Wananchi wakimuangalia mgambo wa Manispaa ya Ilala wakati akichukua magazeti katika moja ya meza Posta mpya jijini Dar es Salaam Aprili 3, 2014 Mkoa wa Dar es Salaam upo katika operesheni kabambe ya kusafisha jiji hilo kwa kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara ndogo ndogo maeneo yasioruhusiwa wilaya zake zote za Ilala, Temeke na Kinondoni.
Mgambo wa Manispaa ya Ilala akiwa amebeba magazeti.
Mgambo wa Manispaa ya Ilala akiwa amebeba magazeti wakivunja moja ya toroli la Kampuni ya TSN katika operesheni safisha jiji maeneo ya Posta mpya Dar es Salaam. Operesheni hiyo inafanyika mkoa wa Dar es Salaam kwa kuzihusisha wilaya zake zote za Ilala, Temeke na Kinondoni.
Mgambo wakiondoa kibanda cha Kampuni ya Simu Tigo.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi wakati wa oparesheni hiyo.
Eneo la Posta Mpya.
TUKIO LINGINE
Wafanya biashara wa Sitendi ya Daladala Mwenge jijini Dar es Salaam wakiwa hawana lakufanya wakiangalia zoezi la bomoa bomoa likiendelea.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi wakati wa oparesheni hiyo.
Mgambo akiondoa moja ya toroli eneo la Mwenge.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa kwenye doria.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwazibiti wafanya biashara eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM).