Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mbunge ‘Zungu’ aishukia serikali dhidi ya machinga, boda boda, mama ntilie

$
0
0

   -awataka wabunge wengine wasije Dar es Salaam, wakae kwenye majimbo yao

zungu pics

Mbunge wa Ilala, Hassan Musa ‘Zungu’

Na Damas Makangale, Moblog Tanzania

MBUNGE wa Ilala,  Musa Hassan maarufu kama ‘Zungu’ leo asubuhi katika kikao cha Bunge la Bajeti kinachoendelea mjini Dodoma amekataa kuunga mkono Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu yenye makadirio ya kiasi cha shilingi trilioni tano.

Akizungumza kwenye kipindi cha  maswali na majibu ya ofisi ya Waziri Mkuu Bajeti ya  2014/2015, Mbunge Musa Hassan ‘Zungu’ amesema kwamba hataunga mkono bajeti ya ofisi hiyo kwa sababu haina kipaumbele kwa mkoa wa Dar es Salaam katika maswala ya miundombinu, kitengo cha maafa na maji.

“Mheshimiwa Naibu wa Spika kwa kweli siungi mkono bajeti ya ofisi ya waziri mkuu kama mambo kadhaa kama ya miundombinu, maji na utendaji mbovu wa baadhi ya wakurugenzi wa jiji kutumia madaraka vibaya na kuwaumiza wananchi ambao ni wapiga kura wetu,” amesema Zungu

Aliongeza kwa kusema kwamba kuna baadhi ya wabunge wamepiga kelele Dar es Salaam inapendelewa wakati miundombinu ya jiji hilo ni mibovu na wananchi wanateseka na mafuriko katika maeneo kadhaa bila msaada wa serikali.

“Na nyinyi wabunge mnaosema kwamba Dar tunapendelewa msije kabisa mkae huko mlipochaguliwa na wapiga kura wenu tusiwaone Dar es Salaam,” amesema Zungu huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge

Zungu amesema kuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam kuna baadhi ya watendaji hasa wakurugenzi wanajiamulia mambo na kuchukua ushuru katika sehemu mbalimbali huku wakisumbua wamachinga, boda boda na mama ntilie kwamba kuna sehemu ni smart areas.

Amesema kwamba hakuna smart areas kama sehemu kubwa la jiji kuna matope na barabara ni mbovu na kuzuia wafanyabiashara ndogo ndogo kushidwa kujitafutia riziki na kuendesha maisha yao ya kila siku.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles