Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Ofisi ya CAG yasaini makubaliano ya kusaidia miradi ya Kimaendeleo.

$
0
0

Ludovick-Utouh

Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Ludovick Utouh.

Na.Eleuteri Mangi- Maelezo

Tanzania kupitia Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imetiliana saini mkataba wa Euro 3,500,000 na Shirika la Deutsch Gesellschaft fü Internationale Zursammenarbeit (GIZ) la nchini Ujerumani ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 3,750,000,000/= za kitanzania kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza mbele  ya Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Ujerumani, Wafanyakazi wa NAOT na  waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam hivi karibuni Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali Ludovick Utouh amesema makubaliano hayo yanalenga kusaidia miradi iliyopo katika ofisi  yake.

 “Mara kwa mara ofisi yangu imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji hivyo makubaliano haya yataisaidia ofisi hii kufanya kazi kiufanisi zaidi na kwa kuzingatia weledi,” amesema Utouh.

Utouh alifafanua  kuwa ofisi yake ina jukumu kubwa na la  muhimu la kuhakikisha kuwa kuwa rasilimali za nchi zinatumika vema na kwa manufaa ya kila mtanzania hivyo fedha hizo zitatumiaka kwa manufaa ya nchi nzima.

Naye Mkurugenzi wa GIZ nchini Dkt. Regine Qalmann alisema shirika lake litaenelea kushirikiana na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania kwa nia ya kudumisha mihusiano yaliyopo  kati ya nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo kati ya Serkali ya Tanzania na Ujerumani yatadumu kwa muda wa miaka mine kuanzia mwaka huu wa fedha.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles