Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Rais Kikwete akutana na Makamu wa Rais wa kampuni ya Viettel Group Ikulu Dar

$
0
0

unnamed (33)

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Viettel Group ya nchini Vietnam Bwana Le Dang Dung ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro).

unnamed (34)

Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Juni 30, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka kampuni ya simu ya Viettel kutoka Vietnam ukiongozwa na Bwana Le Dang Dung ambaye ni Makamu wa Rais wa Kundi la makampuni ya Viettel Group.

Kwenye mkutano huo uliofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Bwana Dung amefuatana na Bwana Tao Duc Thang ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shughuli za Kimataifa za Kampuni hiyo – Viettel Global.

Bwana Dung amemwelezea Rais Kikwete kuhusu mipango ya Viettel kuwekeza katika shughuli ya mawasiliano ya simu hasa kwa maeneo ya vijijini.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles