Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta(katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati namba mbili(2) jana mjini Dodoma alipotembelea Kamati hiyo kujionea maendeleo katika uchambuzi wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Shamsi Vuai Nahodha na Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda .
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta(kushoto) akizungumza na wajumbe wa Kamati namba tano(5) jana mjini Dodoma alipotembelea Kamati hiyo kujionea maendeleo katika uchambuzi wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ,Hamad Radhid Mohammed (katikati) na Makamu wake Assumpter Mshama(kulia).
Mwenyekiti wa Kamati namba 12 ya Bunge Maalum la Katiba, Paul Kimiti(katikati) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta(kulia) alipoitembelea Kamati hiyo jana mjini Dodoma kujionea kazi inayoendelea ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Thuwayba Kissasi.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta(katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati namba kumi na mbili(12) jana mjini Dodoma alipotembelea Kamati hiyo kujionea maendeleo katika uchambuzi wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya.Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Paul Kimiti (katikati) na mwingine ni mwingine ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Thuwayba Kissasi (KUSHOTO).