Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na sasa ni Waziri wa Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) akizungumza na watendaji wa wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri wake na sasa ameteulikuwa kushika nyadhifa ya Uwaziri Dkt. Seif Rashid (kulia), anayefuata ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Kebwe S. Kebwe.Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Waziri, wizarani hapo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Seif Rashid (kulia) akizungumza na watendaji wa wizara hiyo (hawapo pichani) na kutoa shukrani zake za dhati kwa aliyekuwa Waziri wake Dkt. Mwinyi kwa ushirikiano wake kipindi alipokuwa akiongoza wizara hiyo.
Naibu Waziri Dkt. Kebwe S. Kebwe akizungumza na watendaji wa wizara hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano na mahusiano mazuri ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Waziri wa Ulinzi Dkt. Mwinyi akiteta jambo na katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jami, Charles Pallangyo.
Mawaziri hao wakisaini vitabu vya makabidhiano ya Muundo na Utekelezaji wa Wizara.
Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Mwinyi akimkabidhi kitabu hicho Waziri Mpya wa Wizara hiyo Dkt. Seif.
Naibu Waziri Dkt. Kebwe, akikabidhiwa kitabu na Waziri Dkt. Mwinyi.
Mawaziri hao wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano pamoja na watendaji wa wizara hiyo. Wa kwanza kushopto waliokaa ni Katibu Mkuu, Charles Pallangyo, aliyekuwa Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt. Mwinyi, Waziri mpya wa wizara hiyo Dkt. Seif nna wa mwisho kulia ni Naibu Waziri Dkt. Kebwe S. Kebwe ( Picha zote na Catherine Sungura-MOHSW).