Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Shirika la HAPA lamtunukia tuzo mwandishi wa modewjiblog Singida

$
0
0

DSC04814

Mwandishi wa habari wa modewjiblog Singida, Nathaniel Limu, akiwa na tuzo aliyokabidhiwa na shirika lisilo la kiserikali la HAPA kwa mchango wake wa kushiriki utekelezaji wa mradi wa ushiriki sawa kwa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na ujinsia.

Na Nathaniel Limu, Singida

MENEJA wa shirika lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Associations (HAPA) David Mkanje, amewapongeza waandishi wa habari mkoani hapa kwa kushiriki kikamilifu utekelezaji wa mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na ujinsia (TMEP), na kitendo hicho kimechangia mradi huo kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Mkanje alitoa pongezi hizo wakati akizungumza kwenye kikao cha hitimisho la mradi wa TMEP kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa la Roman Katoliki mjini hapa.

Alisema waandishi wa habari ni sehemu ya mafanikio makubwa ya mradi wa TMEP ambao umetekelezwa na shirika la HAPA kwa kipindi cha miaka minne.

Akifafanunua ,Meneja huyo alisema waandishi wa habari wametumia kalamu na kamera zao vizuri katika kuwaelimisha na kuwahamasisha wanaume kuwa chachu ya mabadiliko katika masuala ya afya ya uzazi na ujinsia, na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Akiijengea nguvu hoja yake hiyo, Mkanje alisema mafanikio hayo ya kujivunia,ni pamoja na wanaume wengi sasa wanawasindikiza wenza wao kliniki na sio hivyo tu,wanaume wenyewe wameishatambua umuhimu wa kwenda kliniki kupima na kupata ushauri juu ya afya zao za uzazi.

“Mafanikio hayo yameenda mbali zaidi ambapo kwa sasa wanaume wengi wanashiriki kikamilifu majukumu yote ya kijinsia (yasiyo ya kibailojia) ambayo ni pamoja na kupika, kufua, kufanya usafi wa nyumba, kupeleka watoto kliniki wakati wenza wao wana majukumu mengine, kutafuta kuni, kufua nguo, kuchota maji na kushiriki vizuri shughuli za kilimo”,alisema Mkanje na kuongeza kwa kusema;

“Kabla ya kuanzishwa kwa mradi huo wa TMEP,majukumu yote hayo na mengine,yalikuwa yameelekezwa kwa wanawake pekee bila kujali afya ya mwanamke husika.

Lakini sasa hivi wanaume wanashiriki kikamilifu kutekeleza majukumu hayo kitendo hicho kimechangia kuongezeka kwa mahusiano mazuri na kuimarisha  upendo baina ya wanandoa.Mabadiliko hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na waandishi wa habari”.

Kwa upande wake Meneja wa mradi na mwezeshaji wa mafunzo TMEP makao makuu Dar-es-salaam,Cuthbert Maendaenda,amewahimiza waandishi wa habari na wadau mbalimbali kutoa elimu bila kuchoka juu ya afya ya uzazi na ujinsia na hasa kwa wanaume,ili mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla,iwe na jamii yenye afya bora wakati wote.

Katika hafla hiyo ya hitimisho la mradi huo ambao kwa Tanzania umetekelezwa katika mkoa wa Singida na Rukwa,waandishi wa habari Leonard Manga, Emmanuel Michael, Nathaniel Limu na Phesto Sanga wa TBC TV, Star TV, Modewjiblog na Radio standard. walitunikiwa tuzo na vyeti kwa mchango wao uliotukuka.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles