Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Tazama Simba wakiwa juu ya Mti katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Morogoro

$
0
0

Imezoeleka kuona Simba pekee ambao wanaweza kupanda juu ya Miti ni kutoka hifadhi ya Taifa ya Manyara. lakini hata hivyo kulikuwa hapajajulikana si hifadhi ipi nyengine ambayo Wanyama hao waliweza kuonekana wakiwa Juu ya miti..

Hivi karibuni mtandao  wa Maliasili zetu wakati wa safari zake za kutembelea baadhi ya hifadhi za Taifa ulibaini kuwapata Simba wengine katika Mbuga ya wanyama ya Mikumi wakiwa juu ya Miti.

Simba hao ambao walikuwa ni majike walikuwa wamepanda juu ya mti na kuanza kucheza huko kwa muda wa masaa zaidi ya mawili ambapo waliwaduwaza watalii wengi na kuwaacha waendelee kuwashangaa na kukatisha safari zao ambazo walikuwa wakizifanya kwa masaa yote hayo mawili. …

Hivi ndivyo ilivyo kuwa …

Simba wawili majike wakiwa wametulia wakitazama kwa umakini ni sehemu gani wangeweza kwenda kufanya mawindo yao .
Simba hao wakiwa wametulia 
Simba hao wakiendelea na michezo hapa wanasukumana na kutishiana kama wanataka kuangushana 
Kupanda wamepanda vizuri sasa hapa walikuwa wakihangaika watawezaje kushuka chini ya mti huo.
Simba hao wakiwa wanawashangaa watu mbalimbali waliokuwa wakiwatazama 
 
Simba mmoja akiwa amekasirika baada ya kutishiwa na mmoja wa watalii lakini alishindwa kuruka kutokana na mti kuwa mrefu.
simba hawa (8)
Katika mapozi
 
Wakiangalia windo kwa umakini
Bado wanatazama Windo 
Simba hao wakiwa wameanza tena Michezo 
 
 
Mmoja wa Simba hao akijaribu kutaka kuruka chini , lakini anaogopa 
 
 Watalii wakikwa Bize kuwashangaa Simba hao 
Hapa Simba hao wakiwa wanataka kuanza kushuka kutoka Mtini 
Hao wamepata akili na Kuanza Kushuka 
Mmoja wa Simba hao akiwa anashuka mtini , baada ya muda wa masaa mawili kuwepo hapo
Simba hao wakiwa wanashuka 
 
 
Kwa Muda wa masaa mawili Watalii walikuwa wametulia wakingoja Simba hao na kuwatazama wakicheza juu ya mti.
Sasa wanaondoka …..
 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles