kila kona!! Washangilia: Rais Rais Rais
Mbowe akiwa anatoka baada ya kuisha kwa mgomo wa madereva..! huku watu mbalimbali wakimshangilia na kuimba Rais Rais Rais vijana na pamoja na abiria waliokuwa ndani ya mabasi.!!
Mbowe akiingia kwenye gari lake ..!
Wakilisukuma gari lake hilo hadi jirani na hotel ya Blue Peal Ubungo.. na baadae msafara wa Chadema uliofika Ubungo ulipoondoka ..!
Abiria wakiwa na nyuso zilizokosa matumaini huku wasijue ni muda gani wataondoka, hii ilikuwa majira ya saa tatu asubuhi..!
Mmoja wa madereva akiwa ameshikiliwa baada ya kutokea purukushani na mabomu kupigwa hovyo..!
Mwandishi Mwandamizi wa mtandao huu, Andrew Chale ‘aki-Selfie’ katika aneo la tukio.. ambapo aliweka kambi ndani ya kituo hicho cha Ubungo na kukusanyia matukio haya ya mgomo huu uliodumu zaidi ya masaa 31, ambao ni mkubwa na haujawahi kutokea baadala ya ule wa Aprili 10 mwaka huu ambao wenyewe ulidumu kwa masaa 9 tu. SASA TUSUBIRI siku saba zilizoahidiwa na Mkuu wa Wilaya Paul Makonda kama alivyoahidi na utekelezaji wa kushughulikia mgogoro huo. Asante na Asante wewe msomaji wetu unayeperuzi mtandao huu mara kwa mara, Pia pongezi ziende kampuni ya tecno kupitia kifaa chao: Pad aina ya P9, tecno ndio iliyowezesha kukupigia picha hizi nzuri na za kukuvutia.
…Msomaji wetu na haya ndio tuliowakusanyia yote yaliyoajiri katika mgomo wa madereva uliodumu zaidi ya masaa 31. Modewji blog tunakupa kile kilicho bora kila siku kila saa, endelea kuperuzi nasi pia tushirikishe kama una habari na taarifa kupitia 0719076376 au Whatsapp 0767076376.