Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Ufisadi, madawa ya kulevya na mauaji ya tembo vimewafanya waandishi kuacha kuandika habari za maendeleo – Muhanika

$
0
0

semina pic 1

Katibu Mtendaji wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Henry Muhanika akizungumza na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku pili mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mhadhiri kutoka Shule ya Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) Dkt Ayoub Rioba na Kulia ni Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa.

Na Damas Makangale, MOblog Tanzania

MATUKIO ya kihalifu kama vile ufisadi, rushwa, uigizaji na usafirishaji wa madawa ya kulevya na kukidhiri kwa mauaji ya tembo nchini pamoja na mambo mengine vimechangia vya kiasi kikubwa kwa waandishi wa habari kutoandika habari za maendeleo, MOblog inaripoti.

Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga na kugawa vyeti kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini walioshiriki mafunzo ya kujikinga na hatari wawapo kazini yalioandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC), Katibu Mtendaji wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT) Ndugu Henry Muhanika amesema kukidhiri kwa vitendo hivyo hasa vya ufisadi na mauaji wa tembo katika mbuga za wanyama kumechochea wanahabari kusahau habari za maendeleo.

“kutokana na kukidhiri kwa vitendo hivi kumewafanya waandishi na wahariri kuweka mkazo katika kuripoti matukio haya na kuwaacha wananchi bila taarifa sahihi na za wakati kuhusu maendeleo yao na nchi yao,” amesema Muhanika.

semina pic 3

Mgeni Rasmi, Katibu Mtendaji wa MOAT, Henry Muhanika akimkabidhi cheti mwandishi wa habari mwandamizi kutoka gazeti la ‘The Guardian’ Gerald Kitabu.

Amesema kimsingi habari za maendeleo zinatoa fursa kwa mwananchi hasa wa kijijini kujua kuhusu mfumuko wa bei, kipindi cha mvua katika nyakati za kilimo na kilimo nagni kinafaa kulimwa na mambo mengineo ya afya, elimu na ujasirimali.

Muhanika amesema lakini mafunzo hayo ya siku pili kuhusu waandishi wa habari kujikinga na viashiria vya hatari hasa wakati wa kufuatilia na kuandika habari za uchunguzi kwa mfano ufisadi au wawekezaji wanaodhulumu ardhi ya wananchi na kuchochea migogoro ya ardhi ni lazima wajue kujilinda kikamilifu na viashiria hivyo.

“ili kuweza kuripoti kwa kina mambo ya ufisadi ni lazima ujue kujilinda au kuripoti matukio ya kisiasa lazima ujue hata viashiria ili kuepuka yaliyowahi kuwatokea wakina Kibanda na marehemu Daud Mwangosi kule Iringa,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa amesema mtandao huo unafanya kazi mbalimbali zinazohusu utetezi, kujilinda, kujikinga na madhara au hatari zinazo sababishwa na ukiukwaji wa haki za binadamu.

semina pics2

Onesmo Olengurumwa akizungumza machache kabla ya kufungwa rasmi mafunzo hayo kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini.

“Mtandao wetu unajenga uwezo na kutoa mafunzo mbalimbali na njia mbalimbali za kujikinga na madhara yatokanayo na ukiukwaji wa haki za binadamu na katika eneo hili waandishi wa habari ni muhimu sana kupata mafunzo haya na tutaendelea kutoa mafunzo kama haya pindi tutapoona inafaa,” amesema Olengurumwa

Amesema kuwa waandishi wa habari majukumu yao yanaendana na haki zao pia zikiwemo haki ya kuwa huru dhidi ya uonevu au ukandamizaji.

“Nanyinyi mnatoka katika jamii zetu, mnafamilia na mnahitaji kuishi kwa amani kama watu wengine.

“Tafiti za kimataifa zinaonesha zaidi ya waandishi 70 wanauwa kila mwaka na wauwaji hao wanashindwa kuchukuliwa taratibu za kisheria. Vile vile zaidi ya waandishi wa habari mia moja wanavamiwa na kujeruliwa,”

 “Wakati umefika sasa kujitengenezea mazingira salama ya kazi na mbinu mbali mbali za kujikinga na kujilinda,” aliongeza.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles