Habari za kuthibitika kutoka chanzo chetu kinasema watu wasiofahamika wamerusha kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la mkono (Granade) kwenye Bar maarufu jijini Arusha inayofahamika kwa jina la Arusha Night Park iliyopo maeneo ya Mianzini.
Chanzo chetu kinasema kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa vibaya kutokana na mlipuko huo.
Tukio hilo limetokea wakati umati wa watu ukiwa umekusanyika kwenye Bar hiyo ukitazama mpira jioni hii.
MOblog inaendelea kufuatilia kwa ukaribu zaidi na tutaendelea kuwajuza kadri tunavyopata taarifa stay alert.
TAARIFA MPYA KUTOKA MILLARD AYO.COM INASEMA HIVI