Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Rais Kikwete akutana na Rais mstaafu wa Marekani Bill Clinton jijini Dar

$
0
0

c1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kisha kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam jana April 28, 2015. Rais huyo wa 42 wa Marekani yuko nchini  kukagua miradi ya maendeleo na afya inayofadhiliwa na taasisi za Clinton Development Initiative (CDI) na Clinton Health Access Initiative (CHAI).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumanne, Aprili 28, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa 42 wa Marekani, Mheshimiwa Bill Clinton ambaye anafanya ziara nchini.

Baada ya mazungumzo hayo, viongozi hao walipata chakula cha mchana cha pamoja kabla ya kiongozi huyo wa Marekani kuondoka Ikulu, Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wawili walizungumzia baadhi ya miradi ambayo inadhaminiwa na kugharimiwa na Taasisi ya Clinton Foundation katika nyanja ya afya na hasa katika maeneo ya utoaji wa dawa za kurefusha maisha kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi, afya za akina mama na jinsi ya kupunguza vifo vya watoto wadogo chini ya miaka mitano na jitihada za kupambana na malaria, Nyanja ya kilimo hasa uzalishaji wa mbegu kwa wingi na kilimo cha soya.

c3

c4

 

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles