Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Watanzania tupuuze habari za Uongo, uzushi, Ukipata ujumbe wa chuki, matusi au uongo, FUTA DELETE KABISA!

$
0
0

1005224_161118974079176_1902408761_n

Na Andrew Chale wa Mo dewji blog

Wasomaji wa Mo dewji blog mnaoendelea kuperuzi mtandao huu bila shaka ni wazima wa afya, tunashukuru uwepo wenu na kutembelea kwenu kwenye mtandao huu ndio faraja kwetu sote sie tunaowapasha habari na kwenu mnaopokea habari, tupo pamoja.

Tahariri ya leo Machi 10,  Tunazungumzia namna ya jinsi Tanzania tunavyopiga hatua moja hadi nyingine hasa katika masuala ya TEKOHAMA/ICT.. Hasa kupitia mitandao yaani Intaneti.

Hata hivyo licha ya kuwa huru kwa kila mmoja wetu kufanya afanyavyo, wapo watu wanautumia vibaya Uhuru huu wa ICT yaani wengi wanafanya fujo, kiasi kwamba wanajiona hawatafikiwa na mikono ya sheria?.

Miongoni mwa Habari ambazo mtandao huu iliziripoti jana Machi 9, ni tukio taarifa za uzushi, uongo ambazo zilikuwa zikisambazwa na watu juu ya kifo cha Mjane wa Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere unaweza kutembelea link hii pia kujisomea..: http://dewjiblog.com/2015/03/09/mama-maria-nyerere-ni-mzima-wa-afya-taarifa-za-kifo-zipuuzwe/

Jamani, ni jambo la aibu sana kwa mtu mwenye akili timamu ambaye anakaa na kisha kusambaza taarifa za uongo.

 Hakika maumivu ya moyo anayopata mtu anayesingiziwa ni makubwa sana, huu tunaweza kuita ni uuwaji wa fikra za binadamu mwenzako.

Miongoni mwa uongo ambao husambazwa kwa wingi maeneo mengi katika dunia ya sasa, ambayo Tanzania tunaweza kusema ni muumini wake ni suala la KIFO!. Wapo watanzania wengi wamekuwa mahodari wa ‘KUTANGAZA VIFO’. Utasikia ‘Fulani amefariki ghafla leo, au Sijui X amepata ajali na kufariki dunia, wakati huo anajua si kweli juu ya jambo hilo.

Au wengine wanaenda mbali zaidi, wanasambaza hababari za kifo cha mtu mkubwa/maarufu na kisha kusambaza taarifa hiyo kwenye mitandao ya kijamii, simu za mikononi kupitia meseji, whatsapp,  na njia nyinginezo.

Mo dewji blog, tunaungana na Mamlaka yaa Mawasiliano Tanzania ( Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA),  ( https://www.tcra.go.tz/)katika kampeni yao ya kupinga vitendo hivyo hasa za kusambaza habari za chuki, uongo, uzushi, uvumi na  taabia ya kusambaza picha zisizoendana na maadili  na utu wa Mtanzania.

Ujumbe wa bure, Itambulike kuwa, wale wote wanaosambaza habari, ujumbe, picha za chuki, uongo na uzushi zipo mamlaka husika zinawafuatilia kwa njia moja ama nyingine na ujue tu kuwa kila unachokifanya katika masuala haya ya TEKOHAMA/ICT, unaonekana.

SASA NI WAKATI WA KUSEMA BASI KABLA YA UJASHUKIWA NA KUCHUKULIWA HATUA KALI! ACHANA KABISA NA KUENEZA CHUKI, KAMA WEWE NI BLOGGER BASI WEKA  HABARI ZA KWELI NA KAMA HUNA UHAKIKA NAZO HABARI ZAKO ULIZA KWA BLOGGER WENZAKO WATAKUSAIDIA AMA OMBA USHAHURI…KAMA WEWE UNA AKAUNTI KATIKA MTANDAO WA KIJAMII JUA HAPO HAPO ULIPO UNAPOITUMIA HIYO AKAUNTI YAKO TAYARI UMESHAONEKANA NA MAMLAKA HUSIKA HIVYO CHOCHOTE UTAAKACHOKIFANYA WAO WANAKUONA, HIVYO NI BORA UKAWA MSTAARAABU NA KUFANYA MAMBO YAKO KWA FARAGHA BILA KUINGILIA UHURU/UTU WA MWINGINE.

Mo dewji blog tunaungana na TCRA  na kusema kuwa: “ #Ukipata ujumbe wa chuki, matusi au uongo, FUTA DELETE KABISA!


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles