Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Taswira ya Bonanza la wafanyakazi wa kiwanda cha Tumbaku mkoani Morogoro

$
0
0
 Wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco Co. Ltd. (TLTC) na Tanzania Tobacco Processing Company TTPL wakishindana kunywa soda na kula mkate wakati wa bonanza la siku ya familia iliyofanyika Morogoro.
Wafanyakazi wa kike wa kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco Co. Ltd. (TLTC) na Tanzania Tobacco Processing Company TTPL wakishindana kuvuta kamba wakati wa bonanza la siku ya familia liliyofanyika wiki iliyopita katika viwanja vya Magadu.
 Wafanyakazi  wa kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco Co. Ltd. (TLTC) na Tanzania Tobacco Procesing Company TTPL wakishindana kukuna nazi wakazi wa bananza la siku ya familia ya kampmuni hizo yaliyofanyika wiki iliyopita katika viwanja vya magadu Manispaa ya Morogoro.  Manispaa ya Morogoro.

Mkurugenzi wa sheria na mahusiano wa kampuni hizo Richard Sinamtwa akiwasalimia watoto wa wafanyakazi wakati wa bonanza la siku ya familia lililofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya magadu manispaa ya Morogoro. (Picha na Hamida Shariff, Morogoro).

Na Mwandishi wetu, Morogoro.

Wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco Co. Ltd. na Tanzania Tobacco Processing TTPL wametakiwa kudumisha michezo mbalimbali baada ya saa za kazi ili kujenga mahusiano mema baina yao pamoja na kuwa na afya bora.

Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkurugenzi wa Sheria na mahusiano wa kampuni hizo Richard Sinamtwa wakati akifungua bonanza la siku ya familia kwa wafanyakazi wa kampuni hizo lililofanyika katika viwanja vya Magadu, Maniaspaa ya Morogoro.

Sinamtwa alisema kwa kutambua michezo ni muhimu sehemu za kazi hivyo uongozi wa kampuni hizo uliamua kutenga siku ya maalumu kwa ajili ya bonanza la wafanyakazi.

Alisema kuwa bonanza hilo pia linashirikisha watoto wa wafanyakazi hao ambao nao wamekuwa wakicheza michezo mbalimbali na hivyo kufahamiana na kujenga urafiki.

Hata hivyo aliwataka wafanyakazi hao kudumisha suala la usalama kazini ili kuepuka na majanga na ajali zinazoweza kutokea kazini endapo suala la usalama kazini halitazingatiwa.

Pia aliwataka wafanyakazi kujituma, kudumisha uadilifu, uaminifu na kuongeza ufanisi wa kazi ili kampuni hizo ziweze kuongeza uzalishaji.

Naye Mwenyekiti wa Bonanza hilo Dkt. Mose Makawu alisema kuwa siku hiyo ya familia kampuni hizo zimekuwa zikitoa zawadi kwa wafanyazi bora na waliofanyakazi kwa muda mrefu na kwa uadilifu.

Dkt. Makawu alisema kuwa kampuni hizo pia zimekuwa zikitoa zawadi kwa watoto wa wafanyakazi walioshinda kwenye michezo mbalimbali.

Kwa upande wake mfanyakazi bora wa kampuni hiyo Mhina Katongo alisema kuwa siri kubwa ya yeye kuwa mfanyakazi bora ni kujituma na uadilifu hivyo aliwataka wafanyakazi wenzake kufanyakazi kwa kuzingatia maadili na pia kudumisha nidhamu ya kazi.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles