Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Wanne waangukiwa na mawe mazito Mwanza

$
0
0

mwanza

Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wakiwa wamekusanyika eneo la tukio.

Na Mwandishi wetu, Mwanza

Watu wane wamefriki dunia katika Jiji la Mwanza baada ya nyumba zao kuporomokewa na miamba ya mawe, akitaja waliofariki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola aliwataja waliofariki kuwa ni Emanuel Joseph na Kefa Joseph wanafunzi wa shule ya Msingi Mbugani, Kwinta Geko na Samson Odinya  ambao ni watu wazima

Kufuatia maporomoko hayo vilio vilitawala na watu wengi wa Jji la Mwanza kukusanyika  maeneo ya Sinai-Mabatini jijini Mwanza, kushuhudia miiili hiyo ya watu wanne wa familia mbili tofauti, vilivyotokana na familia  kuangukiwa na mawe mawili yaliyoporomoka usiku

Tukio hilo la kusikitisha linadaiwa kutokea saa 8:55 usiku wa kuamkia juzi, wakati mvua iliyoambatana na upepo wa wastani, na radi nyingi kunyesha, ambapo majabali makubwa ya m awe yanayokadiriwa kuwa na uzito wa kufikia tani mbili ilipoporomoka na kuziponda nyumba hizo kisha kusababisha vifo hivyo na majeruhi kadhaa.

Nyumba zilizofikwa na  maafa hayo zimetajwa kumilikiwa na Joseph William pamoja na nyingine inayomilikiwa na Lameck Jonson Ajiji, na kila nyumba watu wawili wamefariki kwa kukandamizwa na miamba hiyo na mmoja kujeruhiwa.

Aidha waliofarki katika nyumba ya Ajiji walitambuliwa kuwa ni mama wa mji huo, Kwinta Gwego na mumewe ambaye hajafahamika jina, ambapo mtoto Bety Ashirati (4) amenusurika kisha kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake.

Tukio hilo lilivuta  lilivuta hisia tofauti dhidi ya wananchi wakazi wa jiji  huku wengine wakiangua vilio vilivyojaa simanzi, na inadaiwa katika nyumba hizo mbili watu wawili akiwemo mtoto mdogo wa miaka minne wakinusurika kifo.

Mbunge wa Nyamagana jijini Mwanza, Ezekiel Wenje (CHADEMA), alifika eneo la tukio kisha kutoa pole kwa wananchi, ndugu jamaa na marafiki wa familia zilizoathirika na janga hilo, ambapo alionesha kushtuka baada ya kuelezwa na wananchi kwamba hakuna kiongozi yeyote aliyefika eneo hilo.

Akizungumza mbele ya umati wa watu waliokuwa wamefurika katika eneo hilo la tukio, Mbunge Wenje alisema: “Inashangaza sana kuona hata mkuu wa wilaya hajafika hapa. Nitawasiliana na viongozi wa serikali na mchana nitarudi hapa tena,” alisema Wenje aliyekuwa akitumia kipaza sauti.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mwandishi hapo sinai waliiomba serikali kuzuia wananchi kujenga karibu na miamba mikubwa, kwani kufanya hivyo itasaidia sana kuepusha maafa kama hayo, huku wakishauri watu wengine waache kukataza mawe hayo yavunjwe na watu wanayoyahitaji kwa ajili ya Ujenzi na shughuli zingne ila wananchi wa milimani wamekuwa wakikataza.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles