Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibaha Bi.Tatu Suleiman akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(mwenye shati Jeusi) makusudio yao ya kuendelea kuwasaidia vijana kuweza kukabiliana na changamoto za kimaendeleo na kumtaka Naibu Katibu Mkuu kusaidia kuratibu Mafunzo kwa vijana na viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya ya Ujasiriamali na umuhimu wa kuwanyajua vijana katika jamii,wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi.Halima Kihemba akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(mwenye shati Jeusi) juu ya Mikakati mbalimbali inayotekelezwa na wilaya yake ya kuwawezesha vijana ili waweze kujiajiri na kupiga hatua kimaendeleo,ambapo mafunzo mbalimbali ikiwamo ufugaji nyuki,kilimo cha umwagiliaji na shughuli za ujenzi yamekuwa yakiratibiwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana.
Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(hayupo pichani)kuendelea kusimamia utoaji asilimia tano (5%) ya mapato ya halmashauri kwa ajili ya kutumika katika shughuli mbalimbali za za maendeleo ya vijana,wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana.
Wajumbe Mbalimbali walioongoza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana.
Bweni la shule ya Sekondari ya Pangani lililojegwa na Vijana waliopata mafunzo kutoka Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Shughuli iliyoratibiwa na Mkoa wa Pwani ikiwa ni moja ya njia ya kuwawezesha vijana kujiimarisha kimaendeleo, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana.
Mwenyekiti wa kikundi cha TUAMKE akimwonesha Hassan Kibwana (katikati) akimwonesha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kushoto) Moja ya mizinga ya nyuki waliyofadhiliwa na wakala wa huduma za Misitu(TFS) ikiwa ni moja ya njia ya vijana hao kujiajiri na kuweza kuchangia shughuli za maendeleo nchini, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo katika Mkoa wa Pwani Kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana.
Baadhi ya Mizinga ya Nyuki inayosimamiwa na Kikundi cha TUAMKE kilichopo katika Mkoa wa Pwani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(mwenye shati Jeusi) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Ruvu.Kulia ni Mtendaji wa Kata ya Ruvu Bw.Yusuph Mzumeni,wakati alipotembelea Miradi ya Vijana katika vijiji vilivyopo katika kata hiyo Mkoani Pwani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(mwenye shati Jeusi) akiwaangalia vijana wajasiriamali wanaojishughulisha na utengenezaji wa Batiki alipotembelea Kikundi hicho katika kata ya Ruvu Mkoani Pwani.
Mwnyekiti wa kikundi cha WAJASIRIAMALI GROUP kilichopo katika kata ya Ruvu Bw.Paul Jonathan (kulia)akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kushoto) zawadi ya batiki alipotembelea Kikundi hicho Mkoani Pwani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akikagua shamba la bamia linalolimwa na vijana katika kata ya ruvu Mkoani Pwani.(PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO).