Mpaka sasa nilikuwa kimya siamini, hivi kweli Kapteni JOHN KOMBA umekwenda?! Siku yangu ilikuwa ngumu sana nilipoambiwa ingia studio BREAKING NEWS, Mbunge wa Mbinga Magharibi na kada wa CCM Kapteni John Komba amefariki dunia, ulikuwa wakati mgumu sana kwangu na hata saa mbili niliposoma taarifa hiyo kwa mara ya PILI, ilizidi kunipa wakati mgumu. Unaweza kufuru kwanini kipindi hiki Mungu ndo umeamua kumchukua Kapteni KOMBA lakini Mungu wetu ni mwema na kazi yake haitiwi kasoro wala kuuliza kwanini. Nenda babaangu/mtani wangu/kiongozi wangu. Uliyoniasa siku chache zilizopita nitayafanyia kazi ili hata huko mbinguni utakapokuwapo ufurahi, msalimie babaangu Mzee H.Kingalame na wote waliotangulia mbele za haki. I WILL MISS U!
Huo ndio ujumbe wa Grace Kihampa kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Facebook.