Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Balozi Iddi afungua rasmi mkutano wa kikanda juu ya ukuaji wa miji ya Afrika Mashariki

$
0
0

1

Afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) Prof. Joseph Semboja, (Kulia) akimkaribisha Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mh. Balozi Seif Ali Iddi, (kushoto) kufungua rasmi Mkutano wa kikanda uliokutanisha viongozi na watunga sera kutoka nchi za Afrika mashariki, kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika mpaka ifikapo 2050, katikati ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick. Mkutano huo wa siku mbili umefanyika katika hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel ya jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi SeIf Ali Iddi amefungua rasmi mkutano wa kikanda juu ya ukuaji na maisha ya baadae ya miji ya Afrika mashariki ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) ulioanza leo katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es salaam.  

Mkutano huo uliopewa jina la ‘Maisha ya baadae ya nchi za Afrika Mashariki: Jinsi gani tunataka kuishi mwaka 2050?’ umewakutanisha viongozi wa serikali akiwemo Mheshimiwa Hawa Ghasia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Didas Masaburi Meya wa jiji la Dar es salaam na watunga sera kutoka nchi  za Afrika mashariki kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadaye ya miji ya Afrika.

2

Afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) Prof. Joseph Semboja, (Kulia) akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mh, Balozi Seif Ali Iddi, wa tatu toka kulia,  kufungua rasmi mkutano wa kikanda uliokutanisha Viongozi na watunga Sera kutoka Nchi za Afrika mashariki , uliozungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika mpaka ifikapo 2050, Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick, na wa Pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia , mkutano huo wa siku mbili umefanyika leo katika hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo, mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais kutoka Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi- aliishukuru Taasisi ya UONGOZI kwa kumualika na kutumia pia fursa hiyo kuwakaribisha wageni wote kutoka nje jijini Dar es salaam huku akilitambua kama moja ya majiji yanayokua kwa kasi zaidi barani Afrika.

“Ukuaji wa miji ni jambo ambalo halikwepeki na ni kitu muhimu duniani kote na sio Tanzania tu,” alisema Balozi Iddi.

Aliongeza, “Majiji na miji ni sehemu muhimu zenye fursa kiuchumi, teknolojia na ubadilishanaji wa mawazo na uzoefu katika nyanja mbalimbali… Tanzania imepiga hatua katika ukuaji wa miji na serikali kuu imekuwa mstari wa mbele katika kufanya kazi na serikali za mitaa ili kuweza kurekebisha makazi mbalimbali yasiyokuwa kwenye mpangilio.”

3

Afisa mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute)“Uongozi Instutite”, Prof. Joseph Semboja, kushoto, akiongea na Viongozi na watunga Sera kutoka Nchi za Afrika Mashariki katika Mkutano unaozungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika  ifikapo 2050. Mkutano huo umefanyika katika hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro ya jijini Dar es Salaam.

“Nina imani kubwa na wajumbe kutoka Afrika Mashariki pamoja na wengine waliokusanyika hapa kutoka nchi mbali mbali duniani. Hakika hii ni fursa ya kipekee ya kuangalia ni kwa namna gani tunaweza tukaboresha miji na majiji yetu barani Afrika ili kuweza kufaidisha wananchi wetu wa ukanda huu wa Afrika Mashariki,” alisema Balozi Iddi.

 Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute, Prof. Joseph Semboja alisema ya kwamba  mkutano huo unalenga kuangalia na kujadili changamoto na fursa mbalimbali zinazoletwa na ukuaji wa miji Afrika Mashariki na jinsi gani viongozi wa Afrika wanaweza kukabiliana nazo kwa pamoja.

“Mambo tutakayozungumza kwenye mkutano huu sio mapya kwenye masikio ya wengi, ni mambo muhimu ambayo yanahusisha nchi zote za ukanda wa Afrika na dunia kwa ujumla,” alisema Prof. Semboja.

4

Afisa mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa maendeleo Endelevu “Uongozi Instutite”, Prof.Joseph Semboja, wa kwanza kushoto, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia, wa Pili toka kushoto na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mh.Balozi Seif Ali Iddi wakimfuatilia mtoa mada hayupo Pichani wakati wa Mkutano wa kikanda uliokutanisha Viongozi na watunga Sera kutoka Nchi nza Afrika mashariki , uliozungumzia changamoto za  ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika ifikapo 2050, mkutano huo wa siku mbili umefanyika leo katika Hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam.

“Kuna uwiano mkubwa wa ongezeko la watu Afrika (na duniani kwa ujumla) wanaoishi mijini na kupelekea msongamano na shinikizo la nyumba, ajira na huduma za kijamii. Ni kwa matokeo haya jukwaa hili limelenga kujadili namna ya kutatua changamoto hizo na kufikiria miji ambayo itatimiza matakwa yetu,” aliongeza Prof. Semboja.

Kwa mujibu wa chapisho la UN-Habitat ‘Hali ya miji ya Afrika 2014’ , “Afrika Mashariki inashika nafasi ya chini katika miji inayokua duniani lakini ndiyo kanda inayoongoza katika kasi ya ukuaji wa miji yake hivi sasa.  Ifikapo mwishoni mwa muongo huu wa sasa idadi ya wakazi waishio mijini itaongezeka kwa asilimia 50 na jumla ya idadi ya wakazi wa mijini ifikapo mwaka 2040 inatarajiwa kuwa mara tano ya 2010.

Washiriki wa kongamano hilo wametoka nchi mbalimbali ikiwemo Burundi, Ethiopia, South Afrika, Sudan, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan ya Kusini, Tanzania na  Uganda.

5

Mkurugenzi wa Mistra Urban Futures Prof ,David Simon, akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kikanda uliokutanisha Viongozi na watunga Sera kutoka Nchi za Afrika mashariki , kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika ifikapo 2050. Mkutano huo wa siku mbili umefanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

6

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mh, Balozi Seif Ali Iddi, (kushoto) akimsikiliza Gavana wa Khartoum Sudan, AbdelRahman Alkhidir, wakati wa mkutano wa kikanda uliokutanisha Viongozi na watunga Sera kutoka Nchi za Afrika mashariki , kuzungumzia changamoto za  ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika ifikapo 2050, mkutano huo umefanyika katika Hotel ya  Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

7

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (kulia) akifafanua jambo kwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mh, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) wakati wa mkutano wa kikanda uliokutanisha Viongozi na watunga Sera kutoka Nchi nza Afrika mashariki , kuzungumzia changamoto za  ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika ifikapo 2050. Katikati ni Gavana wa Khartoum Sudan, AbdelRahman Alkhidir. Mkutano huo umefanyika katika Hotel ya Hyatt Regency  jijini Dar es Salaam.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles