Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mwanamke mmoja nchini Ufaransa atangaza kuwa tayari kutoa huduma ya kuwanyonyesha watoto wa wazazi wa jinsia moja.

$
0
0

breastfeeding_2636861b

Mwanamke amejitolea kunyonyesha watoto wa mashoga wa kiume kwa gharama ya Euro 100 kwa siku.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 amejielezea kuwa ni muuguzi aliyesomea katika tangazo lililotolewa kwenye mtandao wa Ufaransa.

Mwanamama huyo aliyejitangaza kuwa anakodisha maziwa yake kwa ajili ya kunyonyesha watoto wachanga, ameahidi kuwa anapatikana muda wowote na anaweza kwenda popote kutoa huduma hiyo, na kuahidi pia kunyonyesha mpaka mara 10 kwa siku na kuwa anaishi karibu na Paris.

Akizungumzia muitio wa watu baada ya tangazo hilo, amesema amepata oda nyingi lakini nusu ya waliomuandikia hawakuwa wakimaanisha.

Tangazo hilo limekuja ikiwa ni wiki chache zimepita tangu kupigwa kwa kura iliyokera wananchi na ya kihistoria iliyo halalisha ndoa za jinsia moja nchini Ufaransa.

Mabadiliko katika sheria yaliyoruhusu ndoa za jinsia moja yalifanyika mwezi Mei na kuifanya Ufaransa kuwa nchi ya 14 kuruhusu ndoa za mashoga.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles