Picha juu na chini ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka ngao/sime katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera leo.
Picha juu na chini ni Viongozi wa dini wakisoma dua kwenye maadhimisho hayo. Pembeni ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Jaji Mkuu Mheshimiwa Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman Makungu.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana katika vita ya Iddi Amin Nduli ambao nao walijumuika kuwakumbuka mashujaa waliopoteza maisha katika vita hivyo.
Rais Jakaya Kikwete akitembelea makaburi ya mashujaa waliopoteza maisha wakati wa vita na Nduli Iddi Amini wa Uganda.(Picha na IKULU).