Na Andrew Chale wa Modewji blog
Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) tawi la Mwanza mapema Machi 25 mwaka huu imeendesha warsha ya wadau mbalimbali kuhusiana na Madhara ya Pombe kwa vijana kufuatia utafiti uliofanywa katika maeneo kadhaa ya Tanzania, ikiwemo Mkoa wa Kilimanjaro.
Warsha hiyo iliwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo Madaktari, wakuu wa idara za Polisi barabarani, wakuu wa Taasisi za Afya na mashirika ya kupiga vita matumizi ya vileo na wengineo.
Aidha kwa upande wake Dk. Said Kapiga kutoka NIMR Mwanza aliyetoa mada kwenye warsha hiyo, alisema licha ya wadau kupambana, bado changamoto nyingi zinaikabili Nchi.
“Pombe inasababisha mambo mbalimbali ikiwemo magonjwa mengi zaidi pamoja na hali ya utegemezi kwa jamii” alieleza Dk. Kapiga.
Dk. Ally Kapiga wa NIMR Mwanza akiongea na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia mkutano huo wa wadau kuhusu madhara ya pombe kwa vijana.
Pombe inasababisha kuenea kwa kasi pia ongezeko la magonjwa ya Ukimwi kwani, mtu anapolewa na kisha kujiingiza kwenye vitendo vya ngono ni rahisi kumpelekea vitendo vya kufanya tendo la ngono zembe.
Kwa upande wake, Dk. Ali Mzige alibainisha kuwa pombe pekee ina magonjwa mengi ikiwemo kansa na hata suala kukosa kizazi.
Katika hali nyingine, wadau hao walieleza kuwa, hadi sasa Serikali imeshindwa kushughulikia suala hilo matumizi ya Pombe ikiwemo kushindwa kushughulikia sera thabiti za kupunguza matumizi ya pombe na tumbaku.
Kwa upande wake, baadhi ya wadau hao walienda mbali kwa kueleza kuwa, kwa sasa pombe za viroba ambazo zinapatikana kwa bei rahisi ni hatari kwani zimebainika kutengenezwa kwenye mazingira hatari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama, mtoto na vijana (AMM), Dk. Ali Mzige akitoa mada kwa wadau (hawapo pichani).
“Kwa sasa pombe hizi za viroba kuna maeneo huko Temeke imekutwa mitambo wakizitengeneza kwa kutumia dawa za kupuguza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV) na pia viroba vingine wanatengenezea kemikali za fomaling’.
Kwa upande wake, Mtaalamu wa NIMR Mwanza, Joel Francis alibainisha kuwa katika utafiti wao waliofanya maeneo kadhaa ikiwemo Mkoa wa Kilimanjaro, imebainika kuwa vijana wengi Mkoa huo wanatumia pombe.
Kwa upande wake, Dk. Ali Mzige alibainisha kuwa, pombe zinazokaa kwenye paketi za ‘viroba’ humchukua mtu kulewa ndani ya dakika 6 hivyo pombe hizo ni hatari kwani zinaweza kukusababishia matatizo mengi ikiwemo ya kiafya.
Dk. Laetitia Sayi (Mtafiti binafsi-Freelance consultant) akijitambulisha kwenye mkutani huo wa wadau.
Dk. Macca .A. Balwa kutoka Taasisi ya GIYEDOO inayopambana na masuala ya kupinga matumizi ya Pombe.
Dk. Ali Mzige akiendelea na mada.
Dk. Praxeda Swai kutoka Muhimbili akijitambulisha kwenye mkutano huo.
Dk. Mariam Kalomo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (MoHSW).
Dk. Said Kapiga kutoka NIMR Mwanza, akijitambulisha kwenye mkutano huo wa wadau dhidi ya kupambana na Pombe kwa vijana mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelelea.
Erick Moshi ambaye ni Afisa Mtawala wa Tanzania Public Health Asosiation (TPHA) akijitambulisha kwenye mkutani huo.
Florence .K. Francis kutoka taasisi ya (F.I.T) DSM.
Haika Osaki wa NIMR Mwanza akiwasilisha mada kwa wadau (hawapo pichani).
Insp. Mossi .B. Ndozero kutoka makao makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini (TRAFFIC-HQ DSM).
Joel Msafiri wa NIMR Mwanza akitoa mada kwenye mkutano huo wa wadau.
Mathias Herman mwakilishi kutoka UNESCO akijitambulisha kwenye mkutano huo wa wadau (kushoto).
Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki (kushoto) akijitambulisha kwenye mkutano huo wa wadau.
Mwandishi wa habari wa blog ya Jamii ya kutoka Michuzi Media Group kupitia blog ya Michuzi, Chalila Chibuda akijitambulisha kwenye mkutano huo wa wadau.
Stafu wa NIMR tawi la Mwanza Haika Osaki akijitambulisha kwenye mkutano huo.