Mahakama ya Shirikisho la Ujerumani imesema kuwa sheria inayowapa punguzo la kodi watu walio katika ndoa ya mume na mke pekee yao ni kinyume cha katiba.
Mahakama hiyo iliyoko mjini Karlsruhe imesema kuwa watu walio katika ndoa ya jinsia moja pia wanapaswa kunufaika na punguzo hilo la kodi ambalo linatolewa kwa watu walio katika ndoa.
Kulingana na uamuzi huo, watu walio katika ndoa ya jinsia moja watanufaika na punguzo hilo na itahesabiwa kuanzia mwaka 2001 ambapo Ujerumani ilizitambua kisheria ndoa za jinsia moja.
Serikali ya Angela Merkel inayofuata sera za mrengo wa kulia kwa muda mrefu imekuwa ikipinga haki sawa kati ya ndoa kati ya mume na mke na zile za watu wa jinsia moja.