Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) yazindua wiki ya Mazingira kwa ngazi ya TRL.

$
0
0

mdd

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania-(TRL)  Kipallo Kisamfu akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam kwa ajili ya uzindizi wa wiki ya mazingira kwa ngazi ya TRL uliofanyika katika Stesheni ya Dar es salaam . Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu upande wa Kampuni hiyo ni Fikiri kabla ya kula: hifadhi mazingira kwa uchukuzi endelevu.

chairr

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Reli Tanzania( TRL) Severine Kaombwe akiwahutubia wanyakazi wa Kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa wiki ya mazingira ngazi ya Kampuni nchini kote ambapo kauli mbiu yao ni Fikiri kabla ya kula: hifadhi mazingira kwa uchukuzi endelevu.

stikka

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Reli Tanzania( TRL) Severine Kaombwe akionyesha baadhi ya stika ambazo zitabandikwa katika Mabehewa mbalimbali kwa ajili ya uhamasishaji wa utunzaji mazingira kwa abiria wawapo ndani ya treni . Mwenyekiti alionyesha stika hizo jana jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa wiki ya mazingira ngazi ya Kampuni nchini kote ambapo kauli mbiu yao ni Fikiri kabla ya kula: hifadhi mazingira kwa uchukuzi endelevu.

usafi

 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Reli Tanzania( TRL) Severine Kaombwe akishiriki zoezi la kusafisha maeneo ya Stesheni ya Dar es salaam  jana jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa wiki ya mazingira ngazi ya Kampuni nchini kote ambapo kauli mbiu yao ni Fikiri kabla ya kula: hifadhi mazingira kwa uchukuzi endelevu.

wafanyakazi

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania wakimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Reli Tanzania( TRL) Severine Kaombwe(hayupo katika picha) jana jijini Dar es salaam mara baada ya uzinduzi wa wiki ya mazingira kwa ngazi ya Kampuni hiyo.

zoezi

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania wakishiriki zoezi la usafishaji wa mazingira ya Stesheni ya Dar es salaam  jana jijini Dar es salaam mara baada ya uzinduzi wa wiki ya mazingira kwa ngazi ya Kampuni hiyo.(Picha na MAELEZO_Dar es salaam).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles