Na Andrew Chale wa Mo dewji blog
Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Tanzania Red Cross Society-TRCS), Dk. George Nangale (pichani), kwa habari zilizotufikia chumba cha Habari cha Mo dewji blog ni kuwa amejiuzulu nafasi yake hiyo.
Habari hizo zilibainisha kuwa, Dk. Nangale tayari amewasilisha barua rasmi ya kujiuzulu huku akikabidhi vitu muhimu ikiwemo funguo ya gari ambayo alikuwa akiitumia kama Rais ama Mwenyekiti wa Chama, katika makao makuu ya Red Cross, Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, mtandao huu ulipomtafuta Dk. Nangale kwa njia ya simu juu ya maamuzi hayo, mara zote namba yake ya kiganjani iliitabila kupokelewa.
Kwa upande wa viongozi wa juu ya Makao makuu ya Red Cross nao hawakuweza kupatikana kuelezea hilo huku taarifa zaidi zikieleza kuwa, Viongozi hao wa juu ikiwemo bodi ya chama walikuwa mjini Dodoma katika mkutano mkubwa ikiwemo kujadili jambo hilo la Rais, ambapo inaelezwa kuwa, pande zote mbili zilifungua kesi za kuzuia kila mmoja asijadili ama kutoa maamuzi dhidi ya mgogoro wao ndani yaa chama.
Aidha pia unaweza kusoma taarifa za awali ambazo Rais huyo aliwahi kusimamisha kesi hiyo Mahakama Kuu, soma hapa pia: http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/32947-mahakama-kuu-yasitisha-kikao-bodi-ya-red-cross
Msomaji wa Mo dewji blog, mtandao huu utaendelea kukujuza kila kinachoendelea kwa habari mbalimbali popote pale utapata taarifa bora.. Kujua zaidi juu ya hili endelea kuperuzi nasi.