Maafisa nchini Hispania wamemkamata mwanamume anayetuhumiwa kuwanajisi watoto 11 walio kati ya umri wa miaka 4 na 15 nchini Morocco.
Mtu huyo aliachiliwa hivi karibu baada ya kusamehewa na mfalme wa Morocco.
Daniel Galvan Vina (Pichani) anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama kuu nchini Hispania.
Vina alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 30 kabla ya mfalme Mohammed wa sita kumsamehe pamoja na wafungwa wengine 48 raia wa Hispania wiki iliyopita.
Taarifa za kuachiliwa kwake zilizua maandamano makubwa yaliyoambatana na ghasia nchini Morocco na kumlazimu mfalme huyo kubatilisha uamuzi wake.
Inadaiwa mfalme Mohammed hakufahamu ukubwa wa kosa alilofanya raia huyo mhispania wakati akitoa amri hiyo ya kumsamehe yeye pamoja na wenzake.