Na Andrew Chale wa Modewji Blog
Chama cha Wazalendo ACT-Tanzania kinatarajia kufanya mkutano wake Mkoani Ruvuma, Ijumaa ya Aprili 10, katika eneo la Songea Mjini.
Kwa mujibu wa taarifa kupitia kurasa ya twitter ya chama hicho kilieleza kuwa, viongozi wakuu wa chamaa hicho wanatarajiwa kuwa wazungumzaji wakuu huku Mwanachama mwenye mvuto kwa vijana ambaye pia ni msanii Afande Sele kutoka Morogoro naye akitarajiwa kuwapo kwenye mkutano huo na viongozi wa Kitaifa.
Aidha, chama hicho katika kujiimalisha, kimeendelea kuwataka wananchi wazalendo kuwaunga mkono ikiwemo kujiunga na huduma ya kupata muito wa simu wa chama hicho: Wimbo wa ACT Wazalendo kuwa muito wa simu yako, Kwa mtandao wa Vodacom, Tuma sms “ACT” kwa namba 15577.