Na Andrew Chale wa Modewji blog
Ni kama ndoto lakini mwishowe inakuwa si ndoto bali ni tukio halisi baada ya awali kuzagaa kwa picha tofautio 9, za Harusi ya Mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Nchini, Dk. Reginald Mengi akiwa katika harusi na Jacqueline Ntuyabaliwe, huko fukwe za visiwa vya hadhi ya juu Nchini Mauritius.
Mtandao wa Bongo5.com umekuwa wa kwanza kurusha picha hizo (Exclusive) huku wakiweka ‘brand’ yao kwenye picha hizo ambapo walibandika picha 9 kutoka kwenye harusi hiyo, iliyosemekana imefungwa mwisho wa mwezi March 2015.
Picha hizo zilinaonyesha pia watoto wao wawili mapacha kama wanavyoonekana kwenye picha pamoja na marafiki wengine wa familia pamoja na ndugu ambao idadi yao inafikia 50.
Ndoa imefungwa miezi minne baada ya Reginald Mengi kumchumbia Jacky, Nchini Dubai kwenye siku ya kuzaliwa ya mrembo huyu December 2014. (Tazama picho hizo).
watoto wao ambao ni mapacha wakimkaribisha mama yao