Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mama Salma Kikwete awataka wanaume kuwaunga mkono wake zao kupima saratani za matiti na shingo ya kizazi

$
0
0

mam10

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akikabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwa uongozi kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kulia). Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye Hospitani Kuu ya Jeshi Lugalo kwenye Kitengo cha Uzazi na Mtoto kilichoko Mwenge tarehe 27.2.2015. Aliyesimama pembeni kwa Mama Salma ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando na aliyesimama kulia kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ni Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugal Brigedia Jenerali Josia Mwita Makere.

mam9

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Ndomba akimpongeza Mama Salma Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa kwenye hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwenye hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo tarehe 27.2.2015.

mam81

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ta matiti kwa akina mama kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo. Hafala hiyo ilifanyika kwenye Kitengo cha Uzazi na mtoto cha hospitali hiyo kilichoko eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015.

mam41

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Ndomba akitoa hotuba wakati wa hafla ya kukabidhi mashine ya kupima saratani ya matiti kwa akina mama katika Hospitali ya Lugalo tarehe 27.5.2015.

Na Anna Nkinda – Maelezo

Wanaume nchini wametakiwa kuwaunga mkono wake zao kupima saratani za matiti na shingo ya kizazi na pale watakapokutwa na maradhi hayo wasiwanyanyapae bali wawafariji kwani magonjwa hayo yanatibika kama yatagundulika mapema.

Rai hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mashine ya kisasa ya upimaji wa saratani ya matiti (Mammography) katika Hospitali kuu ya Jeshi la  Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, kliniki ya Mama na Mtoto iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema unyanyapaa wa wanaume huwakwaza wanawake na kuwafanya baadhi yao kusita kujitokeza kupima na kupata tiba dhidi ya saratani.

“Nanyi wanawake msisubiri mpaka msikie maumivu ndipo mkapime maana wakati huo saratani itakuwa imeenea, jengeni tabia ya kupima saratani za matiti na shingo ya kizazi mara kwa mara wataalamu wanasema unapima  mara moja kila baada ya miaka mitatu”.

Bahati nzuri saratani ya shingo ya kizazi ina kinga kwa njia ya chanjo hivyo basi wazazi tuchangamkie kuwapeleka watoto wetu wa kike kupata chanjo hiyo, tutawapatia kinga ya kudumu ya maradhi haya hatari”, alisisitiza Mama Kikwete.

Alisema ugonjwa wa saratani ya matiti unaathiri wanawake wengi nchini na wataalam wa afya wanasema  saratani ya matiti ni ya pili kwa ukubwa nchini ikifuatiwa na  ya shingo ya kizazi.

Mama Kikwete alisema, “Niliamua kukabidhi mashine hii katika Hospitali hii baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wanatibiwa hapa pia huduma ya mama na mtoto hutolewa hapa.Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo ni Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mashariki hivyo inastahili kuwa na mashine ya aina hii ambayo itawanufaisha wanawake wengi wanaokuja hapa kuhudumiwa”.

Kwa upande wa saratani ya tezi dume aliwahimiza wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 45 wajitokeze kupima kwani ikigundulika  mapema inatibika.

Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema, “Wanawake nasi tunao wajibu wa kuwahamasisha  waume zetu kupima saratani ya tezi dume na kuwafariji wakiwa wakiwa kwenye tiba. Tushirikiane kwa pamoja kuleta mabadiliko”.

Naye  Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Samuel Ndomba  alimpongeza Mama Kikwete kwa kazi anayoifanya ya kuiongoza Taasisi ya WAMA yenye lengo la kuinua ustawi wa watoto na akina mama hususani katika nyanja za afya, elimu na huduma za maji safi na salama.

Alisema, “Juhudi kubwa unazozionyesha za kuboresha na kuendeleza huduma za afya ya mama na mtoto zinadhihirisha upendo wa dhati ulionao kwa umma wa watanzania”.

Luteni Jenerali Ndomba  alisema tukio hilo la kukabidhiwa mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa Jeshi hilo ni la kihistoria na la kipekee na kumshukuru Mama Kikwete kwa kutambua umuhimu, kujali na kuthamini afya za wanajeshi, familia zao na akina mama wote.

“Ni dhahiri kuwa ulinzi imara wa taifa letu unategemea wanajeshi na wananchi wenye afya nzuri. Tunakuhakikishia kuwa mashine hii haitatumika kwa wanajeshi na familia zao tu bali itatumika kutoa huduma kwa wananchi wa Tanzania kwa kufuata kanuni na taratibu za huduma ya tiba Jeshini”, alisema Luteni Jenerali Ndomba .

Alimalizia kwa kusema Jeshi hilo litaweka kipaumbele katika mafunzo kwa wataalam ambao wataweza kuitumia na kuitunza vizuri mashine hiyo ili utoaji wa huduma kwa akina mama uwe endelevu.

Mashine hiyo imetolewa na kikundi cha wanawake wajasiriamali wa Tanzania waishio nchini Washington, nchini Marekani cha Wanawake watano (Tano Ladies) kwa kushirikiana na  Chama cha Wanawake wa Afrika na Uelewa wa Saratani (African Women Cancer Awareness Assossiation – AWCAA).

Wanawake hao walimkabidhi Mama Kikwete mashine hiyo ya kupimia saratani ya matiti mwishoni mwa mwaka jana alipokuwa nchini Marekani katika shughuli za kikazi  ili iweze kusaidia na  kuokoa maisha ya wanawake hapa nchini.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles