Wananchi wenye hasira nchini Bolivia wamemzika mtuhumiwa wa ubakaji na mauaji akiwa hai kwa kumtumbukiza katika kaburi la mtu aliyemuua.
Mtuhumiwa huyo Santos Ramos mwenye umri wa miaka 17, alitambuliwa na polisi wa Bolivia kuwa anaweza kuwa ndiye alihusika na kifo cha Leandra Arias Janco aliyekuwa na miaka 35.
Zaidi ya watu 200 waliamua kuchukua sheria mikononi, ambapo inaripotiwa kuwa walimkamata kijana huyo wakati wa mazishi ya mwanamke huyo aliyebakwa na kuuawa na kumzika pamoja nae.
Wanakijiji cha Colquechaca katika wilaya ya Potosi katika miinuko ya kusini mwa Bolivia, waliweka vizuizi barabarani kuwazuia polisi na waendesha mashita wasiingie eneo lililokuwa likifanyika mazishi hayo.
Shuhuda wa tukio hilo amedai kuwa Ramos alifungwa kamba kwanza kasha akatumbukizwa katika kaburi lililokuwa na mwili wa mwanamke aliyedaiwa kumuua na kasha kulifukia kwa udongo.
Matukio ya mauaji wakati mwingine hutoa katika maeneo ya vijijini na maeneo masikini ya Bolivia ambako hakuna hakuna ulinzi mkali wa polisi.