Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Panya road watikisa jiji la Dar

$
0
0

6955917312_d80d4a80e6_b

Kundi linalozaniwa ni la kihalifu maafuru kama “Panya Road” usiku wa leo wametoa hofu kubwa kwa wakazi wa Dar yakiwemo maeneo ya Tandale, Manzese, Magomeni, Mabibo na mengineyo.

Kundi hilo limezua hofu na kusababisha maduka kufungwa mapema huku watu wakikimbia ovyo kwa hofu na shughuli zote kwenye baadhi ya maeneo ya jiji kusimama mpaka pale hali itakapotengemaa.

Imebainika baadhi ya maeneo ni Magomeni, Tabata, Kinondoni na kwingineko kundi hilo limepita na kufanya uhalifu kwa kupora watembea kwa miguu,  madukani na kukaba.

Sekeseke hilo limeanza jioni hii baada ya kundi hilo kutoka makaburini kumzika mmoja wa kundi hilo aliyeuawa na polisi, ndipo walipoamua kulipiza kisasi kwa kufanya fujo hizo za kuvamia, kupora na kuharibu mali za watu kwenye baadhi ya maeneo tajwa hapo juu.

Modewjiblog inaendelea kufuatilia kwa ukaribu zaidi na tutaendelea kuwajuza kadri muda unavyokwenda.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles