Mkurugenzi wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa bidhaa za LG, Tanzania, Rajesh Kumar (kulia) na Meneja Masoko wa LG, Shakti Vellu (kulia) wakizindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko la Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika duka lao lililoko Quality Center jijini Dar es Salaam.
Ubora wa Tv hii unaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja yani huku unaangalia TV na kutumia internet.
Bw. Valerian Banda ambaye ni msemaji wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa vifaa vya LG akiongea kuelezea ubora wa TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko la Tanzania.
LG imezindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania, TV aina ya OLED inayojikunja ni mwanzo wa burudani ndani ya nyumba. Aina yake ya kujikunja ambayo inaitwa IMAX inatupa uzoefu wa hali ya juu pamoja na kuangalia kwa starehe kubwa.
TV hii mpya aina ya OLED kutoka LG ikiwa na teknolojia ya rangi nne, ambayo kwa mujibu wa kampuni inaongeza pikseli nyeupe kwa rangi nyekundu, kijani na blu kwa mtazamo bora. Itakuwa na screen nyembamba aina ya OLED ambayo ukubwa wake ni 4.3mm. Pamoja na stendi yake ambayo ina vipimo ifuatavyo 1227x799x192mm na uzito wa kilo 17.2.
TV aina ya OLED LG namba 55EA9800 inakuja na idadi ya chaguo la kuunganisha ambayo ni HDMI port (x4), port ya kusikiliza muziki ( 3.5mm), RF, AV ( composite), port ya muziki, USB 2.0 (x2), USB 3.0 na LAN port.”
TV hii pia ina kitako ambacho ni wazi kama kioo ambacho TV huwa haionekani kama imeungana nacho na TV huonekana kama inaning’inia hewani. Pia TV hii imewezeshwa kuwa na muonekano wa spika tano kwenye kitako chenye LG 55EA9800 zenye uwezo waku toa sauti ya watti 40.
Bwana Rajesh Darji, wa Garnet Star Ltd Distributor wa LG Home Entertainment Products amesema“ Hii TV aina ya OLED inapatikana katika maduka makubwa ya LG na wakala wake.
Hii itampa mteja uonaji mzuri usiokuwa na mwisho. Burudani ya nyumbani imejazwa na mabadiliko yanayoendelea kila siku na sisi kama Kampuni ya LG ni kazi yetu kuwaletea bidhaa inayoendana na wakati huu”.
Mtengenezaji kutoka Korea ya Kusini amekaririwa akisema kuwa utendaji wa LG 55EA9800 una kasi mara mia zaidi ya TV zingine aina ya LED/LCD, ambayo inaweza kupunguza mwanga wa picha zinazo jionesha kwa kasi ya kioo cha TV.
Kampuni ya LG imeongeza rimoti ya ajabu yenye uwezo wa kupokea sauti na ishara mchanganyiko wa mambo mbalimbali.