Jinsi nguo hiyo inavyoweza kukataa kuingiza uchafu na kuzuia maji kuingia au kupenya ndani.
.Ni aina ya Silic (material) ina maelfu ya nyuzi zinazozuia uchafu wa aina yeyote
.Mashati hayo sasa kuingia sokoni kwa gharama ya Paundi 30 nchini humo
.Maji pia hayawezi kupita ndani
Na MOblog kwa msaada wa mtandao.
Kama wewe ni mvivu wa kufua nguzo basi mashati haya mapya na ya aina yake yatakufaa kwa sababu jinsi yalivyotengezwa yanaweza kuzuia uchafu na kimiminika chochote kwenye mwili wako na taratibu kusafisha aina hiyo ya kimiminika na vigumu kuweka doa.
Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, mbunifu wa nguo hiyo, Aamir Patel, amesema kuwa (material) ya nguo hiyo inaweza kujisafisha kwa uchafu wa aina yeyote hata kama ni soda ya Coca-Cola, nyanya, bia, wino au divai nyekundu.
Mashati hayo ambayo yana mchanganyiko wa kemikali mbalimbali kufanywa hivyo na kuwa sugu kwa aina yeyote ya uchafu wa rangi au kimiminika chochote.
Jinsi nguo inavyokataa uchafu na kuondoa kwa kutumia kemikali zake.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Patel kutoka San Francisco walifanya mfano kutumia dawa-ya kemikali, lakini bado shati hilo liliweza kuondosha uchafu kwa urahisi zaidi na Kisha ikaanza kutafuta njia za kuingiza teknolojia katika kitambaa ili kufanikisha utoaji wa uchafu.
Mwanafunzi huyo anasema pamoja na kuweka kemikali mbalimbali lakini shati hilo halipitishi maji hata tone na huwezi kusikia joto wakati wa kuvaa kwa sababu watu wanadhani aina ya nyuzi zake zinaweza kuleta joto.
“Ni aina ya shati ambao nimetumia kimekali mbalimbali kulitengeneza baada ya kugundua watu wanataka nguo ambazo hazipitishi maji wala uchafu wa aina yeyote na kuondoa gharama za ufuaji kwa mtumiaji,” amesema.