Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Ukosefu wa huduma za afya za kisasa na uhakika zadaiwa kuwa sababu kubwa ya watanzania kufuata huduma hiyo nje ya nchi

$
0
0

CEOsir PIC01

. Ukosefu wa huduma za afya za uhakika na za kisasa zinadaiwa  kuwa sababu kubwa ya watanzania  wengi kufuata huduma hizo nchi za nje.

Hospitali ya Apollo ilikuwa moja ya hospitali za mwanzo kabisa katika bara la Asia, na duniani kwa ujumla kuleta huduma zote za kiafya chini ya paa moja. Na kwa wakati huu, mpango huo kabambe umeifanya hospitali hiyo kufanikiwa katika Nyanja zote za matibabu.

Dr. Prathap C Reddy, muasisi wa huduma za kiafya za kisasa nchini india, alianzisha hospitali ya aina yake nchini humo mwaka 1983. Ikitoa huduma zote za kiafya, hospitali ya Apollo ina zaidi ya vitanda 8000 katika jumla ya hospitali zake zipatazo 50, na idadi ya maduka ya dawa baridi yapatayo 50, vituo vya afya vya uchunguzi wa kina, vituo vya bima za afya pamoja na uchunguzi wa kina wa seli mbalimbali kwa ajili ya utafiti. Hospitali ya Apollo ni hospitali bingwa duniani kwa upandikizi wa viungo mbalimbali vya binadamu duniani. 

Nchini Tanzania, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kama saratani,kisukari, na magonjwa yanahusiana na moyo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi. Magonjwa haya yamesababisha kupotea kwa nguvu kazi ya taifa na pia yanagharimu fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kuboresha shughuli nyingine za kiuchumi.

Hivi sasa, uwezo wa Tanzania kutibu magonjwa ya moyo, upasuaji wa moyo, saratani, na matatizo ya figo ni mdogo, na maelfu ya watanzania hufuata huduma hizi nje ya nchi kwa bei nafuu, hususani nchini India.

Ugonjwa wa moyo ni wa pili kwa kusababisha vifo vingi nchini Tanzania baada ya malaria, ukichangia vifo 287 kwa siku, au 104,755 kwa mwaka, kwa takwimu za taasisi ya moyo Tanzania. ‘Tanzania kwa sasa haina kituo  maalum cha kutoa matibabu ya jumla ya moyo. Asilimia 20 ya vifo vyote hutokana na ukosefu wa utaalamu, vifaa na umaskini, na wale wenye uwezo inawabidi kusafiri nje ya nchi,’ inaongeza taasisi hiyo

Katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita, safari ya hospitali ya Apollo imetengeneza historia ya kupendeza katika hali nzima ya utoaji wa huduma za kisasa za afya nchini India. Taasisi hiyo imeendelea kung’ara kati ya watoa huduma binafsi. Hospitali hii ilikuwa moja ya waanzilishi wa tuzo za juu za utoaji wa huduma ya kisasa duniani.

Hospitali ya Apollo ni moja ya hospitali zinazojulikana vyema miongoni mwa wa-Tanzania, kwani viongozi wengi maarufu, wafanyabiashara na mamia ya wagonjwa wenye uhitaji wa upasuaji wamekuwa wakisafiri na kupata matibabu kutoka hospitali hizi maarufu.

Hivi karibuni hospitali ya Apollo ilifanya upasuaji wa kuwatenganisaha mapacha kutoka Tanzania kwa mafanikio makubwa.

Nchi za India na Tanzania zimekua na ushirikiano mkubwa kihistoria, kiutamaduni, kisiasa na kibiashara, na uwepo wa  hospitali hizo nchini Tanzania utaendelea kudumisha uhusiano mwema kati ya nchi hizi mbili.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles