Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akimwapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad, leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad akisaini hati ya kiapo chake mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akisaini hati ya kiapo cha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad mara baada ya kumwapisha leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman wakati wa hafla fupi ya kuapishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam, Kulia ni Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mh. Zitto Kabwe akisalimiana na Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad(wa pili kutoka kushoto) na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akizungumza jambo la baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali mara baada ya kuapishwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Ikulu jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano uliopo kati ya Ofisi yake kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika kujenga Mfumo wa kisasa wa ukaguzi wenye uwajibikaji unaojenga nidhamu katika mapato na matumizi ya Serikali.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad akiongea na waandishi wa habari kuhusu namna atakavyotekeleza majukumu yote yaliyoainishwa katika ofisi yake kwa mujibu wa sheria.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Juma Assad (aliyeshika maua) akipongezwa na ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kuapishwa leo. Kulia ni aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali aliyestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria Bw. Ludovick Utouh.(Picha na Aron Msigwa –MAELEZO).









