Maelfu ya raia wa Tunisia wameandamana katika mji mkuu Tunis wakitaka kuondoka madarakani kwa serikali ya mpito katika maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu mzozo wa kisiasa kuanza wiki mbili zilizopita.
Maandamano hayo yanakuja wiki chache kabla ya bunge la mpito kukamilisha kazi ya kuandika rasimu ya katiba na sheria mpya ya uchaguzi.
Saa chache kabla ya maandamano hayo, spika wa bunge hilo la mpito Mustafa Ben Jaafar alisimamisha majukumu ya bunge hilo na kusema bunge hilo la muda halitaendelea na majukumu yake hadi serikali na wapinzani wake watakapofanya mazungumzo-DW.