Na Mwandishi wetu wa modewjiblog, Dodoma
Habari zilizotufikia kutoka Mkoani Dodoma: Basi la Kidia One Express lagongana na lori na kudaiwa kusababisha vifo vya watu wawili huku likijeruhi abiria kadhaa. Taarifa hiyo ilieleza kuwa ajali hiyo iliyotokea leo majira ya saa Saba mchana.
Taarifa kutoka chanzo cha ajali hizo zilieleza kuwa, ajali hiyo imetokea maeneo ya Mbande, njia ya kuelekea Dodoma kutoka Morogoro, ambapo basi la abiria la Kidia Express, limegongana na lori.
Imeelezwa kuwa, basi hilo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza. Hata hivyo mtandao huu bado unaendelea na juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO).